Tulichokunywa na kula Ikulu Chamwino

Tulichokunywa na kula Ikulu Chamwino

Mkuu, sidhani kama uzi wangu una tatizo. Nimejaribu kuonyesha namna watanzania tunavyoweza kutumia bidhaa zetu za ndani ili kuinua uchumi na ajira za watanzania. Kuna ugonjwa wa siku nyingi wa watanzania kupenda vitu vya nje. Hiyo ilikuwa hatari kubwa sana kwa uchumi wetu. Ebu jamani penye jambo jema tuunge mkono serikali. Tusibeze au kupinga kila kitu. Ni aibu ikulu kujaza sharbati na maji kutoka ughaibuni.
Manyerere Jackton,

Bado heshima yako imeshuka Mura!

Kwakua mawazo yako yameganda kwenye "ubuge" tu!

Mh. Rais alivaa vazi la Taifa? Au kitu chochote made in Tanzania?

Chukua HOJA nzito zitakazokujengea HESHIMA kwa faida ya walipa kodi walala hoi!

Vinginevyo unaonekana ni kundi lile lile la makanjanja wanaoenda Ikulu kufuata kula!
 
Last edited by a moderator:
Siwezi kuamini kwamba mtu aliyehudhuria kuapishwa Waziri Mkuu wa nchi hawezi kutamka "mapera" anatamka "mapela." Hapana Manyerere hii haikubaliki bwana, pull up your socks.
 
Ila kusema ukweli Azam aboreshe juice zake. Unamimina juice inavyotoka utafikiri nini sijui. Tunathamini vya ndani ila watengenezaji nao watuthamini kwa kutupatia vilivyo bora kama vya huko kwa wengine.

spot on juisi inatoka kama uji flan ivi duh....... angalia ceres juis inatoka vzr sana!!! nadhan iyo ni area moja ya improvement
 
Mimi nahisi Magufuli hajui anachotaka kufanya.Hii sijui ndio ilani ya CCM au ni nini?
Halafu kuna jamaa yangu anapenda kusema ufupi ni kilema, sasa naanza kumwelewa.

Haikuhusu,mfuatilie rais wako simama dede!
 
Manyerere Jackton


Kama hilo ni kweli lilikuwa lengo basi naweza kusema kwamba Raisi Magufuli ameanza na mguu mzuri na huko mbele mambo yatanyooka tu, kinachofwata aanze na furniture za maofisini maseremala wetu wapewe kazi, kwanza wawezeshwe kwa kuwapa utaalamu tuna veta zakutosha tu au hata magereza pia wanatengeneza furniture, hapo itakuwa ni win win situation kwani tutazalisha ajira kwa watu wetu na pia kuongeza ubora wa bidhaa zetu hali itakayopelekea kuanza kuexport nje ya nchi!

Safi sana Magufuli!

Mkuu kwa hili la fenicha nakuunga mkono, niliwahi kuingia Banda la JW nikakuta fenicha nzuri ajabu, wakati huo selekali inaziagiza kutoka nje hasa SA
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kula na kunywa ndio umeamua kuja kujamba humu ili kila mtu ajue ulivimbiwa Chamwino?
 
Rais John Magufuli, amekuwa akisisitiza azma ya Serikali yake ya kufufua na kuanzisha viwanda vipya.

Lakini huwezi kuwa na viwanda vipya kama sisi wenyewe hatutumii bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo.

Leo nimeona jambo la faraja sana Ikulu ya Chamwino. Juisi (sharbati) zote zilikuwa ni za hapa hapa nchini, hasa kutoka Azam.

Zilikuwapo za kila aina kuanzia za machungwa, mananasi, maembe, mapela, na kadhalika. Kwa maji ya kunywa, yalikuwapo Kilimanjaro kutoka kwa Mzee Mengi.

Mvinyo haukuwapo, pengine kwa sababu muda haukuruhusu; kama ungekuwapo, basi bila shaka ungekuwa ni Dompo, Dodoma, Presidential, n.k kutoka hapa hapa Dodoma.

Kama Ikulu wameanza kuthamini bidhaa za ndani, huu ni mwanzo mzuri wa kuimarisha viwanda vyetu vya ndani.

Hakuna sababu ya kunyeshwa juisi za Afrika Kusini au Kenya, ilhali sisi wenyewe tunazo za kiwango cha juu. Huu ni mwanzo mwema.
Wanaume kama mabinti ndio kama nyie!
 
"Huwezi kuwa na viwanda vipya (maana yake havipo) ... kama sisi wenyewe hatutumii bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo (maana yake vipo)."

Swali:

Una maana gani kuanzisha viwanda vipya ambavyo unatusihi tutumie bidhaa zinazozalishwa na hivyo hivyo viwanda vipya? Ni vipya au vipo? Kama ni vipya, hizo bidhaa zinatoka wapi? Kama vipo, huo upya wake unatoka wapi?



Unauliza swali ganu hilo?
 
Manyerere Jackton

Kikwete alipokuwa anaanza madaraka huko Arusha alikataa kunywa maji yaliyotengenezewa Kenya akaomba maji ya Kilimanjaro sasa kilichofuata malizia wewe................uliyekuwa na raisi huko Chamwino

Wakati mwingine uongo na blah blah hazisaidii chochote..

Tangia lini Arusha wakanunua maji kutoka Kenya??
 
Nadhani mabehewa hufuata kichwa binafsi yangu kwa dhati nasema nchi itasonga mbele inaweza isiwe kwa matarajio yetu lakini kwa kiasi fulani tatizo letu ni usimamizi kwani tuna utajiri mkubwa wa rasilimali.
 
mzungu ni mzungu tu.juice ya azam kwenye glass ya made in france.hapo wote mzungu angesema kila mtu abaki na nguo made in tanzania mngebaki uchi

Loh.., u made my day !!@mdukuzi!
 
Nimesikia hata pale Ikulu alipoingia siku ya kwanza kuamkia hapo akakuta chai ya asubuhi ni Buffet akauliza hii chai yote mmempikia nani kwani kunawageni?? Kuanzia siku iliyofuata akapiga marufuku!

JF..., hata kama siku ilikuwa mbaya ukiingia humu lazima utabasamu!

Tushazoea breakfast ya mihogo au viazi vitamu pengine na kiporo cha jana...!

Breakfast za hivyo labda ukienda nje ya nchi.., na hivi safari zimekuwa za hadi kibali maalum kweli namba zitasomeka vyema sana tu.., wasioweza kusoma namba ruksa kukariri!!
 
Nawasi wasi Magufuli alikuwa Muumini wa Upinzani.... maana Mambo mazuri ya Upinzani ndio yake ya kipaumbele na amefikia hadi kuzidisha maradufu ya upinzani maana hadi Upinzani umepwaya kabisa....

Alivyo mjanja yeye kawatega Wabunge kuwa hatogusa Majimbo yao kwani ni majukumu ya Wabunge wenyewe waombe pesa wajenge majimbo yao hatowagusa....ili wapendwe na wapiga kura wao ni bonge la Tego kwa Wabunge wavivu na walaji... maana wakila hawatosalia wakati wa uchaguzi watang'olewa na wananchi wao Chama hakita wabeba...

Tusubiri tuone maana Ahadi za sasa hakuna haja ya kwenda Marekani kuishi mimi nishaghaili siondoki nchini....
 
Mimi naamini magufuli atakuwa kiongozi wa msaada sana kwa watanzania mungu ampe afya njema tu tutfika pasipo shaka tuendako.
Magufuli amesema aombewe sana kwa Mungu kwa sababu ana nia ya kuwashughulikia wauza unga, wanaolipa wafanyakazi wa bwawa la Mtera kupunguza maji ya bwawa wapate tenda za kufua umeme, wanaobuni EPA, ESCROW, wakwepaji wa kulipa kodi wakubwa nk. Anajua anaingiza mkono wake kwenye shimo analoishi nyoka Cobra. Hivi ameanza kusafiri kwenda Dodoma kwa kutumia usafiri wa barabara hawatom-Sokoine kweli?
 
Back
Top Bottom