Tulichokunywa na kula Ikulu Chamwino

Tulichokunywa na kula Ikulu Chamwino

Kichwa chako hakiko sawa aisee dah unatia huruma Magufuli he is not delivering to your expectations matokeo yake wapambe ili awe relevant lazima muleta mapambio ya kijinga magufuli asipokunywa juice za azam mbona zinanyweka tu na watanzania wengine Kenya Uganda Rwanda Zambia Msumbiji watu wanaozipenda wanakunywa tu acha ujinga unajikomba kupita kiasi
 
Kama yakweli haya napendekeza mheshimiwa aanze kuitwa mtoto wataifa tu,baba si tulikuwa nae.Naomba kuwasilisha.
 
Ila kusema ukweli Azam aboreshe juice zake. Unamimina juice inavyotoka utafikiri nini sijui. Tunathamini vya ndani ila watengenezaji nao watuthamini kwa kutupatia vilivyo bora kama vya huko kwa wengine.

Juice ipi ya nje lete mfano!
 
"Huwezi kuwa na viwanda vipya (maana yake havipo) ... kama sisi wenyewe hatutumii bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo (maana yake vipo)."

Swali:

Una maana gani kuanzisha viwanda vipya ambavyo unatusihi tutumie bidhaa zinazozalishwa na hivyo hivyo viwanda vipya? Ni vipya au vipo? Kama ni vipya, hizo bidhaa zinatoka wapi? Kama vipo, huo upya wake unatoka wapi?

Ha ha ha! Watu mna maswali.
 
Kuna watu wanataka walale, wakiamka Dar ipo kama London. Poleni sana...!!
 
Nitafurahi sana endapo Raisi huyu akapiga marufuku Mitumba ili vile viwanda vyote vilivyokufa vianze kufanya kazi!
Viwanda vianze kwanza kufanya kazi tuone aina gani ya nguo zinapatikana, sio wanatengeneza low quality halafu sare sare maua halafu waondoe Mitumba.
 
Kapwila Matulu

Jitahidi kuelewa viwanja vipya kwa kuwa Rais aliahidi kuweka mazingira ya viwanda vipya kujengwa hapa Tanzania (maana yake kukuza sekta ya viwanda toka idadi iliyopo sasa). Amekwisha kuambia kulikuwa na bidhaa za Azam na IPP (hapa anamaanisha kaanza kwa kusapoti vilivyopo ili kukuvutia nawe kufungua chako kwa kuwa sasa watanzania tunataka kula vyetu).
 
Last edited by a moderator:
Baadhi ya waTanzania wana tabia ya unafiki na kujipendekeza sana..
 
Kapwila Matulu"Huwezi kuwa na viwanda vipya (maana yake havipo) ... kama sisi wenyewe hatutumii bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo (maana yake vipo)."

Swali:

Una maana gani kuanzisha viwanda vipya ambavyo unatusihi tutumie bidhaa zinazozalishwa na hivyo hivyo viwanda vipya? Ni vipya au vipo? Kama ni vipya, hizo bidhaa zinatoka wapi? Kama vipo, huo upya wake unatoka wapi?


Viwanda vipo vichache hata hicho kidogo kinachozalishwa hatukitumii ipasavyo!
 
Last edited by a moderator:
Manyerere Jackton

Kikwete alipokuwa anaanza madaraka huko Arusha alikataa kunywa maji yaliyotengenezewa Kenya akaomba maji ya Kilimanjaro sasa kilichofuata malizia wewe................uliyekuwa na raisi huko Chamwino
 
Last edited by a moderator:
Kulikuwa na nyama kidogo za kuku, korosho na sambusa. Kwa hakika ile shughuli sijui hata kama imegharimu Sh milioni 3.
Manyerere Jackton,

Hivi kweli shida za Watanzania ni kusikia mlichokula na kunywa huko Chamwino?

Nilitegemea hoja nzito za kichunguzi toka kwako kama vile kwanini Mh. Rais JPM katumia "Toyota Hilux" Dar - Dodoma (kwa mujibu wa bandiko lako) wakati Gulf Stream iko Geneva?

Je, huyo alokwenda Geneva si angeweza kutumia "Business Class" kwenye Emirates kubana matumizi ili hizo pesa ziengezewe kwenye bajeti kununua MRI?! Haya ndio wewe kama Mwandishi ujikite hapo, na sio kutuletea HABARI za "ubuge" toka Chamwino!

Watanzania wanataka kujua gharama za Gulf Stream 5H - ONE Dar -Geneva - Dar ina gharimu kiasi gani pesa za walipa kodi?

Watanzania wanataka kujua Ndege ya Rais imeingia Dar leo toka Geneva, je ilikua huko na nani na kwa shughuli gani wakati Mh. Rais kapiga marufuku safari zote za nje ili kupunguza gharama kwa serikali!

Watanzania wana haki ya kupata habari kwakua kuna katazo la SAFARI za nje!

Ahsantum
 
Tayeb
Mkuu, sidhani kama uzi wangu una tatizo. Nimejaribu kuonyesha namna watanzania tunavyoweza kutumia bidhaa zetu za ndani ili kuinua uchumi na ajira za watanzania. Kuna ugonjwa wa siku nyingi wa watanzania kupenda vitu vya nje. Hiyo ilikuwa hatari kubwa sana kwa uchumi wetu. Ebu jamani penye jambo jema tuunge mkono serikali. Tusibeze au kupinga kila kitu. Ni aibu ikulu kujaza sharbati na maji kutoka ughaibuni.
 
Last edited by a moderator:
Ni la kheri na Mola amuepushe na majaribu ya kupenda vya nje ya nchi
 
picha ya namna ya kutafuna sharubati na kula mapera..?

Unataka ni cheke mpaka mbavu ziume au? Unaikumbusha za Dr.Mihogo!
Uzalendo mpaka kula Mapera siyo?
Kweli CCM mbele kwa mbele-vipi kuna kiwanda cha Juice ya Mapera?
Wewe unaonekana hukupata vizuri ujumbe wa mleta hoja-kwamba naye alikuwa karibu na akina JP na badala ya kuletewa Juice ya Supermakert ya kutoka Uswisi ililetwa ya kutoka Azam -made ina Tanzania a.k.a from Mkuranga Pwani?.
Unajua Taarifa kama hii siyo rahisi kutuingia kichwani siye wengine wa shule za Kata mpaka tuone picha/uhalisia.

Maana yako mengiya kisanii yanayotendeka kwa mkono wa Magogoni.Mfano Wanakuja Mawaziri wapya muda siyo mrefu lakini taarifa ya mwisho iliyotoka mitandaoni ni ya urudhishaji wa Magari ila Nyumba wanazoishi yaonekana bado wamo humo sasa sijui pengine nao watawakabidhi ofisi Mawaziri wapya sijui?

Wakati huo wale wapya watakaa Serena na Kempeski kwa Muda kula Bata kidogo siyo?
 
Back
Top Bottom