Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?

Nimemsikia Lissu akiyasema makubaliano yetu ya Tanzania na Dubai hayaoneshi kiwango cha uwekezaji utakaofanywa na mgawanyo wa mapato, akitumia hiyo kama moja ya sababu ya kuyaponda makubaliano tuliyoingia na Dubai kuhusu masuala ya uwekezaji.

Lissu anasema haya huku nikiwa na uhakika kuwa anapotosha kwa sababu najua kwa hakika kuwa anajua IGA au BIT ikiwa imetoa nafasi ya kuwepo kwa HGA haiwezi kuzungumzia uwekezaji husika na mgawanyo wa mapato kwa kuwa HGA ndo mkataba wa uwekezaji mahsusi ambao ndiyo unaoonesha aina ya uwekezaji, kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato.

Pili najua kuwa amesoma IGA yetu na Dubai na anajua imeeleza katika Ibara ya kwanza sehemu ya pili kuwa Kutakuwa na Mikataba Mahsusi ya Uwekezaji baina ya Tanzania na Dubai ambayo inaeleza haki na wajibu wa kila upande.
View attachment 2701848

Kwa kuwa najua Tundu Lissu yupo humu na nina uhakika atasoma huu uzi. Leo nataka atuambie humu.

Kuna IGA au BIT gani iliyowahi kuingiwa Duniani (POPOTE PALE) ambayo imetoa nafasi ya kuingiwa kwa HGA ( Mkataba mahsusi wa uwekezaji) alafu still ikaonyesha kiwango cha uwekezaji, aina ya uwekezaji na mgawanyo wa mapato?

Ninaweka ahadi apa! Endapo Tundu Lissu atajibu hili swali au mtu yeyote atajibu hili swali kwa ufasaha na kama nilivyouliza basi nitakuja na Verified ID humu.

Ifike kipindi sasa aache kuwadanganya watu kwa kuwa tu hawana uelewa wa mambo!

Tundu Lissu & Co nawasubiri humu.

Angalizo. Muje na Majibu sio longolongo.

Nawasubiri!!
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo

8.) Kwa nini zabuni ya uwezekezaji haikutangazwa? Kwa nini Mbarawa alidanganya kuwa Zabuni ilitangazwa?

9.) KWA nini walikaa na mkataba kwa miezi tisa kisha wakaupeleka bungeni kwa hati ya dharula?

10.) Kwa nini Zanzibar wameingia ubia na kampuni ya Global Logistics (AGL) kuendesha bandari zao na sio DPW na tena kwa miaka mitano tu?
 
Anzisha uzi wako uongelee hayo. Hapa limeulizwa swali linahitaji majibu. Ulichoweka hapa ni longolongo tu
 
China-Pakistan Economic Corridor (CPEC) walikubaliana ni uwekezaji wa zaidi ya dollar bilioni 46, thamani za mradi mmoja mmoja na pesa za miradi zitatoka katika vyanzo vipi.
 
China-Pakistan Economic Corridor (CPEC) walikubaliana ni uwekezaji wa zaidi ya dollar bilioni 46, thamani za mradi mmoja mmoja na pesa za miradi zitatoka katika vyanzo vipi.
Bwashee acha longolongo. Weka ushahidi kujibu swali kama lilivyoulizwa
 
🤣🤣🤣🤣 Naona upo hoi umechoka sana kwa kumtetea mama Samia. Kama kweli unampenda mshauri achutame mambo yameshaharibika
Kwa hiyo umekuwa msemaji wangu?

Mama Samia yupo vizuri na hadi sasa sioni shida yeyote kwake.

Kwenye suala la Bandari namwambia asonge mbele maana tumechelewa sana. asisikilize kelele za wajinga na wapotoshaji kama wewe na wenzako
 
Haya. Namtakia safari njema
 
Picha ya antena za Vodacom, Tigo, Airtel na TTCL zikiwa zimesimikwa kwenye mnara wa Helios baada ya makampuni haya kusaini mkataba wa upangishaji na Helios

Kuna mtu, Lord Denning, ameuliza swali lifuatalo: Je, kuna mkataba mithili ya IGA iliyosainiwa kati ya Tanzania na Dubai unaotaja gharama halisi za miradi kama vile bei ya huduma na kodi ya pango?

Jawabu kwa swali hili ni "ndiyo," na ufafanuzi ufuatao ni kwa ajili ya kuthibitisha hilo.

IGA na HGA ni mikataba mtambuka (framework ontracts)

Mikataba ya IGA na HGA ni mikataba mtambuka, yaani "framework contracts." Kimsingi, mkataba mtambuka unaweza kuwa na sura mbili.

Kwanza, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi unafahamika, kiasi kwamba ikishasainiwa HGA hakuna haja ya mikataba mingine.

Mfano mzuri ni ule mradi wa bomba la mafuta linalounganisha Tanzania na Uganda, yaani radi wa EACOP.

Pili, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi haufahamiki kikamilifu, kiasi kwamba, kushasainiwa kwa HGA hakuondoi haja ya mikataba mingine. Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu aina hii ya mikataba mtambuka:

Na tatu, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unatambuka miradi tofauti inayotekelezwa ndani ya nchi ile ile moja, lakini miradi hiyo inatekelezwa kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti na watekelezaji tofauti, lakini pasipo ulaiza wa kubadilisha sheria za nchi husika, kiasi kwamba kusainiwa kwa "Framework Contract" pamoja na "Project Contracts" kunaondoa mahitaji ya mikataba mingine, na hivyo kuondoa sababu ya uwepo wa IGA na HGA. Mchoro ufuatao unafafanua zaidi.

Mifano ya Mikataba mtambuka isiyohitaji IGA wala HGA

Hapa nchini, kuna mifano mingi ya "mikataba mtambuka" ya aina hii ya pili. Mikataba hii inaonyesha gharama halisi za miradi husika, hata kabla mikataba ya miradi husika kusainiwa. Mifano mizuri hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:
  1. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na kampuni ya Vodacom,
  2. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Tigo,
  3. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Airtel,
  4. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya TTCL.
  5. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Halotel.
Makampuni ya Halotel, Vodacom, Tigo, Airtel, na TTCL hutoa huduma za mawasiliano ya simu.

Lakini makapuni haya hayana mitaji ya kutosha kwa ajili ya kujenga minara nchi nzima.

MInara ya kurusha mawimbi ya sauti (signal relay stations) huhitajika kwa ajili ya kusimika antena za kupokea na kurusha upya mawimbi ya sauti kutoka kwa mpigaji hadi kwa mpokeaji.

Lakini, Helios ni kampuni ya Uingereza yenye mtaji wa kujenga na kukodisha minara kwa makapuni mbalimbali.

Helios wanamiliki minara zaidi ya 1000, katika Afrika mashariki na Kati. Hivyo, haya makampuni yetu yanakodisha nafasi kwenye minara ya Helios ili yaweze kuweka antena zao kwenye minara hiyo, na kuwahudumia wateja wake.

Kampuni inapoanza kukodisha nafasi kwenye minara ya Helios inakuwa haijui kwa uhakika inahitaji minara mingapi na iliyo wapi.

Kwa hiyo, busara ni kukodisha minara ya Helios kwa awamu, kulingana na wateja wanavyopatikana na wanakopatikana.

Hivyo, mchakato wa kuingia mkataba kati ya kampuni ya Helios na kampuni kama vile Vodacom inachukua hatua nne. Yaani:
  1. Kusainiwa kwa mkataba mtambuka mmoja (framework contract) wenye kutaja taarifa chache za jumla, zitakazoweka singi wa mikataba ya saiti moja moja katika siku za usoni.
  2. Kampuni yenye mahitaji kuiandikia Helios ikiomba huduma ya kukodishwa mnara kwenye site mpya.
  3. Kusainiwa kwa mikataba ya saiti maalum (site cocntract), na hivyo kuongeza idadi ya minara ya Helios iliyokodishwa kwa kampuni pale tu mahitaji ya kampuni yanapoongezeka kwa sababu wateja wapya wamepatikana.
  4. Helios kuandaa mnara kwenye saiti kulingana na mahitaji, na hatimaye kampuni kukabidhiwa saiti hiyo.
Kwa ujumla, mikataba mtambuka kati ya Kampuni ya Helios na makampuni yaliyotajwa hapo juu, inafanana katika muundo na maudhui.

KImsingi, kila "mkataba mtambuka" kati ya Helio na kampuni yoyote hapo juu, una sehemu zifuatazo:
  1. Maelezo ya msingi kuhusu makubaliano: Sehemu hii inaongelea wahusika katika mkataba, malengo ya wahusika, na mwongozo wa jumla kuhusu mahusiano ya siku za usoni.
  2. Kiammbatanisho cha kwanza ("schedule 1"): Kinaongelea "configuration", yaani aina ya huduma ambazo Helios anapaswa kuhakikisha zinapatikana kwenye kila saiti. Mfano:-- kuna sharti kwamba, kama mnara unaotaka kukidishwa uko sehemu ambako hakuna umeme wa gridi ya Taifa, basi Helios aweke jenereta; -- kuna sharti kwamba, kampuni itapewa ukubwa wa eneo la meta moja ya mmraba kwa ajili ya kusimika antena yake; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba tambuka; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba mahsusi utakaosainiwa katika siku za usoni; -- na kadhalika.
  3. Kiambatanisho cha pili ("schedule 2"): Kinaongelea kodi ya pango inayotajwa kwa kutumia kizio cha "TZS/site/month". Gharama hizi ziko katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yenye umeme wa gridi ya Taifa (bei nafuu). Na Kundi la pili ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya Taifa (bei kubwa).
  4. Kiambatanisho cha tatu ("schedule 3"): Kinaongelea muundo na maudhui ya mkataba utakaosainiwa kwa ajili ya kukidisha saiti moja tu, yaani kukodisha mnara mmoja pekee. Kwa hiyo, kama kampuni ya Vodacom itakodisha minara 100, kutasainiwa mikataba mahsusi 100.
  5. Kiambatanisho cha nne ("schedule 4"): Kinaongelea utaratibu wa kuongeza mnara mpya, yaani jinsi kampuni yenye mahitaji itakavyowasiliana na Helios na kuonyesha huduma ya mnara mpya ianze kutolewa lini.
  6. Kiambatanisho cha tano ("schedule 5"): Kinaongelea utaratibu wa kukabidhiana huduma kwenye saiti.
  7. Kiambatanisho cha sita ("schedule 6"): Kinaongelea protokali ya kutumia saiti, maana kwenye mnara mmoja kuna wakodishaji wengi. Yaani, unakuta kuna antena za Tigo, Airtel, Vodacom, na kadhalika.
Hakuna haja ya IGA kati ya Tanzania na Dubai

Baada ya kusema hayo hapo juu sasa nafanya majumuisho muhimu kwa kuzingatia hoja yafuatayo:

Njia mojawapo ya kusanifu hoja, ni kuanzia kwenye ufanano wa vitu viwili. Njia hii huzalisha hoja yenye muundo ufuatao:
  1. Kitu X na kitu Y vinafanana kwa sababu kila kimoja kinazo sifa a, b, and c.
  2. Kitu X pia kinaonekana kuwa na sifa nyingine d.
  3. Kwa hiyo, kitu Y pia kinapaswa kuwa na sifa hiyo d.
Kwa kutumia mantiki hiyo hapo juu, sasa nawea kukujibu kikamilifu kama ifuatavyo:

Mosi, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza na kammpuni ya DPW kutoka Dubai zinafanana kwa kuwa zote ni Kampuni za wawekezaji wa Kigeni wanaotaka mazingira tulivu ya uwekezaji ili wafanikiwe kuwekeza, kuvuna na kuhamisha faida kutoka nchini Tanzania, ambapo HELIOS anajenga na kuendesha minara kwa kuikodisha kwa makampuni yanayosafirisha mawimbi ya simmu hapa Tanzania, wakati DPW anajenga na kuendesha bandari za mmajini na nchi kavu kwa kuzikodisha kwa watu wanaosafirisha mizigo.

Pili, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza inao uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) na "mikataba ya miradi mmahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Uingereza.

Na tatu, kwa hiyo, Kampuni ya DPW kutoka Dubai inapaswa kuwa na uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) na "mikataba ya miradi mmahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai.

Yaani, timu ya Johari Hamza haikuwa na weledi katika mambo haya.

Hitimisho na mapendekezo

Mkataba mtambuka (framework contract) kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba kati ya nchi na nchi (IGA). Na mkataba wa saiti kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba wa ngazi ya miradi kati ya nchi mwenyeji na mwekezaji wa kigeni (HGA).

Kwa hiyo, inawezekana, na ni lazima, kutaja gharama za mradi kama vvile kodi ya pango na pia ukomo wa muda kwenye IGA.

Na kama ambavyo Helios na makampuni ya simu yanasaini "Framework Agreements" na baadaye "Project Site Agreements," vivyo hivyo DPW na TPA wanaweza na wanapaswa kusaini nyaraka za aina hii.

Hakuhitajiki IGA wala HGA kamwe ili kuiwezesha DPW au kampuni yoyote iwayo kuwekeza katika bandari za Tanzania!

Mama Amon Desk
"Summbawanga Town"
Sumbawanga.
30 Julai 2023.

Porojo ndeeeefu za kijinga, umeshindwa kujibu swali jepesi tu.

Ndiyo tuseme una macho lakini hayaoni au ndivyo mlivyozowea kuishi namna hiyo, mpaka mnafikia kujidanganya wenyewe? "Swali ni very simple", Tazama hata heading tu ya huu uzi, ndili swali lenyewe.

Naliruduai hapa, hapa hili bandiko lako refu wapi limejibu?

Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?​

Huna tofauti na wale mawakili wabovu na kina mruma waliokwenda kutuabisha ICSID.

cc: Anna Tibaijuka
 
Huna tofauti na wame mawakili wabovu na kina mruma waliokwenda kutuabisha ICSID.

cc: Anna Tibaijuka

1. Mtu anayesema anaielewa na kuikubali IGA ya DPW hawezi kuniambia kuwa na akili timamu nikakubali.

2. FaizaFoxy anasema kuwa anaielewa na kuikubali IGA ya DPW

3. Hivyo, FaizaFoxy hawezi kuniambia kuwa ana akili timamu nikakubali.
 
China-Pakistan Economic Corridor (CPEC) walikubaliana ni ushirikiano wa uwekezaji wa zaidi ya dollar bilioni 46, pia thamani za mradi mmoja mmoja midogo midogo na pesa za miradi zitatoka katika vyanzo vipi walionyesha.
Porojo ndeeeefu za kijinga, umeshindwa kujibu swali jepesi tu.

Ndiyo tuseme una macho lakini hayaoni au ndivyo mlivyozowea kuishi namna hiyo, mpaka mnafikia kujidanganya wenyewe? "Swali ni very simple", Tazama hata heading tu ya huu uzi, ndili swali lenyewe.

Naliruduai hapa, hapa hili bandiko lako refu wapi limejibu?

Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?​

Huna tofauti na wale mawakili wabovu na kina mruma waliokwenda kutuabisha ICSID.

cc: Anna Tibaijuka
 
1. Mtu anayesema anaielewa na kuikubali IGA ya DPW hawezi kuniambia kuwa na akili timamu nikakubali.

2. FaizaFoxy anasema kuwa anaielewa na kuikubali IGA ya DPW

3. Hivyo, FaizaFoxy hawezi kuniambia kuwa ana akili timamu nikakubali.
Wewe achana na ujinga wa "character assassination", jibu swali:

Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?​

Character ya Anna Tibaijuka ilishakufa alipoiba na kina Ruge wakishirikiana na benki ya kanisa. Yangu huwezi kuiuwa ipo JF peke yake.
 
Back
Top Bottom