Tulichokunywa na kula Ikulu Chamwino

Tulichokunywa na kula Ikulu Chamwino

Kuna watu kazi yao ni kupotosha tu kama walivyokaririshwa leo wako tayari kupinga kila kitu hadi nyeupe wanataka iwe nyeusi, nani kawaambia ili muonekane ni wapinzani ni kupinga kila kitu Upinzani wenu utabaki palepale hata mkikubali penye Ukweli au kukataa tofauti na hayo tutazidi kuwadharau na kuonekana ni WAHUNI FLANI
 
Hii nchi mi nitakuja nihame tu,imejaa watu wenye akili sizizotoshea kwenye kijiko cha chai.

Marekani ikisema buy Amerikan wanaongelea, nunua vipuri vya Marekani, nunua Magari ya Marekani, nunua silaha za Marekani, nunua Treni na meli za Marekani.Vitu vikubwa ~ refer materialistic concept.Vitu vyenye mashiko, vitu vinavyoingiza fedha nyingi yenye impact kwenye uchumi.

Sasa huku Tanzania kuna mtu anaitwa Manyerere anazungumzia buy Tanzanian akimaanisha nunua sharubati, nunua juice , nunua bla bla blaaaa, ....... amesikia mtu akijamba apata matumaini ya kupata gesi.

Manyerere, You are thinking in a right direction but THINK BIG.


Mtoa uzi ameelezea yaliyokuwapo CHAMWINO, sasa mambo ya magari, nguo, treni yametokea wapi,
Mada ya mezan ni hafla iliyofanyika Chamwino, Dodoma, Tanzania.
 
Rais John Magufuli, amekuwa akisisitiza azma ya Serikali yake ya kufufua na kuanzisha viwanda vipya.

Lakini huwezi kuwa na viwanda vipya kama sisi wenyewe hatutumii bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo.

Leo nimeona jambo la faraja sana Ikulu ya Chamwino. Juisi (sharbati) zote zilikuwa ni za hapa hapa nchini, hasa kutoka Azam.

Zilikuwapo za kila aina kuanzia za machungwa, mananasi, maembe, mapela, na kadhalika. Kwa maji ya kunywa, yalikuwapo Kilimanjaro kutoka kwa Mzee Mengi.

Mvinyo haukuwapo, pengine kwa sababu muda haukuruhusu; kama ungekuwapo, basi bila shaka ungekuwa ni Dompo, Dodoma, Presidential, n.k kutoka hapa hapa Dodoma.

Kama Ikulu wameanza kuthamini bidhaa za ndani, huu ni mwanzo mzuri wa kuimarisha viwanda vyetu vya ndani.

Hakuna sababu ya kunyeshwa juisi za Afrika Kusini au Kenya, ilhali sisi wenyewe tunazo za kiwango cha juu. Huu ni mwanzo mwema.
Ni kweli, ila vijana wa ukawa wao ni kuponda kila kitu. Nawachukia sana
 
Huyu Manyerere anaelekea kuwa kubwa jinga kama lile toto wa Malecela.
Any ways link tena Makwaiya atakualika Channel 10 mkaendeleze propaganda za CCM??
 
Baada ya kulihutubia na kulizindua bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI amehudhuria hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wabunge katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma na kuagiza fedha zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla hiyo zipelekwe Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda vya wagonjwa.
Mheshimiwa Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wadau mbalimbali wamechanga kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge.
 
Khaa!! Tingatinga pia angepiga marufuku biashara ya udalali. Kuna mijitu inakula bata mjini wakati mkulima anatokwa na jasho inasubiri mazao yakomae iende ikawalalie wakulima. Hii haikubaliki. Serikali isimamie mfumo wa kumuuwezesha mkulima kupata pembejeo kwa wakati na kumsaidia kupata masoko yenye faida.
 
Manyerere Jackton


Kama hilo ni kweli lilikuwa lengo basi naweza kusema kwamba Raisi Magufuli ameanza na mguu mzuri na huko mbele mambo yatanyooka tu, kinachofwata aanze na furniture za maofisini maseremala wetu wapewe kazi, kwanza wawezeshwe kwa kuwapa utaalamu tuna veta zakutosha tu au hata magereza pia wanatengeneza furniture, hapo itakuwa ni win win situation kwani tutazalisha ajira kwa watu wetu na pia kuongeza ubora wa bidhaa zetu hali itakayopelekea kuanza kuexport nje ya nchi!

Safi sana Magufuli!
Kumbuka kuna kutunza misitu kukabili Climate change
 
Last edited by a moderator:
Hayo mambo unayoshabikia in endelevu?au Luna mkakati endelevu, vinginevyo kama waswahili husema "ukipenda chongo huita kengeza"
 
Mtoa uzi ameelezea yaliyokuwapo CHAMWINO, sasa mambo ya magari, nguo, treni yametokea wapi,
Mada ya mezan ni hafla iliyofanyika Chamwino, Dodoma, Tanzania.

Another bullshit,
Kwahiyo essence ya mada wewe umeona ni hafla?
Seriously unataka tujadili walikula takataka gani watakunya nini?
Think outside the box bwanaaa ahhh!
 
Manyerere Jackton


Kama hilo ni kweli lilikuwa lengo basi naweza kusema kwamba Raisi Magufuli ameanza na mguu mzuri na huko mbele mambo yatanyooka tu, kinachofwata aanze na furniture za maofisini maseremala wetu wapewe kazi, kwanza wawezeshwe kwa kuwapa utaalamu tuna veta zakutosha tu au hata magereza pia wanatengeneza furniture, hapo itakuwa ni win win situation kwani tutazalisha ajira kwa watu wetu na pia kuongeza ubora wa bidhaa zetu hali itakayopelekea kuanza kuexport nje ya nchi!

Safi sana Magufuli!

Hata samani kutoka nje amepiga marufuku.Zitatumika za hapa hapa nchini.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom