Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

NILIOKOLEWA NA JIRANI NA WAZUNGUView attachment 1426951

Mimi ilikua siku nikiachwa mwenyewe nyumbn basi hio ndio siku ya kujaribu mengne yote ambayo nakatazwaga,

Siku moja hv wakubwa wote wakaenda shamba kuvuna mahindi nikaachwa mwenyewe, wakati wanaondoka Mama akaniambia "Leo usipotulia litakalo kupata utajisaidia mwenyewe maana kambini watu karbu wote leo wanaenda shamban kuvuna mahindi" (tulikua tunaish kwenye kambi za maliasili na utalii na ipo isolated na vijiji vingne) mtoto wa mamkubwa akacheka akasema "leo sijui tutakuta kituko gani?"

maana wiki iliyopita nilikutwa nimelala kwenye maua baada ya kupanda juu ya bati na kujitia fundi wa antena nikashuka nayo, nilipo angukia ndo hapo hapo nilipokutwa nimejikunyata, wapita njia walikua wananiona ila hawakujua kama nimepattwa na tatzo maana hapo hapo mbuzi wakaja kujilaza kwa kunizunguka, jiran baada ya kuona mbuzi wameondoka wamekuja kuku mimi bado nipo ndo akapigwa na machale akaja kunibeba akanipeleka dispensary,

Sasa basi, baada ya bimkubwa kunipa onyo wakasepa, nikanywa kwanza chai, wakati anaongea vile nilikua nasubr tu amalize lakn kichwan nishapanga leo lazima nijifunze baiskeri.

Nikaenda stoo nikachomoa mphoenix nikakokota mpk barabarani, mimi raha yangu nikokote mpk kwenye mteremko/kilele cha mlima halaf nipande inishushe then nikokote tena nirudie,

Nikaenda mara ya kwanza safi tu, mara ya pili niliumia kdg matakoni baada ya kujibamiza kwenye ule mtalimbo unaounganisha sterring na kiti maana nilikua sikai kwenye kiti ili nifikie sterring na pedal vizuri(tulikua tunaita kuisimamia),

Mara ya tatu ndo kimbembe sasa,
Kwa sbb nilishajihs kuweza mzee nikashuka kwa kasi huku nimekaa kwenye kiti, kitu kikaanza kuyumba, speed ikaongezeka zaid, break nikashndwa kushika maana siwez kutanua vidole nizifikie na nikilazimisha napoteza balance maana huku nyuma nako kiti nimekikalia pale kwenye ncha(pale wanaposema panawatoaga wanawake waendesha baisker bikra) huku nimeinamia sterring,
ule mlima n mrefuu mpk ufke chini, chini ikawa inapanda gari ya watalii wanaenda kule kambini kuchukua kibali ofisini ili waingie porini huku wanachukua video, wakaniona nashuka kwa kasi sanaa ikabd wao ndo wanikwepe,
Sasa pale mwisho wa mlima pana kona kali, juu kuna mto/bwawa kubwa lenye kina hasa, then karavat mbili kubwa hasa, chini maji yanakoshukia ni maporomoko kwenye maweee makubwa na pembeni chaka la miba.

Kona nilijua niwazi kbsa sitaweza kukata na nikilazimisha tuu zile moramu pale chini na mawe mali yangu,

Nikawaza kule juu kwenye bwawa nitakufa bila hata kuonekana nyama, kwenye karavati jinsi yalivyo makubwa na nikisikia yale maji yanavyofoka sikutaka hata kuwaza, kule chini yale maporomoko ndio hata hilo wazo halikunijia, option ikabakia kwenye chaka la miba(miba flan hv mifupi imejikunja halaf inawasha sana ikikuchoma),

Nikalifakamia bwanaaaaa, niliingia mpk kati kati ya lile biwi kubwa la miba, huko ndani kulikua na vicheche, bundi, kware, wanyama flani hv wananuka sana na wale wanaopenda kujisaidia sehem moja hata wakienda mbali watarud pale n.k wote walitoka nduki kila yule kwa mlio wake, nilibananishwa na miba ukijitikisa tu kdg inakuchoma,
kumbe wale wazungu walipigwa na machale, walipaki gari wakarud kuniangalia, wakanikuta nimejaa damu hata kulia siwezi maana nikitanua mdomo tuu nakutana na miba inazidi kupenya, ikawa naangusha tu machozi na migunoo,
mmoja akaenda kwenye gari kuchukua vifaa wakatumia zaid ya masaa mawili kunitoa mule ndani ya lile biwi la miba bila kuniumiza zaidi, wakanipa huduma ya kwanza(walikua na vifaatiba ving),

Wakanipeleka ofisini,
huko tukamkuta mzee na wafanyakaz wenzake, nimejaa ma bandage ofce nzima wakaanza kuitana "jaman njooni mmuone ..... Tena Huku, ya leo kalii"
Yaani baada ya kusununika watu hoi kwa vicheko maana washanizoea sasa,
hapo naonekana tu kijimdomo na macho tu, wale wazungu wakawa marafk zangu kuanzia pale mpk wanaondoka, wakaniachia bonge ya Nokia na PC, niliwashwa siku tatu, kuanzia pale ikawa kuachwa nyumbn mwenyewe n mwiko.
In asubuhi ila nimecheka mno has a hapo ukitanua mdomo unachomwa so unabaki kimya..I believe uliacha utundu kuanzia siku hiyo
 
Mimi kaburi liliniita kabisa.
Kifo kilitaka kunimeza...

Kipindi nasoma tulikuwa na masomo ya jioni ...tukitoka saa8 mchana muda wa lunch ,tunaingia saa 10 ,,hapo kutoka saa12..
Nilikua na utararibu wa kurudi nyumbani kwenda kula chakula ili kupunguza gharama za kula shule.
Pia nyumbani ilikua karibu sana Kama dk 5 tu kwa gari nakuwa nimefika.
Kwa hiyo kwenda na kurudi nilitumia sh300.
Nikawa napumzika then saa 10 kasoro narudi shule.

Ikafika siku yangu..
Kama kawaida yangu..wakati narudi shule niligongwa na gari katika harakati za kuvuka barabara....
Ilitokea gari iliovertake ghafla ikaja kunipiga..nilikuwa naelekea mwisho kabisa ..ilinipiga ikanitoa nje kabisa.
Ilikwapua mguu wangu ,,ikaondoka na soksi...nguo zote chakachaka..na zilikuwa mpya maana ilikua mwanzo wa mwaka tu.
Nilijipiga kichwa chini...nikachika Mdomo,Kuna kipande Cha jino kilikatika na juu ya jicho.
Jamani ajali isikie kwa Mtu..isiwe kwako.
Nilizima pale chini dk chache,,

kulikuwa Kuna gari ya magereza pembeni..wakanibeba wakisaidiana na baadhi ya wanafunzi wenzangu.
Kwenda hospital damu zinanimwagika tu pale...nikapitilizishwa kwenye msaada wa haraka.
Kusafisha vidonda yaani niliona dunia inafika mwisho...Yale maumivu niliyoyapata.
Wakaniuliza km nakumbuka namba za ndugu zangu.
Nimeksriri namba ya mama kuliko nyingine zote..nikataja..
Kumpigia mama anastuka anashangaa.,na mama yangu alikua akiishi wilayani huko,huku nilikua naishi na dada.wakamwambia mwanao yupo hsp ya rufaa...
Mama akampigia dada..dada kupanda gari..akajua niliumia kidogo..akawa anaenda shule..
Haijafika mbali akakuta mama anamwambia eti mtoto Yuko rufaa
Alishuka hakumlipa konda nauli

Kufika pale Niko hoi bin taaban nasubiri kwenda x Ray..wapige kichwa mkono na mguu.
Na kipindi hicho madaktar walikuwa na mgomo,shemeji alikua anafahamiana na mtu wa x-ray..hatukupata shida...

sikulazwa nilirudi home..
Kule wazaz wakafunga safari kuja.
Jamani kuugua vidonda usiombe

Baada ya siku 2 walikuja wale walionigonga..walienda kuuliza shule wakaelekezwa.
Walikuwa bega kwa bega na wazaz Hadi nilipo pona

Ila namba niliisoma vema.
Mwezi mzima sili,sitembei,sioni,siongei.
Kiuno kiliteguka,mguu haufunction,usoni ndio usiseme... nilikua km yule mama kwenye Avatar ya Zero IQ

12.02.2012 hii siku siisahau
Duuh pole Saint..hakika Mungu ni mwema siku zote
 
hii sasa ilikua funga kazi japo mwanzo wake ilikua kam utan na kwa waliosoma shule ya msingi mbata mbeya mjin watakua wanakumbuka (hasa mtot wa meya wa mbeya enzi izo (meya alikua anaitwa kapunga) ndo alikua msaada kwangu kwan tulikua tunakaa mtaan mmoja uitwao nonde

Ilikua siku ya ijumaa na kwa taratibu za shule waislamu wanaruhusiwa kwenda kuswali na wengine vipindi vinaendelea kam kawaida

Tuendelee

2.Kuna mwalimu alikua mkal san sasa akawa amekuja kupiga biti na akawa anasema "leo adhabu ntakazowapa hamatakuja sahau" kwan kuna makosa tulifanya jana yake (ila sikumbuki ni makosa gan).baada ya hapo akawa ametoka kwenda kutafuta fimbo

Basi bwana ujuaji mwingi + utundu nikaruka dirisha ili nitoroke zangu. Yaan ata sielewi kilitokea nin kwan mpak kesho nashindwa kueleza vizur ila nilipokuja kutua chini nikawa nimekatika ulimi na kubaki kipande kidogo san kinachounganisha (apa niweke sawa, kam ushawahi kata nyama basi unakata alaf hautenganishi kabisa yaan unaacha kipande kimoja cha nyama kiungane na kingine)

Ninachokumbuka kidogo ni kuna kitu chenye ncha kilinichoma kidevuni ila kidg saan na nikajigonga kidevun pia .kutokana na kujigonga meno yakaenda kung'ata ulimi na kuchana kabisa

Wakati kitendo kinatokea kumbe yule mtot wa meya aliniona na alikua mkubwa kidg kwangu ndo kwenda kutoa taarifa om.

Basi nikapelekwa hospital iliopo karibu apo apo inaitwa 'kiwanja mpak' (wenyeji wanaifahm).ila wakasema tatiz ni kubwa nikapelekwa moja kwa moja hospitl ya rufaa ya mbeya. Kila daktari alishangaa imekuaje ila hawakuweza kupata jibu kwan muhusika siwezi kuongea kwa wakati huo.

Kumbuka ulimi umekatika kiasi kwamba nikifumbua mdomo basi lazima ulimi nishike na mikono kwan kipande kilichobaki kimeshikwa na ngozi ndogo san (alaf cha kushangaza sikua nasikia maumivu yoyote yale)...kila daktari akawa ansema wazi wazi ili tatizo kubwa na anaweza akawa bubu kabisa apo mama analia balaa kwan mim ndo jembe lake la kwanza.

Kuna mama mmoja (daktari ) akasema najitolea kumshona ila tuwe tayar kwa chochte kitakachotokea kwan hajwah kutana na kitu kam icho (huwa namshukuru mpak kesho yule daktar). Nikashonwa na kupona kabisa ila effect yake nikawa na saut ndogo saan ukilinganisha na umri wangu.

Nashukuru nimepona kabisa saiz nipo fresh san
Kwanza pole sana mkuu

Sauti yako ni ndogo sana au kubwa?
 
wale ambao utotoni tuliugua hadi wazazi wakakata tamaa tunacomment wapi??

Mimi niliumwa hadi wazee wakaamua kunibadilishia jina na mwezi wa kuzaliwa hadi leo jina lililopo kwenye birth certificate ile inayotolewa mwanzoni hospitali na niliyo nayo sasa ni tofauti kuanzia jina hadi mwezi ingawa najua nilizaliwa mwezi wa 3 ila birthday yangu ni mwezi wa 4 wakuu acheni tu
Ilikuwaje hii mkuu
 
Kaka yangu alikua na kigugumizi tulivyokuwa wadogo alikua anapenda kunikorofisha(tumefuatana) ..nikasikiaga ukimfunikia ungo mtu mwenye kigugumizi wakati anaongea anakosa pumzi..siku yake ikafika Bana alinikorofisha nikasema dawa yako inachemka.

Nikambamba siku hiyo anaongea Tena alikua ananiongelesha kwa ugomvi nikakumbuka ungo nikaingia ndani nikachukua ungo vile anaendelea kuongea nikafunika alianza kukata kuongea ametoa tu mimacho ana hema kwa shida Mama anatoka nje ananikuta nimefunika ungo na mwanae ahemi akaniambia wewe utamuua Kaka yako akawahi kufunua ule ungo.

Tangu hapo akunichokoza tena
 
Unajua kuna wakati unakua mtundu hadi wazazi ndugu wanakususa hawataki hata kusikia jina lako maana wamechoka habari zako.

Hiyo hali ilinikuta mimi maana nilikua troublemaker tabia zote mbaya zangu sio wizi,mademu,bangi,nk yani zoteee kilichonisaidia ni wazazi wangu hawakufikia roho mbaya ya kunipeleka gerezani japo mjomba angu alikua akiwasisitiza kila siku huyu tukamfunge akae magereza hata mwaka tu ila wazazi wangu hawakumsikiliza.

Kwa ukorofi wangu nilipiga demu mmoja alikua mpenzi wangu,nilimfumania red handed geto kwa msela...Nilianza kupiga Jamaa plus dem maana nilikua na Panga,nilipiga wale watu ndani,bahati mbaya yule jamaa akanishnda nguvu akachoropoka Ndukiiii,Nikabaki na dem wangu asee nilipiga yule dada alipiga ukunga hadi sauti ilikata.,Baada ya kuridhika na kumchakaza nikatoka na panga langu lina damu nikasepa.

Si unajua bangi mbaya bwana,,,bangi ilipokata akili ikanirudia nikagundua kua nilimpiga sana yule mdada kiasi kwamba hata uhai wake ulikua mashakani,nikaamua kukimbia nyumbani kabisa maana nilijua lazima kesi ifike polisi,na kweli ikawa vile.

Baada ya kukimbia hapo sina mbele wala nyuma,nikageuka mtoto wa mtaani nalala nnche nazurura yani Full kuwa mtoto wa ajabu ajabu yani,siku moja nikasema HAPANA hii imefika mwisho siwezi teseka kiasi hiki bora nife mimi,basi nikatafuta kamba nikasema ni bora nikajiua..Usiku nikazurura kwenye nyumba za watu nikakuta Kamba ya kuanikia nguo imefungwa imeanikwa nguo..Nikatoa nguo zote nikatupa chini,nikafungua Kamba nikasepa nayo.

nilipopata kamba yangu nikasema hapa ngoja nilale hlf kesho ntatafuta mti porini ulioimara nikajitundike,pakakucha kesho yake nikazama porini nikatafuta mti nikauona..nikaenda kufunga kamba huku nalia peke angu,Nikajifunga kamba nikajiachia BWANA BWANA BWANA BWANA sikuweza vumilia yani shingo ilikua inakatika,nilibembea na ile kamba nataka nijiinue juuu kamba inateleza Jamani natamani nielezeee mnielewe lakini sijui.

Nilikukuruka kamba ndio inazidi kunikaba Mungu si athumani sijui nini kilitokea nikajikuta nimedondokea mgongo kwenye jiwe,Ndio ikawa pona yangu ila koo liliniuma mwezi mzima nikawa siwezi meza hata Mate...

Sikieni tu Mtu kajinyonga...
Asee nimecheka hadi nimepaliwa
 
Unajua kuna wakati unakua mtundu hadi wazazi ndugu wanakususa hawataki hata kusikia jina lako maana wamechoka habari zako.

Hiyo hali ilinikuta mimi maana nilikua troublemaker tabia zote mbaya zangu sio wizi,mademu,bangi,nk yani zoteee kilichonisaidia ni wazazi wangu hawakufikia roho mbaya ya kunipeleka gerezani japo mjomba angu alikua akiwasisitiza kila siku huyu tukamfunge akae magereza hata mwaka tu ila wazazi wangu hawakumsikiliza.

Kwa ukorofi wangu nilipiga demu mmoja alikua mpenzi wangu,nilimfumania red handed geto kwa msela...Nilianza kupiga Jamaa plus dem maana nilikua na Panga,nilipiga wale watu ndani,bahati mbaya yule jamaa akanishnda nguvu akachoropoka Ndukiiii,Nikabaki na dem wangu asee nilipiga yule dada alipiga ukunga hadi sauti ilikata.,Baada ya kuridhika na kumchakaza nikatoka na panga langu lina damu nikasepa.

Si unajua bangi mbaya bwana,,,bangi ilipokata akili ikanirudia nikagundua kua nilimpiga sana yule mdada kiasi kwamba hata uhai wake ulikua mashakani,nikaamua kukimbia nyumbani kabisa maana nilijua lazima kesi ifike polisi,na kweli ikawa vile.

Baada ya kukimbia hapo sina mbele wala nyuma,nikageuka mtoto wa mtaani nalala nnche nazurura yani Full kuwa mtoto wa ajabu ajabu yani,siku moja nikasema HAPANA hii imefika mwisho siwezi teseka kiasi hiki bora nife mimi,basi nikatafuta kamba nikasema ni bora nikajiua..Usiku nikazurura kwenye nyumba za watu nikakuta Kamba ya kuanikia nguo imefungwa imeanikwa nguo..Nikatoa nguo zote nikatupa chini,nikafungua Kamba nikasepa nayo.

nilipopata kamba yangu nikasema hapa ngoja nilale hlf kesho ntatafuta mti porini ulioimara nikajitundike,pakakucha kesho yake nikazama porini nikatafuta mti nikauona..nikaenda kufunga kamba huku nalia peke angu,Nikajifunga kamba nikajiachia BWANA BWANA BWANA BWANA sikuweza vumilia yani shingo ilikua inakatika,nilibembea na ile kamba nataka nijiinue juuu kamba inateleza Jamani natamani nielezeee mnielewe lakini sijui.

Nilikukuruka kamba ndio inazidi kunikaba Mungu si athumani sijui nini kilitokea nikajikuta nimedondokea mgongo kwenye jiwe,Ndio ikawa pona yangu ila koo liliniuma mwezi mzima nikawa siwezi meza hata Mate...

Sikieni tu Mtu kajinyonga...
Badae ikawaje sasa mkuu? Ukarudi home?
 
Na kweli nilivyouachia kidogo anivamie bila mama kuwepo pale ningebutuliwa vibaya mno
Yaaan unamfunika kichwani?

Ngoja kuna kimkaka kina kigugumizi nishakiambia sikitaki kinang'ang'ania ntakifunika nione
 
Back
Top Bottom