Usifanyie lamination hati yako ya umiliki wa ardhi. Tuhifadhi vipi hati zetu za umiliki wa ardhi zisichakae?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Wizara ya Ardhi inakushauri usijaribu kufanyia lamination hati yako ya umiliki wa ardhi kwa sababu inaweza kukwamisha wakati wakuuza ardhi husika, kukopa au kufanya transfer yoyote.

Ndugu wananchi tunaomiliki ardhi tuchukue ushauri huu na kuufanyia kazi una manufaa makubwa kwetu wamiliki na vizazi vyetu.

Swali, tutahifadhi vipi zisichakae?

=====


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga, amesema Hati miliki za Ardhi zinazotolewa kwa wamiliki wa ardhi nchini hazitakiwi kuwekewa 'Lamination'.

Mhandisi Sanga ametoa kauli hiyo wilayani Chalinze mkoa wa Pwani, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii kukagua utekelezaji Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) katika eneo la Msolwa .

Amebainisha kuwa, wizara yake ya ardhi itaendelea kutoa elimu juu ya suala hilo sambamba na kutoa maagizo kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi kuweka matangazo kwenye ofisi zao kuhakikisha wananchi wanapata elimu kwamba hati milki ya ardhi haitakiwi kufanyiwa Lamination' iwe mpya au ya zamani.
 
Swali kwanini wasibadili mifumo yao ili kuendana na kasi ya wanaotaka kutunza nyaraka hizo kwa ku laminate?
 
Back
Top Bottom