Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000

Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
2,296
Reaction score
5,248
20260512_180234.jpg

#HABARI Kijana mmoja mfanyabiashara mkazi wa Mbugani Jijini Mwanza, anayejulikana kwa jina la Mzafaru Yunus (26), amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa kikatili ndani ya Baa iliyopo Kona ya Bwiru, Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, kufuatia kushindwa kulipa bili ya vinywaji yenye thamani ya Sh 8,000.

Tukio hilo limeibua taharuki miongoni mwa wakazi huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likiwashikilia watu tisa wanaodaiwa kuhusika, wakiwemo walinzi wawili maarufu kama mabaunsa.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema marehemu alishambuliwa kwa ngumi, mateke, vipande vya mbao pamoja na bomba la chuma sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza maisha.

Soma Pia: Arusha: Polisi auawa na wananchi akidhaniwa kuwa mwizi, Sita wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Amesema miongoni mwa waliokamatwa ni meneja wa baa hiyo, wafanyakazi wa usafi na walinzi wawili, huku watuhumiwa wengine wakidaiwa kutoroka kabla ya kukamatwa na polisi wanaoendelea na uchunguzi wa tukio hilo. #EastAfricaTV
 
Mabaunsa kila siku natamani kuwaambia msijifanye makamanda sana kupitiliza..ona sasa unaamkia mahabusu BUTIMBA na kesi ya MURDER
Kaka usiwe unayaambia hayo majamaa ,ni mabishi sana alafu yanaringa .
Siku ukijaa kwenye hamsni zao ,yanapiga kweli kweli alafu yanapiga sehemu sensitive kabisa
 
Kaka usiwe unayaambia hayo majamaa ,ni mabishi sana alafu yanaringa .
Siku ukijaa kwenye hamsni zao ,yanapiga kweli kweli alafu yanapiga sehemu sensitive kabisa
Hayajui kumuadhibu mtu kuzingatia pressure points...mwaka 2021 nilikua bar moja hapo kona ya bwiru kuna jamaa walimdunda sana hadi nikahama bar za namna hyo...nikahamia club kubwa tu CLUB ELEVATE na THE CASK
 
Hayajui kumuadhibu mtu kuzingatia pressure points...mwaka 2021 nilikua bar moja hapo kona ya bwiru kuna jamaa walimdunda sana hadi nikahama bar za namna hyo...nikahamia club kubwa tu CLUB ELEVATE na THE CASK
Ulifanya vizuri kabisa kaka .
Yaani bar zenye mibaunsa yenye nguvu usipende kwenda unaweza kujichanganya yakakudunda kipigo cha mbwa mwizi
 
Mmiliki kapoteza kila kitu hapo, probably wote wataishia jela for life, make sure ukiajiri unatoa mafunzo kwa wafanyakazi wako ili kuzuia disaster kama hizi, ujumbe kwa mabaunsa kazi yenu ni kudhibiti sio kupiga na kuumiza au kuua mtaishia jela na kuharibu maisha yenu
 
Back
Top Bottom