Mimi kaburi liliniita kabisa.
Kifo kilitaka kunimeza...
Kipindi nasoma tulikuwa na masomo ya jioni ...tukitoka saa8 mchana muda wa lunch ,tunaingia saa 10 ,,hapo kutoka saa12..
Nilikua na utararibu wa kurudi nyumbani kwenda kula chakula ili kupunguza gharama za kula shule.
Pia nyumbani ilikua karibu sana Kama dk 5 tu kwa gari nakuwa nimefika.
Kwa hiyo kwenda na kurudi nilitumia sh300.
Nikawa napumzika then saa 10 kasoro narudi shule.
Ikafika siku yangu..
Kama kawaida yangu..wakati narudi shule niligongwa na gari katika harakati za kuvuka barabara....
Ilitokea gari iliovertake ghafla ikaja kunipiga..nilikuwa naelekea mwisho kabisa ..ilinipiga ikanitoa nje kabisa.
Ilikwapua mguu wangu ,,ikaondoka na soksi...nguo zote chakachaka..na zilikuwa mpya maana ilikua mwanzo wa mwaka tu.
Nilijipiga kichwa chini...nikachika Mdomo,Kuna kipande Cha jino kilikatika na juu ya jicho.
Jamani ajali isikie kwa Mtu..isiwe kwako.
Nilizima pale chini dk chache,,
kulikuwa Kuna gari ya magereza pembeni..wakanibeba wakisaidiana na baadhi ya wanafunzi wenzangu.
Kwenda hospital damu zinanimwagika tu pale...nikapitilizishwa kwenye msaada wa haraka.
Kusafisha vidonda yaani niliona dunia inafika mwisho...Yale maumivu niliyoyapata.
Wakaniuliza km nakumbuka namba za ndugu zangu.
Nimeksriri namba ya mama kuliko nyingine zote..nikataja..
Kumpigia mama anastuka anashangaa.,na mama yangu alikua akiishi wilayani huko,huku nilikua naishi na dada.wakamwambia mwanao yupo hsp ya rufaa...
Mama akampigia dada..dada kupanda gari..akajua niliumia kidogo..akawa anaenda shule..
Haijafika mbali akakuta mama anamwambia eti mtoto Yuko rufaa[emoji16][emoji16][emoji16]
Alishuka hakumlipa konda nauli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kufika pale Niko hoi bin taaban nasubiri kwenda x Ray..wapige kichwa mkono na mguu.
Na kipindi hicho madaktar walikuwa na mgomo,shemeji alikua anafahamiana na mtu wa x-ray..hatukupata shida...
sikulazwa nilirudi home..
Kule wazaz wakafunga safari kuja.
Jamani kuugua vidonda usiombe[emoji23][emoji23][emoji23]
Baada ya siku 2 walikuja wale walionigonga..walienda kuuliza shule wakaelekezwa.
Walikuwa bega kwa bega na wazaz Hadi nilipo pona
Ila namba niliisoma vema.
Mwezi mzima sili,sitembei,sioni,siongei.
Kiuno kiliteguka,mguu haufunction,usoni ndio usiseme... nilikua km yule mama kwenye Avatar ya
Zero IQ
12.02.2012 hii siku siisahau