Duh, Wabongo kwa kumbukumbu siwawezi.
Uliyesema kuhusu mashamba ya shule umenikumbusha miradi ya Elimu ya Kujitegemea (EK), sijui kama mashamba haya yapo hadi leo, maana Kapuya na Mungai wametuvurugia sana shule zetu hizi.
@Katibu Tarafa
Nakumbuka wakati wa kufunga shule tuoikuwa tunadundana sana mangumi, hata bakora sometimes. Yaani ilikuwa noma sana, kiasi kwamba kuna baadhi ya jamaa zangu walikuwa hawafiki shule siku ya kufunga, kwa kuhofia bifu za namna hii. Mambo ya LY yameniacha hoi!
@Msanii
Ni kweli enzi zetu kulikuwa na utaratibu kwa shule kuwapa msosi wanafunzi, sijui sasa. Hata hivyo nakupa pole kwa kusikitikia shule yako, kwamba miradi ya mashamba imekufa na kilichobaki ni uzio wa matofali. Nakuunga mkono katika kumtimua Mungai, na Kapuya pia. Hawa wawili ndio wameua kila kitu wizarani pale, we fikiria mtu na akili zake timamu anafuta UMISHUMTA/UMITASHUMTA. huku ndio kulikuwa na vipaji haswa vya kila kitu, iwe riadha, mpira, kwaya, utamaduni, kuruka viunzi, kurusha mikuki na kisahani nk.
@Gamba
Mchakamchaka upo kwa baadhi ya shule za vijijini, mie nilishuhudia mnamo mwaka 2005 watoto wakikimbia na kuimba nyimbo za Azimio la Arusha (kama lipo), na "Jua Lile Literemke".
Tunatoka mbali.