TAMISEMI yafafanua kasoro za majina ya walimu walioitwa kwenye ajira 13,000 za Magufuli

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Serikali yaanika sababu kasoro majina kwenye ajira za walimu

SERIKALI imeeleza sababu zilizochangia kuwapo kwa kasoro mbalimbali kwenye majina ya ajira za walimu 13,000 zilizowekwa kwenye tovuti hivi karibu.

Hali hiyo ilizua mjadala na maswali mengi katika mitandao ya kijamii, huku ikibainisha hatua zilizochukulia na zikazochukuliwa kuanzia jana.

Ufafanuzi huo ulitolewa jana na makatibu wakuu watatu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanaga, Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo.

Mhandisi Nyamhanga alisema kuwa kutokana na kuwapo kwa maswali mengi katika mitandao ya kijamii kuhusu majina ya walimu waliopata ajira za ualimu, wameshazifanyika kazi baadhi ya dosari.

Alisema maswali ambayo yalikuwa yakihojiwa ni mwalimu mmoja jina lake kujitokeza zaidi ya mara 196, hivyo kuibua mjadala.

“Hili tayari tumeshalifanyia kazi na hii ilitokana na tulivyokuwa tukiandaa orodha hii ili kupandisha kwenye tovuti… kuna tatizo la kiufundi lilitokea, lakini hali hii siyo kama imeathiri lolote au mwalimu huyo kuchukua nafasi za wengine 195, tumeshalifanyika kazi tumeona leo tuwaite ili kuwaeleza suala hili namna ambavyo tumelitatua,” alisema Nyamhanga.
Aidha, alisema dosari nyingine mbayo ilikuwa ikilalamikiwa ni majina ya baadhi ya watu waliopata ajira kuonekana ni wahitimu wa kidato cha nne mwaka jana.

“Tayari tumefanya uhakiki kubaini kuwa hii ilitokana na waombaji kukosea kuandika taarifa zao, wengi wao waliandika miaka waliyomaliza kidato cha nne na mwaka waliopata shahada yao basi… lakini ukweli ni kwamba hakuna mhitimu wa mwaka 2019, 2018 wala 2017 aliyechaguliwa kwenye ajira hizi,” alifafanua Nyamhanga.

Alisema kwa mujibu wa vielelezo walivyovipitia, kwa waliochaguliwa kupata nafasi hizo ualimu wengi wao ni wahitimu wa kidato cha nne kuanzia mwaka 2010 hadi 2014.
Vile vile, Katibu Mkuu huyo alisema wanaendelea na uhakiki wa majina yote ili kujiridhisha kama ni watu wanaostahili na kuondoa dosali zote.

“Uhakiki huu utaanza leo (jana) na tunatarajia ukamilike ndani ya siku mbili ili watakaostahili waripoti katika maeneo yao na kupatiwa stahiki zao kama ambavyo taarifa ya awali ilivyokuwa inabainisha,” alieleza.

Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema wao ndio wenye mamlaka ya kutoa vibali vya ajira na katika mwaka huu wa fedha, jumla ya walimu 13,000 watapatiwa ajira.
Alisema katika ajira hizo 13,000, walimu 8,000 ndiyo ambao majina yao yametolewa kwenye mtandao na wengine 5,000 watatangazwa baadaye.

Akizungumza kuhusu uhakiki, Dk. Ndumbaro alisema walimu ambao watabainika kuwa wamepata nafasi hizo kwa udanganyifu wataondolewa, na nafasi zao kupatiwa mtu mwingine mwenye sifa.

“Mfumo huu uliotumika kuomba ajira kuna baadhi ya walimu ambao walikuwa ni wa Historia, lakini wamejaza na somo la Hisabati ili mfumo uwatambue,” alisema na kuongeza:

“Sasa niseme tu kwa yeyote atakayebainika amepata ajira kwa somo ambalo hajalisomea, ataondolea na kumzuia asipate tena ajira serikalini.”

Chanzo: NIPASHE
 
Majibu mazuri Sana kutoka kwa viongozi wetu lkn yananipa mashaka mpaka Sasa mifumo yetu haiwezi kudhibitiwa ikatoa taarifa sahihi hatari Sana
UCHUMI WA KATI
 
Hizo nna za formfour vp if walikosea mwaka wa kumaliza ualimu vipi iathiri namba zao zamitihani form four.
 
Mkuu upo Bar saivi?
Amemaanisha vipi kuhusu ufaFanuzi juu ya namba zao za form four kuwa tofauti, maana mheshimiwa ametolea ufafanuzi kwenye mwaka kwamba yawezekana watu kukosea kuandika mwaka wa kuhitimu sasa je na hii ya kukosewa au kuandikwa namba ya mtu mwingine nayo walikosea au vipi?
 
Haya ni majibu baada ya mikadala kuibuka! Hii inaonesha nini? Inaonesha kuwa Makatibu wakuu wanaosimama hapo kwaajili ya kumuwakilisha Rais Magufuli , hawafai na wanatakiwa watoke ,,wapishe watu wengine wachukue nafasi.

Utaachiaje majina yenye makosa makubwa zaidi mtandaoni? Hawana utaratibu wa uthibitisho ama kuhakiki kabla ya kuyatoa hewani? Hii ni janja janja
 
Jamii isingeibua madudu haya, where would these sheer explanations be delivered to?
 
Kutokana na madudu yaliyojitokeza kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa wiki iliyopita, pamoja na utetezi dhaifu ulitolewa na wahusika kutokana TAMISEMI, Wala haihitaji akili kubwa kujuwa kuwa kuna harufu ya Rushwa na watu kubebana

Tena mbaya watu kubebwa ingawa hawakuwa na sifa. Kulikuwa na waombaji zaidi ya 200,000 wenye sifa, Sasa Kati ya waombaji laki 200,000 unawezaje kuhangaika na mtu ambaye umebaini kwamba alikosea namba yake ya Kidato Cha Nne, Mtu aliyechagua masomo ambayo hakusoma (mfano hesabu wakati alisoma kiswahili) n.k

Tukiendekeza huu ujinga tunakoelekea ni kulitumbukiza Taifa la Tanzania katika shimo.

Rais ondoa huu uchafu pale TAMISEMI ili kufanya serikali yako kuaminika zaidi.
 
Hizi bangi tu,unafanyaje makosa Kama haya, kwani hizo data zinajiweka automatic zenyewe?na baada ya kuweka,kwanini hamkuhakiki?
Ma PHD uchwara
 
Binafsi nilishakubali kuwa Mpumbavu kwa hawa viongozi wa Serekale

Inawezekanaje mfumo ulio rasmi ukakubali kupokea taarifa zisizo na Ukweli za Kitaaluma? Mfano mdogo tu ni kwenye kuomba nafasi za chuo, ukikosea herufi moja tu inakukataa huwezi kuendelea kuomba kujisajili chuo kwa hatua ya mwanzo. Hili liliwezekanaje!?
 
Back
Top Bottom