Waliochukuliwa maeneo kulipwa Tsh. Bilioni 4.5 Dodoma

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuanzia wiki ijayo Halmashauri ya Jiji la Dodoma itaanza kulipa fidia wananchi ambao maeneo yao yalitwaliwa na tayari Sh bilioni 4.5 zimetolewa na serikali kwa ajili hiyo.

Akizungumza kuhusu kliniki ya ardhi iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Jiji, Silaa alisema wananchi wanaodai fidia ya viwanja, jji limeanza kupima ili walipwe.

"Mkurugenzi wa Jiji ameshapata fedha za fidia Sh bilioni 4.5 kulipa wananchi fidia ambao maeneo yao yametwaliwa ili upimaji wa ardhi uanze na wataanza kulipwa kuanzia wiki ijayo. Tukiri kupokea maele kezo ya chama na tumeanza kuyatekeleza, pamoja na jitihada ambazo zinafanywa na wizara lakini tuongeze kasi, leo tunazindua kliniki nyingine tena Jiji la Dodoma," alisema.

Alisema kwa maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kupitia kamati iliyokuwa imeundwa tayari wizara imeanza utekelezaji na sasa Jiji la Dodoma ni Mkoa maalumu wa Ardhi na utakuwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi.

Alisema wamejipanga kuhakikisha matatizo ya ardhi Dodoma yanakwi-sha na yaliyopo nchini na kunafanyika mabadiliko ili Watanzania wasiwe na kero na sekta ya ardhi kulingana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Silaa alisema kliniki hiyo ya ardhi haitakuwa na mwisho hadi matatizo ya ardhi Jiji la Dodoma yaishe na baada ya kazi hiyo kutakuwa na ofisi za kisasa zenye kamera.

Alitumia fursa hiyo kumuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuhakikisha wataalamu wa maeneo yote nchini wanatoka maofisini kwenda kuhudumia watu kwa uwazi.

"Mimi kuanzia Jumatatu nikitoka bungeni saa nane mchana nakuwa hapa kusikiliza kero za wananchi ambazo zinahitaji zisikilizwe na Waziri tụ na nimeelekeza ofisi zote za ardhi wataalamu watoke na kliniki kama hii ziwe kote nchini," alisema.
 
Back
Top Bottom