Naamini hii ni kazi ya shetani na inawezekana inafanywa na kikundi kidogo cha watu ndani ya nchi yetu wenye madhumuni yafuatayo: -
1. Kujaribu kuonyesha kwamaba serikali ya JK ni ya kidini na imeshindwa kulinda dini mojawapo na kutetea dini ingine.
2. Kujaribu kudhoofisha kwa makusudi juhudi za serikali na CCM ionekane imeshindwa kabisa kumlinda mtanzania na kuwa inafaa iondolewe madarakani. Na katika hili inawezekana wahusika wapo ndani ya CCM ama Serikalini wakitumika kwa namna moja ama nyengine na shetani huyu aliyekaa pembeni akitutazama jinsi tunavyohangaika wenyewe kwa wenyewe na kupakana ubaya na uadui kwa faida yake na genge lake. Na katika hili naweza kabisa kuhisi ni mbio za uraisi wa 2015 na si vinginevyo.
Hawa watu wanaotumika na shetani wanaweza kabisa kuwa kutoka dini ama dhehebu lolote kwa kuwa wanapata ujira kwa maslahi binafsi na si kwa taifa wala dini yoyote.
Ni wakati sasa kwa serikali na CCM kujitazama upya na kujitafakari sana inawezekana ndani yake kuna mamluki wanaofanya kazi kama nyoka wa ndimi 2 si hivyo tu bali itakapofahamika wahusika si kucheka nao bali waletwe hadharani na wanyongwe bila huruma.