Kibuyu Kazi
JF-Expert Member
- Jun 3, 2017
- 303
- 90
Hahahah[emoji38][emoji38][emoji38]twende tu tuliambiwa waliokua wanaishi kama peponi wataishi Kama mashetani
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Unamuheshimu huyu Kibibi?aumfahamu vizuri.Dereva, mpishi, mfagiaji, messenger wakajiendeleze wawe na vyeti vya f4 ilihali mabosi wao mawaziri, maRC, maDC, MP wasimamiz wakuu wa serikali ktk ngaz husika wakiongoza wakuu wa idara nyetinyeti na kututungia sheria na kutupitishia mikataba kwa niaba ya taifa zima wao hata hicho cheti cha std7 sio lazma kuwa nacho ili mrad ajue kusoma kuandika na kuhesabu bas amequalify kuhodhi ofisi....
.
.
Wewe mama unaetetea huu ujinga acha kujidhalilisha wengne tunakuheshimu sana
Umri umeenda ni bibi tumsamehe.Alafu anajifanya anajua uislamu,wakati yuko arogant kuliko maelezo,kutwa kujifanya grammar nazi/police.uislamu unatuhimiza ukarimu,kauli nzuri na huruma,lakini huyu mama hana vyote.
Vipi kuhusu wabunge na wakuu wa mikoa wasiokua na elimu yoyote?Magari ya siku hizi ni computer controlled, inatakiwa awe na uelewa wa kusomea na kuelewa maelekezo kwenye dashboard. Sasa darasa la saba la miaka hii si anafanya miujiza?
Hata jikoni siku hizi kama haujuwi kusoma na kuelewa Kingereza ni kasheshe.
Nawashauri walioishia darasa la saba wote wakipata fursa waende hata shule za watu wazima wakajiendeleze na masomo.
Mkuu ni bora umuheshimu cocochanel kuliko hyu bibi....Dereva, mpishi, mfagiaji, messenger wakajiendeleze wawe na vyeti vya f4 ilihali mabosi wao mawaziri, maRC, maDC, MP wasimamiz wakuu wa serikali ktk ngaz husika wakiongoza wakuu wa idara nyetinyeti na kututungia sheria na kutupitishia mikataba kwa niaba ya taifa zima wao hata hicho cheti cha std7 sio lazma kuwa nacho ili mrad ajue kusoma kuandika na kuhesabu bas amequalify kuhodhi ofisi....
.
.
Wewe mama unaetetea huu ujinga acha kujidhalilisha wengne tunakuheshimu sana
Hawezi kuridhika mpaka atapoona mashetani yametapakaa mtaani........Tulipoambiwa "Watumishi hewa" tukashangilia sana, japo hatukuwaona
Wakaja waliofoji vyeti na kutumia "Vyeti fake" wakapugwa bila huruma, ndipo wengine tukahoji uhalali wa DAUDI Albert.
Limekuja la wenye elimu ya Darasa la saba, watu ambao waliajiriwa kwa Qualification hiyo, wanajua kuendesha magari, wanajua kufagia vyoo, wanapiga deki, na kweli wengi wanajua kututengea chai na chakula maofisini. Na leo hii tunaambiwa waondoke. Yaani kazi zao na Taaluma ya makaratasi wapi na wapi?
Unajiuliza Dereva ambaye aliajiriwa kwa cheti chake cha Darasa la Saba, na veta, ameendesha Gari la Mkurugenzi kwa Zaidi ya miaka mitanno bila kupata ajari, yaani hakuwahi kuiba mafuta, anaondolewa kazini, haambiwi hata hatima yake iwapo atalipwa chochote au lah.
Yupo mhudumu, mfagizi wa chooni, anajua sana kupiga deki, kama ilivyo kwa Dereva, naye Amefanya kazi takribani miaka kumi, ghafla anasitishiwa mshahara anaambiwa Ondoka ofsini, kabidhi kila kitu.
Anao watoto kibao, anaye mke ambaye naye hana kazi, Watoto wake wanasoma, yeye mwenyewe alipoanzisha kibiashara chake, alihamishwa kazi, kwahiyo hana hata kibanda cha kuuza mchicha, Naye ni Mtanzania, nasema si Mkimbizi, jiulize ingekuwa wewe.
Tunaposema haya mambo yakikufika ndipo utajua hali ilivyo ngumu na ngafu, tuendelee kusifu ili likitufika nasi tusimulie kama wenzetu.
Lakini katikati ya haya, unasikia eti Sifa ya Mkuu wa mkoa au Waziri haihitaji kuwa msomi wa kiwango kikubwa, yaani kwamba ati Nafasi zao ni za kisiasa. Wewe shangilia yanayowakuta wenzako, kwani hata hawa darasa la saba yanayowakuta, hawakujua kama itakuwa hivi. Kipindi yanawakuta wenye vyeti fake walidhani wako salama.
Sijafahamu kama hili agizo la Darasa la saba limetoka kwa Rais, nakumbuka Rais alisema "Mtu afanye kazi inayolingana na Taaluma yake" Najiuliza iwapo Udereva unahitaji taaluma kubwa Zaidi ya uendeshaji vizuri? Je Ufagizi au uhudumu unahitaji taaluma gani?
Anyway Yangu macho, na masikio nayatega kushuhudia mengi Zaidi. kwani ndo kwanza mwaka wa pili huu.
Fundi Mkuu
Hiyo habari ilinipita, ila mpaka serikali ifikie maamuzi ya kuhamia kwenye gari hizo nafikiri hata hao wazee wa darasa la saba watakuwa waneshajiendeleza kielimu na wengine watakuwa wameshastaafu, wangeweza kuondolewa taratibu.Huelewi kuwa moja ya washirika wa Tesla wamepewa ardhi kubwa sana ya madini ya kuundia battery za hizo gari?
Jisomee: Ahsante Kikwete, utajiri mpya Tanzania
Alaaaaa kumbe huyu ndio wale wale kina cocopapuchi na nanyapiMkuu ni bora umuheshimu cocochanel kuliko hyu bibi....
kiingereza cha nini mbona china wanapetaKupika mtori lazima ujue kiingereza? Kupika makongoro nako ujue kiingereza?
Huyu ndio mama yao..Alaaaaa kumbe huyu ndio wale wale kina cocopapuchi na nanyapi
Huyo ni Muislam Ngumbaru tu...hana loloteAlafu anajifanya anajua uislamu,wakati yuko arogant kuliko maelezo,kutwa kujifanya grammar nazi/police.uislamu unatuhimiza ukarimu,kauli nzuri na huruma,lakini huyu mama hana vyote.
Sipendi nikupoteze..tembea taratibuila katika hili ni upuuuzi wa kiwango cha juuu
Mambo ya sasa hayo si ya miaka ijayo. Hata sasa hivi ukiitaka tesla unanunuwa. Na zipo nyingi zaidi ya tesla.Hiyo habari ilinipita, ila mpaka serikali ifikie maamuzi ya kuhamia kwenye gari hizo nafikiri hata hao wazee wa darasa la saba watakuwa waneshajiendeleza kielimu na wengine watakuwa wameshastaafu, wangeweza kuondolewa taratibu.
Kuna familia moja watu wanne 4 wameachishwa kaziSio siri anajichumia DHAMBI KUBWA kwa Mwenyezi Mungu.
Nilienda wilaya moja majuzi na kumkuta Mzee aliyekuwa dereva wa Halmashauri amefukuzwa kazi na binti yake aliyekuwa masjala naye pia akatumbuliwa wakati kazi yake ilikuwa ni kuwajuza tu watumishi yalipo mafail yao na kuwaletea baas.
Yule mzee alikaribia kulia mbele yangu.