msomi uchwara
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 4,795
- 9,162
Ila like tangazo la ukimwi like! Mpaka leo hii linanirudia kichwani.
Ule wimbo ilikua na wasanii walio Tunga na kuimba vizuri.
Usione soo sema nae kuhusu kusubiri ama kutumia kondom.
Kila mwenye simu alionekana ana mobitel, Mobitel ilikuwa ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi. Kwa hiyo ukiwa na simu ya mkononi utasemwa una mobitel. Ilipelekea mwanamuziki mmoja wa kike mnenguaji kuitwa kimobitel
😁😁😁😁Miaka hiyo Mr nice na Dudubaya wametupa sana burudani. Nakumbuka Songea miaka hiyo kuna chimbo moja lilikua linaitwa Buhemba. Bata zote zipo hapo. Ujambazi ulikua wa kutosha miaka hiyo songea. Watoto tulikua tunainjoi sana maisha ukiamka asubuhi unaenda unaenda uwanjani tunaanza kucheza mpira..mchana tunaenda kuogelea jioni kuruka sarakasi kwenye mapumba ya mpunga, tunaporudi tunapitia makaburini kwenda kutikisa maembe hatujali makaburi wala nini
98 niliwachukia sanaa ufaransa baada ya kuwapiga brszil😁😁😁😁Kama tulivyokuwa tunashindana kamari za sticker za Ronaldo de Lima ktk bigijii, ukimpata delima kwenye sticker, unaongezewa bigijii nyingine, hilo ni kombe la dunia la mwaka 1998 na la mwaka 2002.
AixeeeMiaka hiyo kuingia south ilikua simple SANA na pesa ilikuwepo bongo MPAKA south kwenye we, huwa nawahurumia vijana WA Sasa wanao pambana KUTAFUTA pesa MPAKA wakjibinue mitandaoni MABINTI MPAKA kuuza nyapu na KUJIOneSHA insta ILIHALI miaka hiyo Kuna wakina mama walitengeneza pesa kupitia KAZI ZAO za KAWAIDA TU, namkumbuka mama MMOJA pale GEITA ujenzi KanISA la roman Catholic, alichangia mifuko mia nne MZEE peke yake, ni mfanya biashara TU enzi HIZO, ALAFU alikua muislamu alikua anaitwa mama KULWA ana WATOTO mapacha wote wakike, enzi hizo Leo hii makando kando KIBAO udangaji usi seme
Shule mlikuwa manenda sangapi? Bombambili oyeeMiaka hiyo Mr nice na Dudubaya wametupa sana burudani. Nakumbuka Songea miaka hiyo kuna chimbo moja lilikua linaitwa Buhemba. Bata zote zipo hapo. Ujambazi ulikua wa kutosha miaka hiyo songea. Watoto tulikua tunainjoi sana maisha ukiamka asubuhi unaenda unaenda uwanjani tunaanza kucheza mpira..mchana tunaenda kuogelea jioni kuruka sarakasi kwenye mapumba ya mpunga, tunaporudi tunapitia makaburini kwenda kutikisa maembe hatujali makaburi wala nini
Hahah mkuu shule ilikua sio kila siku maana kipindi kile unakuta mtu yuko primary lakini anawaza kusaka pesa. Mwaka 2004 tulikua tunafunga shule, mimi nilikua mashujaa shule ya msingi, tulikuja kucheza na bombambili primary. Tulijichanganya kuanzisha vurugu walitupiga vibaya sana. Kovu la kile kipigo ninalo hadi leo mkononi.Shule mlikuwa manenda sangapi? Bombambili oyee
98 niliwachukia sanaa ufaransa baada ya kuwapiga brszil😁😁😁😁
Ndio maana una akili za kitoto sana😁😁Nakumbuka kipindi hicho 2001 ndio mama ananizaa, ilikuwa usiku tena alikuwa peke yake nyumbani,ndani ya nyumba ya makuti ikiwa imemulikwa na mwanga hafifu wa kibatari,akashikwa na uchungu,akajiegamiza kwenye nguzo akanizaa na akakata kondo peke yake,mzee alikuta tu mwamba Jaga Kaya Ogihonge analia. Nilifurahi sana siku hiyo ya kuzaliwa
🔥🔥🔥🔥Kipindi Bora kabisa dunia imewahi kupitia ni 2000s hadi 2010
Filamu
Jumba la dhahabu ya Tuesday Kihangala
Shumileta na Nsyuka ya Musa Banzi na Sultan Tamba
Johari njia panda ya ray na kanumba
Misukosuko ya J bras na Seba
Muziki
1. Juma nature na hakuna kulala, ugali, mugambo wanaruka na kukanyagana
3. Temba na chege na Tmk wanaume family na Dar mpaka Moto
4. Mb Dogg na sagabrasha, latifa
5. Z anto na bint kiziwi na mpenzi jini
6. Ferooz na profess J state he
7. Mandojo na domokaya bila kusahai sog dogg
TV NA RADIO
1. Chemsha bongo ya redio one stereo
2. Mizengwe ya ITV
3. Nani zaidi ya redio one
4. Kwetu fleva ya DJ majizo ya magic FM
5. Mchezo ya Mzee jangala radio Tanzania
6. Matangazo ya chai Jaba na fataki na funda moja la ziada litakuumbua
7. Channeli ya C2C mtu kwao ilikuwa inapiga muziki balaa
8. Redio free afrika na kipindi cha sitasahau na je huu ni uungwa cha fredwaa
Kulikuwa ni kipindi cha dhahabu kwa kweli haitakaa itokee, sasa hv ni kama vile kila kitu kimepoteza mvuto
Daah maxx 🥲🥲Marehemu max..zembwela..kingwendu..kumsaka nyoka mwenyew vichwa Saba kanda ilikua ya VHS
AaahNdio maana una akili za kitoto sana
Golikipa wa Argentina aliyedaka michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 1998 anaitwa Carlos Roa, alikataa kusajiliwa na timu yoyote kuanzia mwaka 1999 akiamini mwaka 2000 ni mwisho wà Dunia😄Waliozaliwa '95 kuja hivi walizaliwa nyakati ambazo ukimwi ulikuwa tishio sana. Wengine walizaliwa nao na baadhi nadhani kwa sababu dawa hazikuwa kwa wingi walifariki mapema tu.
Tulibahatika kushuhudia Y2K, kwamba 2000 inaweza kuwa mwisho wa dunia.
Puff DadyEnzi hizo kuitwa P. diddy ulikua ni unyama sana tofauti na sasa hivi.