Tulipoambiwa watumishi hewa...

Tulipoambiwa watumishi hewa...

Dereva, mpishi, mfagiaji, messenger wakajiendeleze wawe na vyeti vya f4 ilihali mabosi wao mawaziri, maRC, maDC, MP wasimamiz wakuu wa serikali ktk ngaz husika wakiongoza wakuu wa idara nyetinyeti na kututungia sheria na kutupitishia mikataba kwa niaba ya taifa zima wao hata hicho cheti cha std7 sio lazma kuwa nacho ili mrad ajue kusoma kuandika na kuhesabu bas amequalify kuhodhi ofisi....
.
.
Wewe mama unaetetea huu ujinga acha kujidhalilisha wengne tunakuheshimu sana

Na hao wakagombee nafasi za kisiasa, kuna mtu aliwazuwia?

Sasa hivi kuna mtu nimesoma pm yake amenitumia anasema "Bi Faiza wasikusumbue hao, sasa hivi hata ukinunua Scania mpya ni lazima upeleke driver kampuni ya Scania kufundishwa namna ya kuitumia hiyo gari na ku diagnose, wengi wamefeli kwa kuwa tu hawaelewi screen inawapa maelezo gani".

Haya madereva mlio feli huko Scania jitokezeni mseme ukweli.
 
Punguza ushabiki, walipewa muda maarufu wa kujiendeleza.. Tokea wana ajiliwa
 
Tulipoambiwa "Watumishi hewa" tukashangilia sana, japo hatukuwaona
Wakaja waliofoji vyeti na kutumia "Vyeti fake" wakapugwa bila huruma, ndipo wengine tukahoji uhalali wa DAUDI Albert.

Limekuja la wenye elimu ya Darasa la saba, watu ambao waliajiriwa kwa Qualification hiyo, wanajua kuendesha magari, wanajua kufagia vyoo, wanapiga deki, na kweli wengi wanajua kututengea chai na chakula maofisini. Na leo hii tunaambiwa waondoke. Yaani kazi zao na Taaluma ya makaratasi wapi na wapi?

Unajiuliza Dereva ambaye aliajiriwa kwa cheti chake cha Darasa la Saba, na veta, ameendesha Gari la Mkurugenzi kwa Zaidi ya miaka mitanno bila kupata ajari, yaani hakuwahi kuiba mafuta, anaondolewa kazini, haambiwi hata hatima yake iwapo atalipwa chochote au lah.

Yupo mhudumu, mfagizi wa chooni, anajua sana kupiga deki, kama ilivyo kwa Dereva, naye Amefanya kazi takribani miaka kumi, ghafla anasitishiwa mshahara anaambiwa Ondoka ofsini, kabidhi kila kitu.

Anao watoto kibao, anaye mke ambaye naye hana kazi, Watoto wake wanasoma, yeye mwenyewe alipoanzisha kibiashara chake, alihamishwa kazi, kwahiyo hana hata kibanda cha kuuza mchicha, Naye ni Mtanzania, nasema si Mkimbizi, jiulize ingekuwa wewe.

Tunaposema haya mambo yakikufika ndipo utajua hali ilivyo ngumu na ngafu, tuendelee kusifu ili likitufika nasi tusimulie kama wenzetu.

Lakini katikati ya haya, unasikia eti Sifa ya Mkuu wa mkoa au Waziri haihitaji kuwa msomi wa kiwango kikubwa, yaani kwamba ati Nafasi zao ni za kisiasa. Wewe shangilia yanayowakuta wenzako, kwani hata hawa darasa la saba yanayowakuta, hawakujua kama itakuwa hivi. Kipindi yanawakuta wenye vyeti fake walidhani wako salama.

Sijafahamu kama hili agizo la Darasa la saba limetoka kwa Rais, nakumbuka Rais alisema "Mtu afanye kazi inayolingana na Taaluma yake" Najiuliza iwapo Udereva unahitaji taaluma kubwa Zaidi ya uendeshaji vizuri? Je Ufagizi au uhudumu unahitaji taaluma gani?

Anyway Yangu macho, na masikio nayatega kushuhudia mengi Zaidi. kwani ndo kwanza mwaka wa pili huu.

Fundi Mkuu
Waambieni wabunge wabadili sheria msilaumu watu walioapa kuilinda na kuitunza katiba bila kuogopa. Tumia bongo kidooogo utanielewa. Walaumu waliounda sheria hiyo. Angalia ulipojikwaa si vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?

Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.

Nawashauri walioishia darasa la saba wote wakipata fursa waende hata shule za watu wazima wakajiendeleze na masomo.
Mkuu usiseme hivyo kwakuwa hayajakufika Mtu anaendesha gari ya halmashaur imechoka Land Rover Tena manual unaniambia anahitaj elimu, ipi hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie wa darasa la saba mnaolalamika hapa mmeambulia nini?

View attachment 557086
View attachment 557087
Nilitaka tu dada yangu ninayeheshimu sana michango yako unisaidie kama hoja ni magari ya sasa yapo computerized. Kama hawa walioajiriwa baada ya 2004 hawawezi ku operate hayo magari kwa sababu yanatumia mifumo ya computer, je walioajiriwa kabla ya 2004 wanaweza kutumia hayo magari ambayo ni computerized?
 
Magari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?

Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.
Kufanya maamuzi yahusuyo mamia ya familia kwenye MKOA inahitaji kusoma na kuandika tu??? Ndicho unachojaribu kutueleza???

Kwamba kusugua choo na floor, kuendesha gari hizo unazosema COMPUTER CONTROLLED kuna hitaji elimu ya watu wazima?
 
image.jpeg
Hii nitafsirieni wa darasa la saba, or in this matter hata wa form IV za karibuni:
 
Magari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?

Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.

Nawashauri walioishia darasa la saba wote wakipata fursa waende hata shule za watu wazima wakajiendeleze na masomo.
pumba....... inawezekan huna cheti cha 4m4 ila unachet cha computer kizuri' huna cheti cha 4m4 ila kiingereza unakijua vizur sana mbona wapo wenye cheti cha 4m4 ila hawajui kusoma wala kuandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAMEONDOKA kazini watu waliofanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa wala serikali haikutambua michango yao. Msemo kwamba serikali haina shukrani hata uifanyie maajabu makubwa ikiamua utoke kazini unatoka. Mtu anashindwaje kuwa siyo muaminifu na mla rushwa akifikiria haya? Hao wenye elimu isiyotakiwa serikali inashindwa nini kuwapa elimu wabaki mpaka muda wao wa kustaafu waondoke kwa furaha? Kwa mtindo huu wengi wataondolewa kazini kabla ya muda wao wa kustaafu kwa kigezo cha elimu ndogo.Leo la saba kesho kidato cha nne si kitu.Elimu haina mwisho.
 
Huyo ni Muislam Ngumbaru tu...hana lolote

Yaani yeye ni kama Malaika ajuae kiiila kitu na kukosoa wanadamu ambao ndio sisi

Hakuna mtu anaudharaulisha uislam wenu hapa jamvini kama huyo FF

Mimi huwa natamani aje kuquote comment yangu nimbinue.

Tatizo anakimbia kimbia tu...!

Watakan...kata
True
 
Back
Top Bottom