NILIOKOLEWA NA JIRANI NA WAZUNGU
View attachment 1426951
Mimi ilikua siku nikiachwa mwenyewe nyumbn basi hio ndio siku ya kujaribu mengne yote ambayo nakatazwaga,
Siku moja hv wakubwa wote wakaenda shamba kuvuna mahindi nikaachwa mwenyewe, wakati wanaondoka Mama akaniambia "Leo usipotulia litakalo kupata utajisaidia mwenyewe maana kambini watu karbu wote leo wanaenda shamban kuvuna mahindi" (tulikua tunaish kwenye kambi za maliasili na utalii na ipo isolated na vijiji vingne) mtoto wa mamkubwa akacheka akasema "leo sijui tutakuta kituko gani?"
maana wiki iliyopita nilikutwa nimelala kwenye maua baada ya kupanda juu ya bati na kujitia fundi wa antena nikashuka nayo, nilipo angukia ndo hapo hapo nilipokutwa nimejikunyata, wapita njia walikua wananiona ila hawakujua kama nimepattwa na tatzo maana hapo hapo mbuzi wakaja kujilaza kwa kunizunguka, jiran baada ya kuona mbuzi wameondoka wamekuja kuku mimi bado nipo ndo akapigwa na machale akaja kunibeba akanipeleka dispensary,
Sasa basi, baada ya bimkubwa kunipa onyo wakasepa, nikanywa kwanza chai, wakati anaongea vile nilikua nasubr tu amalize lakn kichwan nishapanga leo lazima nijifunze baiskeri.
Nikaenda stoo nikachomoa mphoenix nikakokota mpk barabarani, mimi raha yangu nikokote mpk kwenye mteremko/kilele cha mlima halaf nipande inishushe then nikokote tena nirudie,
Nikaenda mara ya kwanza safi tu, mara ya pili niliumia kdg matakoni baada ya kujibamiza kwenye ule mtalimbo unaounganisha sterring na kiti maana nilikua sikai kwenye kiti ili nifikie sterring na pedal vizuri(tulikua tunaita kuisimamia),
Mara ya tatu ndo kimbembe sasa,
Kwa sbb nilishajihs kuweza mzee nikashuka kwa kasi huku nimekaa kwenye kiti, kitu kikaanza kuyumba, speed ikaongezeka zaid, break nikashndwa kushika maana siwez kutanua vidole nizifikie na nikilazimisha napoteza balance maana huku nyuma nako kiti nimekikalia pale kwenye ncha(pale wanaposema panawatoaga wanawake waendesha baisker bikra) huku nimeinamia sterring,
ule mlima n mrefuu mpk ufke chini, chini ikawa inapanda gari ya watalii wanaenda kule kambini kuchukua kibali ofisini ili waingie porini huku wanachukua video, wakaniona nashuka kwa kasi sanaa ikabd wao ndo wanikwepe,
Sasa pale mwisho wa mlima pana kona kali, juu kuna mto/bwawa kubwa lenye kina hasa, then karavat mbili kubwa hasa, chini maji yanakoshukia ni maporomoko kwenye maweee makubwa na pembeni chaka la miba.
Kona nilijua niwazi kbsa sitaweza kukata na nikilazimisha tuu zile moramu pale chini na mawe mali yangu,
Nikawaza kule juu kwenye bwawa nitakufa bila hata kuonekana nyama, kwenye karavati jinsi yalivyo makubwa na nikisikia yale maji yanavyofoka sikutaka hata kuwaza, kule chini yale maporomoko ndio hata hilo wazo halikunijia, option ikabakia kwenye chaka la miba(miba flan hv mifupi imejikunja halaf inawasha sana ikikuchoma),
Nikalifakamia bwanaaaaa, niliingia mpk kati kati ya lile biwi kubwa la miba, huko ndani kulikua na vicheche, bundi, kware, wanyama flani hv wananuka sana na wale wanaopenda kujisaidia sehem moja hata wakienda mbali watarud pale n.k wote walitoka nduki kila yule kwa mlio wake, nilibananishwa na miba ukijitikisa tu kdg inakuchoma,
kumbe wale wazungu walipigwa na machale, walipaki gari wakarud kuniangalia, wakanikuta nimejaa damu hata kulia siwezi maana nikitanua mdomo tuu nakutana na miba inazidi kupenya, ikawa naangusha tu machozi na migunoo,
mmoja akaenda kwenye gari kuchukua vifaa wakatumia zaid ya masaa mawili kunitoa mule ndani ya lile biwi la miba bila kuniumiza zaidi, wakanipa huduma ya kwanza(walikua na vifaatiba ving),
Wakanipeleka ofisini,
huko tukamkuta mzee na wafanyakaz wenzake, nimejaa ma bandage ofce nzima wakaanza kuitana "jaman njooni mmuone ..... Tena Huku, ya leo kalii"
Yaani baada ya kusununika watu hoi kwa vicheko maana washanizoea sasa,
hapo naonekana tu kijimdomo na macho tu, wale wazungu wakawa marafk zangu kuanzia pale mpk wanaondoka, wakaniachia bonge ya Nokia na PC, niliwashwa siku tatu, kuanzia pale ikawa kuachwa nyumbn mwenyewe n mwiko.