Tulifika Dar saa 9 usiku kutoka Zanzibar, kitu cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi

Kabisa bandari ikeshe..soko la kariakoo likeshe..etc
Bandari zinakesha, hapa inachoongelewa ni boti moja tu ya Unguja kuja Dar.

Uzembe unaofanyika safari ilipoanzia na kampuni binfasi ambayo haifati muda wa "schedule" zake. Inawawacha abiria kwenye boti ikifahamu kuwa imekiuka muda wa kuingia bandarini italambwa faini ikishusha abiria muda huo.
 
Unasema alichelewa kwa vigezo vipi vyoko au vya mleta mada? Au unakurupuka na kukariri kuwahi ni asubuhi tu?
Wewe unaongea nini?
Kasema mwenyewe alichelewa akalazwa majini kwamba wateremke muda custom wako hai.
Kawaida tu hiyo.
Si tulikaa Russia masaa manne ndio kutoka na hatukufika mbali tukaanza kughasiwa.
Tukarudi ndani kutulia.
Kulikua na kila kitu mle so
watoto hawakuboreka
chochote.
Nimekujibu kistaarabu kwasababu hujaongea matusi.
Kaa kwa Amani
 
Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar, baada ya shughuli zangu nilikwenda bandari lakini nikawa nimechelewa boat. Nikalazimika kupanda ile ya saa 3 usiku. Tulifika Dar saa 9 usiku ila cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi. Hii iliniacha na maswali sana kama kuna kusafiri usiku kwa nini tusishuke maana kwa Dar saa 9 usiku ni kama kumekucha tu. Kama issue ni bandari basi uwekwe utaratibu ila kwa sasa ni kusumbuana aisee. Yaani haya mambo ni viashiria vya umasikini wa nchi.
Huenda mlimsindikiza mtu ambaye hamkujua mnaye kwenye chombo
 
Kuna boat ya kutoka Zanzibar saa tatu usiku inatembea mwendo mdogo sana inaingia Dar saa tisa usiku. Abiria hamruhusiwi kuteremka Hadi ifikapo saa kumi na mbili asubuhi.

Ni boat nzuri na ya kisasa, sema Kuna mende wengi kwenye ile boat sijapata kuona... Sijui wahusika hawajaliona hilo
..boat za kisasa zimeboreshwa na ni high speed hiyo inatembea ka konokono unasema ya kisasa? hiyo ni kwa ajili ya wachelewaji ndo maana mnaondoka usiku
 
Tatizo ni nini mpaka kuwasubirisha watu masaa matatu? Giza au kukosa wafanyakazi, unaonekana akili zako ndio za hao hao anaowaongelea.
Nani anafanya kazi sa 12 asubuhi hapo bongo?
Mtu atoke mbezi kimara afike kazini foleni ni saa 2 saa 3.
Ndio mana hao jamaa wanapark mlale humo mpk wafungue.
Ni kawaida tu,wakikiuka watapigwa ban,leseni italambwa na kila kitu kinaishia hapo..
So follow the rules,
Umechelewa mwenyewe unakuja kuita watu Maskini.
Upumbavu gani huu
 
Kuna siku ilinipata hiyo kadhia nikitoka Dar kwenda Zanzibar, tulipanda zile Azam Sea Link ( sio speed boat) ni ya mizigo, magari na abiria wengi zaidi ila Mara nyingi inasafiri usiku.

Tulifika Unguja saa tisa usiku na tuliruhusiwa kushuka Kwa vile kulikua na magari ya BoT ya kusafirishia pesa kwenye hiyo meli.

Turudi kwenye hoja ya mleta Uzi.

Zile meli Mara nyingi zinapakia abiria na kushusha eneo la bandarini, sio huku kwenye speed boat. Hapo inabidi wahusike maofisa wa usalama, TRA, Bandari na wenye chombo wenyewe, ina maana ikiwa mojawapo ya maofisa kati ya hao hapo juu hawatakuwepo, ni nadra sana mizigo na abiria kuruhusiwa kushuka usiku.

Flying Horse siku hizi safari zake ni Unguja - Pemba.

Hitimisho, kama una haraka na hauwezi kuchukua mwewe, Bora usubirie boat ya saa moja inayofika saa tatu kasorobo. Vinginevyo ukubali kubaki kwenye chombo hadi papambazuke.
Meli za mizigo zinaruhusiwa kubeba abiria au wanakula vichwa kinyamela?
 
Ni mambo ya kiusalama na utendaji zaidi. Wewe umefikiria upande wako wa abiria lakini hujafikiria upande wa wafanyakazi wakaokuja kukuhudumia. Wengine hiyo saa 9 usiku ndiyo wanatoka makwao ili waje kukuhudumia wewe saa 12 asubuhi.

Kifupi ni mipangilio ya kikazi tu.

Tatizo letu kubwa Tanzania ni ujinga tu, kwanini meli iondoke huko ilitoka saa ambazo wanafahamu itafika Dar saa 9 usiku na abiria watakalishwa ndani ya boti mpaka ifike 12 asubuhi?

Ni ujinga tu wa safari ilipoanzia siyo ilipoishia.
Usitetee vitu vya ajabua ajabu,
Kwa nini bandarani hawafanyi kazi masaa 24?
DP World hawajaanza kufanya kazi??
 
Wanaweza kukuambia hatuna wafanyakazi wa kufanya check in/out mpaka saa 12 asubuhi, ni dalili ya umaskini wa akili hakuna zaidi, kwa wenzetu mfano Bank za kimarekani ukiwa ndani ya Bank unasubiri huduma na imetokea muda wa kufunga umefika, security watafunga milango yote ya kuingilia ndani wataacha wa kutoka tuu, mtahudumiwa mliokuwa ndani mpaka wamemaliza wote au wakiona foleni zinakuwa kubwa ujue mpaka meneja atatoka ofisini kuja kuhudumia wateja, ikishindikana kabisa wako wakulipe au wakupe huduma bure kesho yake, niliwahi kulipwa dollar 800 kwa sababu ndege ilikuwa imejaa wakauliza yeyote ambaye yuko tayari kuachia sit mpaka next flight tunakupa 300$ hawakupata mtu mpaka walipopandisha 800$ mchizi nikanyoosha mkono:D
Hiyo ya benk za marekani hata huku ndio utaratibu
 
Bandari zinakesha, hapa inachoongelewa ni boti moja tu ya Unguja kuja Dar.

Uzembe unaofanyika safari ilipoanzia na kampuni binfasi ambayo haifati muda wa "schedule" zake. Inawawacha abiria kwenye boti ikifahamu kuwa imekiuka muda wa kuingia bandarini italambwa faini ikishusha abiria muda huo.
Hapo bandarini hakuna wahudumu na maafisa usalama muda wote ambao wangeona kuna boti imefika ila haishushi abiria wakaulize shida ni nini?! Huu ni ufanyaji kazi wa wapi??

Wewe utakuwa na wajomba zako wanaofanya kazi bandarini unawatetea.
 
Back
Top Bottom