Nakumbuka baada ya kumaliza chuo kikuu Dom,
Niliamua kuanza Maisha dodoma Mjini.
Nilijiingiza katika biashara ya mitumba.Nimetembeza Sana mitumba, baada ya miezi kama sita, nilichoka nikapata kakijiwe Maeneo ya Mashujaa.
Mchana haturuhusiwi,Jioni ikifika ndo tulikuwa tunajiachia kumwaga pembeni mwa barabara ya Mashujaa kama unaelekea jamatini kutoka stendi ya Mabasi Makubwa.
Sasa nilikuwa nakopeshwa mzigo,ili kufidia mzigo uuzwe haraka nilikuwa nawahi sana saa 5 asubuhi mm nimemwaga,nilikuwa namwaga mzigo chini ya miti iliyo pembezoni mwa barabara.
Ikifika jioni nasogea barabarani.
Siku yangu ilifika,nimetandika turubahi vizuri,nikatandaza mzigo wangu,pembeni ya mti Mmoja.
wakapita wateja kama sita hivi wamama wakajaa mbele Mimi nimewageukia nawahudumia.Nimetizama barabara wao wameipa mgongo barabara.
Ghafla tulishtuka kuona kusikia kishindo kikubwa Sana kikiambatana na vumbi kali sana ambalo lilitufanya wote tuonekane kama tumetoka mavumbini ndani ya sekunde tano tu.
Kugeuka nyuma yangu nakuta saloon toyota hiace zile private rangi ya kahawia ikiwa imepigiza kwenye ule mti wangu,huku inaendelea kuunguluma.
Nikashangaa kundi kubwa la watu wamefika pale wameshika vichwa.
Walijua asilimia mia nimeshaaumia maana ni eneo langu.
Nashkuru Mungu skupata hata mchubuko zaidi ya kuoga vumbi,kuibiwa mzigo katika ile taharuki,na Mzigo kuchafuka sana na vumbi.
Kilichoifanya ile gari igote pale kwenye mti. nadhani ni Mungu tu,laiti ingepitiliza saizi nisingekuwa hapa kusimulia,
Ilikuja kubainika kuwa ile gari ilitoka Car wash iliyopo maeneo ya jirani pale maeneo ya garden ya mashujaa,na aliyekuwa anaendesha hakuwa anajua anachofanya ni basi tu utundu wa vijana waosha Magari wakiachiwa Magari.