Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Miaka hiyo kuingia south ilikua simple SANA na pesa ilikuwepo bongo MPAKA south kwenye we, huwa nawahurumia vijana WA Sasa wanao pambana KUTAFUTA pesa MPAKA wakjibinue mitandaoni MABINTI MPAKA kuuza nyapu na KUJIOneSHA insta ILIHALI miaka hiyo Kuna wakina mama walitengeneza pesa kupitia KAZI ZAO za KAWAIDA TU, namkumbuka mama MMOJA pale GEITA ujenzi KanISA la roman Catholic, alichangia mifuko mia nne MZEE peke yake, ni mfanya biashara TU enzi HIZO, ALAFU alikua muislamu alikua anaitwa mama KULWA ana WATOTO mapacha wote wakike, enzi hizo Leo hii makando kando KIBAO udangaji usi seme
 
Ndio miaka ambayo muziki wa bongo fleva unashika hatamu kwenye anga la Tanzania na kuishusha miziki ya congo, dansi na taarabu. Mdj wakali wakali kama kina sebastian maganga, abubakary sadiki wanaibuka kuupiga sana muziki wa bongo fleva katika vituo vya redio
Na bongo fleva ya mwaka 2000 ilikuwa na ujumbe na mafunzo, siyo bongo fleva ya sasa, matusi matupu yanayoharibu maadili ya watoto wetu.
 
Basi ulikuwa wakishua wajuba tulikuwa enzi hizo games na movies mpaka vibanda umiza , majirani Wenye Tv masharti kibao wanavimba
Sisi baba alinunua TV mwaka 1995 iliitwa Hitachi, ya chuma. Ikaja kufa mwaka 2008, eneo tulilloishi, ni familia mbili tu ndo zilikuwa na TV, kwahiyo majirani wrote wakawa wanakuja kutazama, watu wanajaa hadi kero.
 
Kulikua na bifu la kibonzo Zena na betina gazeti la sani.
Sani nilikuwa nalinunua kila jumamosi, pia kaka yangu alikuwa mchora katuni gazeti la Alasiri, katuni anaitwa dogo, mfupi halafu kichwa chake kimepigwa pasi juu.
 
Kama tulivyokuwa tunashindana kamari za sticker za Ronaldo de Lima ktk bigijii, ukimpata delima kwenye sticker, unaongezewa bigijii nyingine, hilo ni kombe la dunia la mwaka 1998 na la mwaka 2002.
 
Eneo gani hilo ulikuwa unaishi? Ni Dar hii hii kweli? Mbona limechelewa hivyo, yaani mwaka 2005 TV ziwe za kuhesabu duh, sisi tunayo tangu 1995.
 
Back
Top Bottom