Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,463
Rais John Magufuli, amekuwa akisisitiza azma ya Serikali yake ya kufufua na kuanzisha viwanda vipya.
Lakini huwezi kuwa na viwanda vipya kama sisi wenyewe hatutumii bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo.
Leo nimeona jambo la faraja sana Ikulu ya Chamwino. Juisi (sharbati) zote zilikuwa ni za hapa hapa nchini, hasa kutoka Azam.
Zilikuwapo za kila aina kuanzia za machungwa, mananasi, maembe, mapela, na kadhalika. Kwa maji ya kunywa, yalikuwapo Kilimanjaro kutoka kwa Mzee Mengi.
Mvinyo haukuwapo, pengine kwa sababu muda haukuruhusu; kama ungekuwapo, basi bila shaka ungekuwa ni Dompo, Dodoma, Presidential, n.k kutoka hapa hapa Dodoma.
Kama Ikulu wameanza kuthamini bidhaa za ndani, huu ni mwanzo mzuri wa kuimarisha viwanda vyetu vya ndani.
Hakuna sababu ya kunyeshwa juisi za Afrika Kusini au Kenya, ilhali sisi wenyewe tunazo za kiwango cha juu. Huu ni mwanzo mwema.