Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi?

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by Mbunge, Sep 24, 2008.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Sep 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUMEPOKEA kwa masikitiko makubwa amri ya serikali kusimamisha utoaji hati za ardhi kwa wote wenye nyumba na viwanja huko Kigamboni. Kwa kifupi kulingana na sheria mpya ya ardhi inayotka kumpa uwezo mwananchi kuitumia ardhi kama njia ya kujikwamua na umasikini huu ni uonevu na mauaji ya kiuchumi.

  Ni haki kwa kila mtu hata kama ananunua ardhi leo huko Kigamboni kupewa hati ya ardhi ili hao wenye matrilioni ya halali na ufisadi wanapotaka kuja kujenga wanunue ardhi hiyo toka kwa wananchi na sio kwa wajanja wachache serikalini.

  Inavyoonekana ni kwamba Wizara ya Ardhi inataka wao na wanasiasa waliowaweka hapo wafaidike pale ardhi hiyo itakapopaa bei na wananchi wa kawaida Kigamboni waendelee kula kisamvu, dagaa na ugali wa bada. Hilo hatulikubali.

  Tunaomba serikali itengue uamuzi huo na kama wizara hiyo haina fedha ya kutengeneza hati za umiliki viwanja na ardhi basi wapewe wakala watu au makampuni yenye uwezo kufanya kazi hiyo. Inatuuma sana maana wizara hii ndiyo inachoyachangia kwa kiasi kikubwa umasikini wetu na matatizo yanayotukabili sisi wananchi wa kawaida hapa Tanzania.
   
 2. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Walianza na bagamoyo, sasa kigamboni....................... tutajuta mwaka huu!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wana JF mbona humu hamchangii UA HAIWAHUSU.
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kwa namna hoja ilivyowasilishwa, tumekosa ufahamu mzuri wa kinachoendelea.

  Mpaka niliposikia kwenye habari ndipo nilipotambua kwamba kuna hoja ya msingi kwenye mada aliyoleta mbunge.

  Kuna gazeti moja la Mengi (Kulikoni nadhani), litaripoti hii issue.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mbunge,

  Tatizo la Tanzania ni UFISADI na stunts zinazochezwa na viongozi lakini kama kweli Tanzania ingekuwa na malengo na mwelekeo mzuri kuhusiana na eneo la Kigamboni ningekubaliana sana na tamko la serikali..

  Siku zote miji yote mbali na kupimwa ardhi viwanja hujengwa ktk meza kwa kuweka na kutenganisha sehemu za makazi, sehemu za biashara, sehemu za parks, shule Hospital na kadhalika. Kigamboni viwanja vimetolewa kiholela kiasi kwamba hakuna anayefahamu kutajengwa kitu gani sehemu gani na ramani ya mji inaonyesha kitu gani.

  kabla ya kutolewa viwanja hivyo ilisemekana kuwa Kigamboni itakuwa sehemu ya Mahotel ya Kitalii hasa ktk sehemu za pwani zenye nafasi a mchanga mzuri, na mapendekezo ya daraja yalifuatia kutokana na kuitazama Kigamboni kama mji mpya, lakini kwa maajabu ya Mussa sehemu hizo tayari zimekwisha pewa watu ambao hawana mpango wa kujenga mahotel isipokuwa wanavitumia viwanja hivyo hivyo kuviuza kwa wageni hasa wazungu...

  Kwa hiyo kama kweli serikali imesitisha utoaji hati kwa madhumuni ya kuthibitisha kile kinachokusudiwa kujengwa kulingana na plan ya mji ama sehemu hiyo nadhani hili ni wazo zuri sana isipokuwa tu nachelea kusema kwamba hakuna kizuri kilichokusudiwa na viongozi wetu isipokuwa kuna baadhi yao wametupia jicho mtaji wa viwanja hivyo!.. Wanavitaka wao.

  Pili kuna uwezekano mlipigwa stunt mkauziwa viwanja ambavyo serikalii likuwa bado haijafikia kuvitoa kwa wananchi..kumbuka wacheza sinema wengi bongo wala sintashangaa kabisa kuwa viwanja hivyo vilitolewa kwa njia haramu na vibali mlivyobeba vimegushiwa..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkandara

  Nakubaliana na mtazamo wako kuhusu hili tamko la serikali (sijui limetolewa lini).

  Kinachonishangaza kidogo ni kuwa Kigamboni ilishagawiwa tangu Makamba alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dsm. Ninachojuwa ni kuwa hakuna kiwanja "kinacholipa" kigamboni ambacho hakimilikiwi na Kigogo. Pia, Hati za Kumiliki Viwanja za Muda mrefu (miaka 66) zimeshatolewa chini ya mradi ule wa Makamba.

  Sasa sina uhakika Mbunge anaposema Serikali imesitisha kutoa hati za arthi kigamboni anamaanisha viwanja ambavyo "havijapimwa" au vile vya mradi lakini yeye/wao bado hawajachukua hati zao?

  Mbunge, tafadhali fafanua kidogo au tunaomba link ya hilo tamko ili tujisomee wenyewe kabla hatujaanza kupaniki..!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tatizo hii nchi yetu imejaa mafisadi kila kona, hadi kwenye ardhi.......

  Wameona Kigamboni imekuwa na Panton jipya karibia linaanza kazi, na NSSF wamejitolea kujenga daraja basi ndio wamekumbuka kwamba kuna sehemu inaitwa kigamboni na kuja kuzuia watu wasipime viwanja vyao....

  wameshachungulia deal na wamegundua muda si mrefu kigamboni viwanja vitakuwa deal na wao wanataka kujiwekea sehemu ili baadae waje kuuza kwa bei kubwa.

  Siku zote Kigamboni ilikuwepo, umeme hakuna usafiri shida maji shida, mbona hawakuvitaka hivyo viwanja...............iweje sasa ndio waone kigamboni deal.

  Mimi nasema kiwanja changu hawachukui ng'o walete WAWEKEZAJI WAO Lakini mimi eneo langu sihami hata wakileta FFU...... labda wanipe kiwanja masaki, sinza au mikocheni ndio nitakubali kuhama.

  Wamezidi kutuonea WATANZANIA KWA SABABU SISI NI WAPOLE SANA.
   
 8. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kuna jamaa mmoja hapa katania nilipomwuliza kuhusu hili, anasema ati ni kwasababu huko kigamboni mmejaa wapemba na wazanzibari mnaotaka kujitenga..hahahaha. nimecheka kweli.
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna wasukuma wengi tu Kigamboni, wanalima viazi kwa ustadi kweli.
   
 10. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hayo maoneo uliyoyataja ni majina tu lakini hayana beach yenye mchanga laini na usiokuwa na mawe kama Kigamboni. Nakushauri utulie hapo hapo kama umekaa kwenye kiti cha kinyozi.
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Msaada kwenye tuta: kwani huko Kigamboni kiwanja cha kienyeji cha wastani wa kujenga nyumba na sehemu ya bustani ikabaki kwa wastani ni kiasi gani kwa sasa? any idea pls
   
 12. C

  CHAUMBEYA Member

  #12
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 15, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndugu mbunge,
  nafikiri utagundua kuwa watu hawachangii kwa sababu hujatueleza kwa undani hilo tangazo la serikali limetolewa lini na wapi.

  mara nyingi uamuzi kama huo huwa unatangazwa katika gazeti la serikali. ila sina uhakika kama hilo ni sahihi kwa kuwa ninafahamu kuwa vibali vya kibada vinaendelea kutolewa na huko ni kigamboni.

  ila kwa kukufahamisha tu ni kuwa kuna mpango wa kuibadlisha kigamboni kuwa ndiyo city center (kama ilivyo kisiwa cha manhatan new york). hiyo ni vision aliyokuwa nayo kikwete na ndiyo pia ni dira ya serikali. hii ndio maana serikali inatumia jitihada kubwa kuhakikisha kunakuwa na daraja la kwenda kigamboni. Daraja hili linajengwa na NSSF na watu, magari, mtu na treni (nayo itapita hapo juu) watalazimika kulipia. sioni katika mtazamo wangu watu masikini wa kigamboni kama wako katika mpango wa serikali.

  definetely hata nyumba zote za kiswahili zinatakiwa kuondoka ili yaweko maghorofa. (mpango ni kuweka maghorofa ambayo minimum height yake ni floor 30 kwenda juu).

  Sidhani kama mpango huu bado upo maana siku hizi siko serikalini na nimejaribu kumuuliza mtu wa usalama wa taifa ameniahidi kunipatia jibu baada ya kutafuta.

  naomba wengine wenye ufahamu wa siku za karibumi watupe habari.
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwa ufahamu wangu ndugu masatu mimi nilinunua huko kama miaka mnne ilikua 1.5 mil,ila kwa sasa nikama 7 million ukimlalia mtu na ina tegemea na umabli kutoka kwenye ferry.
   
 14. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  CHAUMBEYA

  Na haya sasa mapya.

  Embu hiyo source yako iiulize vizuri je mambo hayo yatafanywa kuanzia wapi maana kigamboni ni mkubwa.kuna sehemu ya mladi ule waselikari ambao uliishia kibada mpaka sehemu furani za Mji Mwema sasa je sisi tulio anzia Kibugumo A na B na kuendelea mpaka Geza ulole tutaathirika?

  nNa je mimi mfano nishaweka jengo langu kwa thamani na la kisasa ingawa si nghorfa je pia nitaathirika?

  Muulize vizuri huyo bwana ili tuanze kujiaanda.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ili tangazo la lini maana kuna hati za viwanja vilivyopimwa zinaendelea kutolewa hata hivi tunavyoongea maana nilikuwa ardhi tarehe 19/09/2008 na hati yangu hipo kwenye process nzuri.

  Labda ukitoa clarification zaidi itakuwa vizuri zaidi ili tuweze kuchangia kitu tunachokijua.
   
 16. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  soma PM yako.
   
 17. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna tamko limetoka kwenye magazeti ya leo kwamba Serikali ina mpango wa kuchukua eneo karibia lote la Kigamboni ili kutengeneza mji wa kisasa.

  Kuan tetesi kuwa eneo hilo litapewa kwa mwekezaji wa nje. Kibaya ni kuwa wananchi wa maeneo hayo hawajaambiwa chochote na kuna hatari wakazulumiwa maeneo yao.

  Wana JF, kuna mtu mwenye taarifa ya kina kuhusu mpango huu? Ni nini kinaendelea? Unahusu nini? Ni wa nani? Kwanini mambo yanapelekwa kwa chini chini sana bila ya kuwashirikisha wananchi? Kama wananchi wanataka kudai haki watapotimuliwa kinguvu ni nini wafanye?

  Naomba kutoa hoja.
   
 18. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hayo ndiyo mauzo kamili ya nchi, hilo linaitwa Azimio la Kigamboni
   
 19. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mwendo huu ni hatari kweli kweli. Watu tutaanza kuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu wenyewe.
   
 20. w

  wajinga Senior Member

  #20
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio kama tutanza tumeshakuwa wakimbizi. Huoni tuko hali tweende sausi tukapigwe risasi kuliko kufa na njaa hapa.
   
Loading...