Hapa kuna tatizo kama lile la `Rais kasafiri na gari kwenda Dodoma``
Manyerere ameonyesha tena ushabiki na kuipa taaluma kisogo
Hoja yake, Rais ameanza kuthamini vitu kuwezesha viwanda vya ndani kufanya vizuri.
Hakuna sababu za kunywa Juisi za Afrika kusini au Kenya`
Manyerere,
kama utakumbuka kiwanda cha general tyre.
Matairiyaliuzwa kwa magendo nchi za jirani na kuua soko la matairi
Kiwanda kilikufa si kutothamini bidhaa, bali uongozi na siasa.
Pesa za mwenge na nafasi za watoto wa vigogo. Kikashindwa ushindani
Kibo match ilikufa,watu wanapenda viberiti vya Pakistan, vya kibo , viberiti vina njiti 30 zenye baruti ni 7.
Kikiingia umande kwisha
.
Wateja wakaamua kununua something worth for the moneny kutoka Pakistan
Tulikuwa na Tanbond, hatujui imeishia wapi.
Tulikuwa na Moproco wateja wanasubiri mafuta.
Tulikuwa na maturabai wateja wa EA wanasubiri hadi kesho
Mifano hii inatosha kumwambia Manyerere, juisi za South Afrika au siagi za Kenya si ufahari.
Soko huria linakwenda na ushindani. Hizo Ikulu kamazitaingia mitaani na chuya na magugu, tutanunua za Kenya
Kinachoua viwanda vya ndani si wateja. Ni kukosa ushindani katika kila Nyanja, Masoko, bei na ubora.
Watu wanataka quality products katika affordable price. Soko huria linawapa choice
Manyerere angetakiwa kwa taaluma yake aende mbali zaidi ya kusifia rangi za maembe
Magufuli alikuwawaziri awamu 2 wa serikali zilizouza viwanda na nyumba za serikali
Leo Manyerere anatumabia huyu si Magufuli wa miaka 20 ndaniya cabinet
Kwa mwendo alio nao anyerere, hakika ni tatizo katika fani.
Ni lazima ajipime kama anawakilisha fani au ni katika jitihada.
Waswalihili wanasema udongo uwahi ungali maji, na biasharaasubuhi jioni kuhesabu mali.
Pasco