Unajua kuna wakati unakua mtundu hadi wazazi ndugu wanakususa hawataki hata kusikia jina lako maana wamechoka habari zako.
Hiyo hali ilinikuta mimi maana nilikua troublemaker tabia zote mbaya zangu sio wizi,mademu,bangi,nk yani zoteee kilichonisaidia ni wazazi wangu hawakufikia roho mbaya ya kunipeleka gerezani japo mjomba angu alikua akiwasisitiza kila siku huyu tukamfunge akae magereza hata mwaka tu ila wazazi wangu hawakumsikiliza.
Kwa ukorofi wangu nilipiga demu mmoja alikua mpenzi wangu,nilimfumania red handed geto kwa msela...Nilianza kupiga Jamaa plus dem maana nilikua na Panga,nilipiga wale watu ndani,bahati mbaya yule jamaa akanishnda nguvu akachoropoka Ndukiiii,Nikabaki na dem wangu asee nilipiga yule dada alipiga ukunga hadi sauti ilikata.,Baada ya kuridhika na kumchakaza nikatoka na panga langu lina damu nikasepa.
Si unajua bangi mbaya bwana,,,bangi ilipokata akili ikanirudia nikagundua kua nilimpiga sana yule mdada kiasi kwamba hata uhai wake ulikua mashakani,nikaamua kukimbia nyumbani kabisa maana nilijua lazima kesi ifike polisi,na kweli ikawa vile.
Baada ya kukimbia hapo sina mbele wala nyuma,nikageuka mtoto wa mtaani nalala nnche nazurura yani Full kuwa mtoto wa ajabu ajabu yani,siku moja nikasema HAPANA hii imefika mwisho siwezi teseka kiasi hiki bora nife mimi,basi nikatafuta kamba nikasema ni bora nikajiua..Usiku nikazurura kwenye nyumba za watu nikakuta Kamba ya kuanikia nguo imefungwa imeanikwa nguo..Nikatoa nguo zote nikatupa chini,nikafungua Kamba nikasepa nayo.
nilipopata kamba yangu nikasema hapa ngoja nilale hlf kesho ntatafuta mti porini ulioimara nikajitundike,pakakucha kesho yake nikazama porini nikatafuta mti nikauona..nikaenda kufunga kamba huku nalia peke angu,Nikajifunga kamba nikajiachia BWANA BWANA BWANA BWANA sikuweza vumilia yani shingo ilikua inakatika,nilibembea na ile kamba nataka nijiinue juuu kamba inateleza Jamani natamani nielezeee mnielewe lakini sijui.
Nilikukuruka kamba ndio inazidi kunikaba Mungu si athumani sijui nini kilitokea nikajikuta nimedondokea mgongo kwenye jiwe,Ndio ikawa pona yangu ila koo liliniuma mwezi mzima nikawa siwezi meza hata Mate...
Sikieni tu Mtu kajinyonga...