Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by masharubu, Oct 26, 2010.

 1. masharubu

  masharubu Senior Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:

  1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo

  2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.

  3.magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka

  4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake

  tupeni majina zaidi
   
 2. w

  wela masonga Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  5. Academic Desert - Mwalimu wa agriculture F3 aliye kuwa na kipara

  6. Walking Encyclopedia - Mwalimu wa English F5 aliyekuwa anapenda kuongea bombastic words.
  7. Mwalimu Peasant - Mwalimu wa agriculture F 2 aliyekuwa anajihusisha na kilimo ili ku suppliment income kwa vile mshahara ulikuwa hautoshi.
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  basuba-mwalimu wa english tulimfuma kona anacheza wimbo mmoja hivi wa kikongo uliokuwa na kikorombwezo basubaaaa
   
 4. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mwalimu Domain, alikuwa anafundisha hesabu na alophamia shuleni kwetu topic aliyoanza nayo ni ya mambo ya domain na range. Kwa hiyo kila dakika utamsikia akiuliza what is the domain?
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Fuvu:
  huyu alikuwa discipline master. noma. mwembambaaaa kama snoop dogg.

  Kisu:
  Bonge la headmaster niliyewahi kumuona. Aligeuza shule iliyokuwa ya wahuni kuwa shule yenye heshima inayofaulisha kwa kiwango cha juu bila mitihani kuvuja. Huyu jina yake kamili ni Kisusange. Kuna wakati alihamaki, akauliza wanafunzi: "naskia kuna wanafunzi wananiita Kisu, hivi wewe baba yako unaweza kumuita ba?"
   
 6. Ernie

  Ernie JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  karika papaya : mwalimu wa Agric
  Kitini : Ticha wa Kiswahili
   
 7. Ernie

  Ernie JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ngwema : Head Master, alikuwa mnoko balaa
   
 8. Catagena

  Catagena Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fiudo-mwalimu anyefundisha Civics, pat ya modes of production (Feudalism)
  Exotic-Mwalimu aliyepewa jina baada ya kufundisha exotic breeds of livestock
   
 9. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  "Ni Kwamba"--huyu alikuwa mwalimu wetu wa Siasa enzi hizo. Alikuwa kila baada ya sentesi 2 anatumbukiza "ni kwamba",siku moja tukaamua kumuhesabia hizo ni kwamba zinakuwa ngapi ktk kipindi cha dk 45;jamaa yetu akahesabu zikafika 78,basi ndo likawa jina lake hilo.
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kibanga ampiga mkoloni
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Von soden= mwalimu wangu wa history la sita (topic ya scramble for and partition of africa)
  Diki short form ya DICTATOR= rector wangu secondary alikuwa mkali dunia nzima
  Perfomerr= Mwalimu wangu na manual work cordinator, huyu jamaa alikuwa kama john cena ulingoni
  Maya= mwalimu wangu wa commerce na book keeping; alikuwa mtu mzima but she behaved like a teenager
  Lawino= mwalimu wangu wa literature aligombana na mumewe zikachapwa kavu kavu shuleni tena baada ya parade ya saa tisa.
  Babu= ni kawaida kwa walimu wazee
  Mandible= mwalimu wangu wa biology form three alikuwa na mdomo mpana balaa
  Kenge= huyu ticha alikuwa mkali halafu ana sura ka jiwe
  Nyerere= mwalimu wangu wa siasa la tano, mwaka mzima alifundisha juu ya azimio la Arusha
  kipipa= alikuwa mwalimu wangu wa kiingereza la nne, alikuwa binti na kiherehere usiombe ukutwe na kosa halafu upelekwe ofisini na ye awepo alikuwa na umbo la mviringo mwili mzima ka mpira.
  Kimbilio= huyu alikuwa maza angu si mnajua alikuwa ticha wa primari? alikuwa mpole na alipenda kuwatetea madenti!
  Faru huyu aliitwa Mwl Byarugaba, alikuwa akitokea kule BK kwa kina iwe, alikuwa ka faru, uwe na kosa huna ukikutana naye unakula kwenzi (nyundo). Alipenda sana kunywa "pingu" hata aubuhi alikuwa nzwi!
  Kuni= huyu mama nadhani hakuwa na bajeti ya mkaa manake kila ijumaa alituagiza kuni!

  Jamani tumetoka mbali!
   
 12. ADUI

  ADUI Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  SHAMBOKO: Alikua mwalimu wa kiingereza. Ilikua mkimuudhi na anataka kuwaadhibu kwa fimbo basi anasema 'ntawachapa sjambok' sisi tunakawa tunasikia kama amesema shamboko, ndio likawa jina lake tangu hapo.
   
 13. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  NGUDI -= Mwalimu wa kiume alikuwa kabinuka kwa nyuma
  Colloque - Mwalimu wa kiingereza
  Museveni - alikuwa discipline master mnoko zaidi ya unoko wenyewe yaani hata akicheka huwezi kuamini kuwa anacheka
  Desert - Rector alikuwa na kiupara

  Kwa kweli maisha ni safari, kwani unoko wao ndo umetufanya tufike hapa lasivyo tungeishia pabaya sana
   
 14. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mapua - headmaster wa 70s Pugu
   
 15. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Caitano--Mwalimu Mkuu Kahororo,alikuwa mkali lakini mpenda maendeleo ya wanafunzi.Alikuwa tayari kukuchapa fimbo kwa kosa ambalo ungeweza kufukuzwa shule.Jina lake Mwakyulu.

  Yesu- Mwalimu wa Kemia.

  Mabomu/Budhizim--Mwalimu wa Jiografia.
  Burugo/Fang fang-- Mwalimu wa michezo.
   
 16. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  monera -mwalimu wa bios f3
  piano-mwalimu wa eng f2
  tozi-mwl wa history f4huyu alikua anapenda kuvaa jins na tshirt na tai
  nguvu-mwl wa history1 f5huyu alikua anatumia nguvu nyingi sana kuchapa
  chaja-mwl wa lang1 f5 alikuwa anakigugumizi
  beberu-mwl wa gs f6 alipenda kuita watu beberu
  gaucho-mwl wa language f6 alikua na kichogo kikubwa sana


   
 17. Natty Bongoman

  Natty Bongoman JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbichwa ... headmaster alikuwa na k ichwa kikubwa
   
 18. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama kuna mwana Jitegemee yeyote asiyemjua DUDUWASHA huyu alikuwa displine master.Na kwa wale Azania tulimpa mwalimu wetu jina la NOMALE sababu tu alikuwa akipenda kusema normally.
   
 19. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dah, umenikumbusha mbali sana juu ya hii stori ya Kisu na ba-si alikuwa wa Iyunga Tech huyu? Aisee siyo siri jamaa ni noma ktk headmasters-Thanks Ng'wanangwa
   
 20. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  (Kangaba)=mwalimu wangu wa history form 2 kibaha sec,alipenda sana kuiongelea historia ya falme ya kangaba.(Abacha)=mwalimu wa nidhamu kibaha secondary.(Marlboro)=Mwalimu wangu wa jiografia,alipenda kuvaa kofia aina ya pama na muda wote alikuwa na sigara mdomoni.
   
Loading...