Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 6.



Haukupita muda ba'mdogo akawa amerudi ndani na kusema amejaribu kutazama kila pembe ya lile jiko hakuona mbuzi.Sasa tukawa tunajiuliza yule mbuzi alikuwa akilia mle ndani ya jiko au alikuwa akililia nje?,mashaka na hofu viliendelea kutawala sana.

"Naona hawa wajinga wanataka tena kurudia mambo yao" Alisema ba'mdogo.

"Hizi dalili siyo nzuri kabisa za kuendelea kuishi hapa,haya mambo yalinitesa sana kipindi fulani ila yalikoma,naona sasa yanaanza kurudi" Aliendelea kusema.


Tulikaa macho kiasi kwamba mpaka kukapambazuka mida ya saa 11 alfajiri.Sasa Ema nae akawa anajigeuza geuza akiugulia maumivu ya kipigo alichokuwa amepokea usiku.Ilipofika mida ya saa 1 asubuhi headmaster alielekea shuleni akisema angewahi kuja ili aelekee kwa mwenyekiti wa kijiji kutoa taarifa uenda ingesaidia kama mwanzo.
Mimi niliendelea na shughuli zangu za kawaida hapo nyumbani,sasa wakati nikiwa nje jamaa akawa ametoka anachechemea akaenda kukaa kwenye jiwe akawa anaota jua!.
Nilimsalimia lakini aliitikia kama vile hataki,sasa nikawa namdodosa ajaribu kunieleza usiku ilikuwaje mpaka kufikia kuning'inizwa kwenye makenji ya darasa,Jamaa alikuwa anasonya tu!,niliendelea kumsihi ajaribu kunieleza lakini akaendelea kukaa kimya!.

Baada ya kuona ana kiburi nilimuacha nikaendelea na mambo yangu.Ilipofika mida ya saa 5 headmaster alirudi pale nyumbani akiwa na wazee wawili ambao sikuwafahamu.
Sasa akaniita akaniambia "Hebu mwambia huyo aje hapa"

Nikatoka nje nikaenda kumuita jamaa aliyekuwa amejianika juani kama kibambala.Baada ya jamaa kuingia ndani ikabidi na mimi sasa nisogee karibu ili nisikie umbeya maana nilivyojaribu kumwambia aligoma kuniambia.

"Dogo mwenye ndo huyu hapa mwenyekiti" alisema ba'mdogo.

Aliendelea "yaani jana hatujalala kabisa"

Mwenyekiti "Eti wewe!,hebu tuambie ni nini kilikupata"

Ema "Mi sijui chochote,nilishituka nikaona nimefungwa juu ya mbao huku nikipigwa"

Mwenyekiti "Waliokuwa wanakupiga uliwaona?"

Ema "Hapana"

Ba'mdogo "Yaani ni hatari mwenyekiti,nadhani nilikueleza haya mambo ya kiendelea mi nitaondoka"

Mwenyekiti "Sasa mwalimu Wambura utaondoka halafu watoto wetu nani atawafundisha!?"

Ba'mdogo "Siwezi kuendelea kukaa hapa wakati unaona kabisa huu ni ushirikina"

Mwenyekiti "Sasa rafiki wakati wanakupiga hawakusema chochote?"

Ema "Mi wakati wananichapa nilikuwa nasikia wanacheka na nilikuwa napigwa na watu wawili,maana alipokuwa ananipiga huyu na mwingine pia ananipiga"

Mwenyekiti "Hebu toa shati nione"

Ema alivua shati alilokuwa amevaa akamgeuzia mgongo yule mwenyekiti.Ema hakuwa na majeraha lakini mgongo ulikuwa umeumuka kama andazi.

Mwenyekiti "Mwalimu hebu tuteremke na huyu kijana senta akapate dawa pale kwa Malimi"

Basi baada ya maongezi yalichokuwa takribani nusu saa waliondoka wote kuelekea huko Senta.Siku hiyo ilikuwa ngumu sana na sikutaka kabisa kuzurura hovyo,ilipofika mida ya saa 10 alasiri nilichukua zangu dumu nikaelekea lamboni kuchota maji ya kuoga.Usiku wa siku hiyo jamaa hakulala kabisa,japo alikuwa akijifanya mbishi lakini ilibidi arudi kitandani kulala maana aliona angeendelea kulala chini yangemkuta kama ya usiku ulokuwa umepita.

Sasa hali ya mambo ikawa shwari kwa siku kadhaa na yale mauzauza hatukuyaona.

Nakumbuka siku moja mida ya saa 11 jioni headmaster akiwa amerudi nyumbani,alinituma niende Senta nikanunue betri za redio,sasa wakati naondoka sikutaka kabisa kupita njia ya ile miembe kwasababu nilianza kuingiwa na hofu,ilinibidi nizungukie njia ya kwenye lambo japo ilikuwa ya mzunguko lakini ilikuwa salama kabisa.Sasa wakati nikiwa napita kando kando mwa lambo nikama nilimuona yule binti aliyekuwa na Ema pale kwa rafiki yake Jackson ule usiku wa varangati la yeye na Deborah.
Wakati namtazama alikuwa anachuma yale majani marefu huwa yanaota kando kando mwa maji yanayotumikaga kutengenezea majanvi.
Sasa wakati navuta taswira huku nikigeuka nyuma kumtazama ili nimpe hai!,ghafla sikumuona,nikashituka ikabidi nisimame nitazame vizuri,kweli hakuwepo.Sasa ile nageuka zangu mbele niendelee na safari ya kuelekea senta nikakutana naye uso kwa uso akiwa amejitwisha yale majani kichwani!,kiukweli niliogopa sana na nikajikuta nimepiga kelele "Mamaaaaaaa".

Ili kuondoa aibu ya kiume,nikajifanya "Umenishitua".

Yule binti akaanza kucheka huku akiniambia "kumbe na wewe shemeji yangu ni muoga hivo eeenh".

Mimi "vipi lakini"

Yeye "freshi"

Mimi "Huonekani"

Yeye "Mi nipo,ndugu yako hajambo?"

Mimi "Yeye mzima"

Yeye "Wapi mbona upo spidi?"

Mimi "Naelekea senta mara moja"

Yeye " sawa shemeji tutaonana,ngoja niwahi nyumbani kupika"

Niliondoka nikiwa namtazama yule binti lakini sikummaliza hata kidogo,nilijiuliza maswali mengi sana ambayo kiukweli sikupata majibu.
Basi nilifika Senta nikachukua nilichokuwa nimekifuata na kurudi zangu nyumbani.

Nilipofika nyumbani baada ya kukabidhi zile betri kwa Headmaster nilirudi kule kwenye chumba chetu,sasa safari hii jamaa akaanza kuongea na mimi kwa furaha sana,sikujua ile furaha alikuwa ameitoa wapi maana kwa siku kadhaa alikuwa ameninunia kama mwanamke.

Ema "Baadae nataka unisindikize kwa debo kaka"

Mimi "Kuna nini?"

Ema "Tulipo onana shule aliniambia niende kwao baadae"

Mimi "Mlishayamaliza?"

Ema "Tuliyaongea yakaisha kaka"

Mimi "Sasa baadae ya saa ngapi?"

Ema "Tusubiri kwanza headmaster akilala tuondoke"

Mimi "Haitakuwa noma?"

Ema "Hapana,huwa akiingia kulala ni mpaka asubuhi"

Mimi "Sawa nitakusindikiza".

Kweli,baada ya kupata msosi wa usiku,tuliingia ndani kwenye chumba chetu na headmaster alifunga mlango wa sebuleni akaingia chumbani kwake.

Sasa ilipofika mida ya saa 3 ikabidi jamaa anaimbie tusepe.Kule kijijini kutembea usiku ilikuwa ni kitu cha kawaida sana,kulikuwa hakuna majambazi wala vibaka,changamoto ya kule ilikuwa hayo mambo ya kishirikina.
Tukiwa njiani tuelekea kwao debo,nikamwambia jamaa nilikutana na demu wake alikuwa anamsalimia.

Mimi "Hivi huwa mnasoma nae?"

Ema "Kale kademu nilionana nako pale mashineni siku moja nikienda kusaga"

Mimi "Ooh sawa,nikajua labda ni kanafunzi"

Ema "Halafu siku ile nilikaambia kaondoke kakawa kanang'ang'ania kulala kaka"

Mimi "Kwahiyo baada sisi kuondoka ulilala nako mpaka asubuhi?"

Ema " Niliamua kulala nako kaka,yaani huwezi amini siku ile Deborah nilikuwa namuona kama mavi pamoja na uzuri wake wote"

Mimi "Inaonekana kalikupa vitu ambavyo debo hajawahi kukupa"

Baada ya kumwambia hivyo jamaa akaanza kucheka sana huku akiniambia "Hamna kaka ni kawaida tu"

Mimi " Huwa anakaa wapi?"

Ema "Anakaa kule Masairo"

Sasa baada ya jamaa kuniambia hiyo sehemu inayoitwa masairo na nikipiga umbali niliomkuta yule binti pale lamboni nilibaki nimechoka,hiyo Masairo aliyoniambia jamaa kutoka tu hapo senta mpaka hapo masairo si chini ya kilometa 7,sasa vuta picha kutoka pale lamboni ambapo ilikuwa jirani na shule mpaka huko masairo,kiukweli ilikua ni mbali mno kikawaida tena kwa mtoto wa kike ndipo nikabaki najiuliza maswali yasiyokuwa na idadi.

Sikutaka kumwambia jamaa kile nilichokuwa nimekiona pale lamboni wakati ule,ilibidi nikaushe ili niendelee kujifanya bwege stori zinoge.

Sehemu ya sita Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe
Hatari sana
 
Kuna muda unawaangalia wapumbavu humu JF unashindwa kuelewa nani aliyewaroga unakosa majibu,hivi nyie mmezaliwa Tanzania hii hii au labda kuna nchi mlitoka tofauti na hii?au labda kusoma ndiko hujui?

Nilichosema hapo ni kuwa hao wanafunzi 12 ndiyo waliomaliza form 4 kwa mwaka wa kwanza toka shule hiyo ianzishwe mwaka 2003 na walifaulu wote! Kwenda shule za michepuo ya sayansi!.,Huko ni kijijini na yawezekana wanafunzi walikuwa hata 20 ila kwasababu ya mambo ya Bush wakawa wanapungua na waliofanya mtihani wakawa 12,sasa hapo wewe mwenye akili ambacho huelewi ni nini?.

Halafu wewe unataka kunilazimisha kwenye banda nililipa 500 wakati mimi ndiye niliyekuwa nalipa 100,yaani wewe kwa akili yako unaona mia ya mwaka 2004 ilikuwa ndogo,hebu tuambie wewe uko ulipokuwa mlikuwa mnalipa shi ngapi!,yaani mtu anataka akulazizimishe useme ambacho hata hukufanya ilimradi tu yeye alidhike

Hilo swali la kwanini tulilipa shilingi 100 alipaswa ajibu mtu wa banda na siyo mimi mlipaji,pengine gharama za vifurushi vya dstv vilikuwa bei chee ili kuwavuta wateja wengi, siwezi jua,sasa kama mjini tulikuwa tunalipa shilingi 200 iweje kijijini kusiko na biashara na mzunguko wa hela tulipe 200?,Unajua kama kuna maisha hukuwahi kuyaishi usiwe unakaa mbele ya wanaume unavimbisha kitambi na tumbo lako kwa ubishi!,Na ndiyo maana nikasema mwenye banda alikuwa akisubiri mpaka muda wa gemu uanze ndipo anawasha,yale mambo ya kuangalia uchambuzi yalikuwa hamna!.

Wewe nahisi kichwani hazikutoshi T14 Armata
Nipo hapa ntarudi
 
Ndugu zangu nisameheni sana leo nilikuwa kwenye matatizo ya kifamilia.

Nilienda huku bunju ambako nafanyia shughuli zangu kama kawaida,sasa nikiwa huko nikapigiwa simu na mke wa brother kwamba kuna mgogoro wa kifamilia,sasa nimefika pale nikakuta kuna kashikashi la kufa mtu lilipolekea mimi na brother kutwangana makonde hasa!.

Sasa kwa hasira nilizokuwa nazo nimejikuta hata kuendesha pikipiki kwa umakini nashindwa ikapelekea kupata ajali,ingawa sijaumia sana ila nimepata vimichubuko vya hapa na pale ila pikipiki imeumia!.

Hivyo mniwie radhi ndugu zangu leo imekuwa siku mbaya sana kwangu!.
Pole Sana kk
 
Wapo wanaosema chai japo kwangu Mimi iwe au isiwe nilipenda tangu nisome tu jina la simulizi!
Huko duniani tunakofahamiana yupo jamaa anaitwa George Iron Mosenya yule bwana kwangu mimi ndio bingwa wa simulizi kwa kizazi hiki na nikiwa naisoma hii nakumbuka simulizi yake moja inakwenda kwa jina la MAMAAKE MAMA
 
Hivi baada ya kupakana dawa mwili mzima,ulioga ndio ukaondoka? au ulioondoka na mipako yako ya dawa? au ilikuaje?...na hizo dawa zilikua km poda/vumbi au zilikua km mafuta mkadinyana huku ikitelezea ndani kilaini
Daah huko naona hata baada ya mdunyano hakuna kuoga mnabaki na mitelezo yenu🤣🤣
 
Back
Top Bottom