Acha mama aitwe mama. Nikiwa mdogo nina kama miaka 5 miaka ya 1988 hivi. Tunatoka kuteka maji kisimani na na watoto wa jirani. Kumbe houseboy kawaponda na jiwe nyuki wamesambaa mji mzima. Tulikuwa na mizinga mingi ya nyuki home, sasa wameuma kuku wote wamekufa wameuma mbuzi zizini wamekufa ng,ombe tu walifanikiwa kuvunja zizi na kutoroka.
Sina hili wala lile nastukia nimevamiwa na jeshi la nyuki, ukilia wanaingia mdomoni, ukifumbua macho wanakudunga machoni nlitupa ndum lita5 na kukimbia sikwenda hata mita 50 nikazidiwa nikadondoka. Basi kumbe mama aliyekuwa amejifungia alisikia nalia
Mama alitoka ndani bila kujali hao nyuki na kuja kuniokota nlipokuwa na kunipeleka kwa jirani. Kichwani nlikuwa mweupe maana wadudu wale wamedunga sindano zao na kuziacha hapo. Nyuki kumbe wanashambulia kichwani tu. Nikanyweshwa maziwa na maji ya moto nikatapika sumu ya nyuki balaaa. Nikapewa huduma pale baada ya siku 3 nikaanza angalau kuona kidogo. Ila nlikuwa nife aiseee