Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Miaka hiyo Mr nice na Dudubaya wametupa sana burudani. Nakumbuka Songea miaka hiyo kuna chimbo moja lilikua linaitwa Buhemba. Bata zote zipo hapo. Ujambazi ulikua wa kutosha miaka hiyo songea. Watoto tulikua tunainjoi sana maisha ukiamka asubuhi unaenda unaenda uwanjani tunaanza kucheza mpira..mchana tunaenda kuogelea jioni kuruka sarakasi kwenye mapumba ya mpunga, tunaporudi tunapitia makaburini kwenda kutikisa maembe hatujali makaburi wala nini
 
Ila like tangazo la ukimwi like! Mpaka leo hii linanirudia kichwani.

Ule wimbo ilikua na wasanii walio Tunga na kuimba vizuri.

Usione soo sema nae kuhusu kusubiri ama kutumia kondom.

Namkumbuka msanii Raha P kwenye huu wimbo, alikuwa kifaa sana yani kabla ya kukutana na bwana tapeli akamzamisha US akapotea na usingle mom, hope kajipanga sasa baada ya lijamaa kuzalisha na kupigwa lupango kwa drugs!
 
acfc6f51-b743-4aa9-83b3-eea6ac090354.jpeg
 
Miaka hiyo Mr nice na Dudubaya wametupa sana burudani. Nakumbuka Songea miaka hiyo kuna chimbo moja lilikua linaitwa Buhemba. Bata zote zipo hapo. Ujambazi ulikua wa kutosha miaka hiyo songea. Watoto tulikua tunainjoi sana maisha ukiamka asubuhi unaenda unaenda uwanjani tunaanza kucheza mpira..mchana tunaenda kuogelea jioni kuruka sarakasi kwenye mapumba ya mpunga, tunaporudi tunapitia makaburini kwenda kutikisa maembe hatujali makaburi wala nini
😁😁😁😁
 
Kama tulivyokuwa tunashindana kamari za sticker za Ronaldo de Lima ktk bigijii, ukimpata delima kwenye sticker, unaongezewa bigijii nyingine, hilo ni kombe la dunia la mwaka 1998 na la mwaka 2002.
98 niliwachukia sanaa ufaransa baada ya kuwapiga brszil😁😁😁😁
 
Miaka hiyo kuingia south ilikua simple SANA na pesa ilikuwepo bongo MPAKA south kwenye we, huwa nawahurumia vijana WA Sasa wanao pambana KUTAFUTA pesa MPAKA wakjibinue mitandaoni MABINTI MPAKA kuuza nyapu na KUJIOneSHA insta ILIHALI miaka hiyo Kuna wakina mama walitengeneza pesa kupitia KAZI ZAO za KAWAIDA TU, namkumbuka mama MMOJA pale GEITA ujenzi KanISA la roman Catholic, alichangia mifuko mia nne MZEE peke yake, ni mfanya biashara TU enzi HIZO, ALAFU alikua muislamu alikua anaitwa mama KULWA ana WATOTO mapacha wote wakike, enzi hizo Leo hii makando kando KIBAO udangaji usi seme
Aixeee
 
Miaka hiyo Mr nice na Dudubaya wametupa sana burudani. Nakumbuka Songea miaka hiyo kuna chimbo moja lilikua linaitwa Buhemba. Bata zote zipo hapo. Ujambazi ulikua wa kutosha miaka hiyo songea. Watoto tulikua tunainjoi sana maisha ukiamka asubuhi unaenda unaenda uwanjani tunaanza kucheza mpira..mchana tunaenda kuogelea jioni kuruka sarakasi kwenye mapumba ya mpunga, tunaporudi tunapitia makaburini kwenda kutikisa maembe hatujali makaburi wala nini
Shule mlikuwa manenda sangapi? Bombambili oyee
 
Shule mlikuwa manenda sangapi? Bombambili oyee
Hahah mkuu shule ilikua sio kila siku maana kipindi kile unakuta mtu yuko primary lakini anawaza kusaka pesa. Mwaka 2004 tulikua tunafunga shule, mimi nilikua mashujaa shule ya msingi, tulikuja kucheza na bombambili primary. Tulijichanganya kuanzisha vurugu walitupiga vibaya sana. Kovu la kile kipigo ninalo hadi leo mkononi.
 
Maisha ya zamani yalijaa ufukara na umaskini uliopitiliza. Nakumbuka tu barabara ya kona Mbauda - Mromboo ilikuwa vumbi. Kaloleni kulikuwa na nyumba kibao za udongo. Viwanja vya Soweto vilikuwa wazi kwa wananchi wote kufanyia mazoezi. Matukio ya ujambazi yalikuwa yamekithiri Arusha. Mtoto mdogo aliuwawa kwenye kontena la Vodacom mwaka 2004. Huyu Banjoo ambaye kwa sasa ni shujaa wa CHADEMA alikuwa jambazi hatari. Miaka hiyo pia nilikuwa mnufaika wa Takrima iliyotolewa na Godbless Lema maeneo ya Mbauda.
 
Brazil si alitoka kushinda kombe la dunia kwa mara ya nne mwaka 1994, sasa unataka awe anashinda kila kombe? 1994 baada ya Muitali Roberto Baggio kukosa penalty, ndo ikaipa ushindi Brazil.

Sasa 1998, Brazil alipigwa 3-0 na ufaransa ktk fainali, mbili Zidane, moja Emmanuel Petit goli la tatu, na ufaransa ikawa ndo mara ya kwanza kushinda kombe, so waachie tu. Brazil ikashinda tena kombe la dunia kwa mara ya tano mwaka 2002. Kizazi cha wachezaji wa kipindi hicho mpaka kuja 2010 hivi, sidhani kama kutakuja kutokea.
98 niliwachukia sanaa ufaransa baada ya kuwapiga brszil😁😁😁😁
 
Nakumbuka kipindi hicho 2001 ndio mama ananizaa, ilikuwa usiku tena alikuwa peke yake nyumbani,ndani ya nyumba ya makuti ikiwa imemulikwa na mwanga hafifu wa kibatari,akashikwa na uchungu,akajiegamiza kwenye nguzo akanizaa na akakata kondo peke yake,mzee alikuta tu mwamba Jaga Kaya Ogihonge analia. Nilifurahi sana siku hiyo ya kuzaliwa
Ndio maana una akili za kitoto sana😁😁
 
Kipindi Bora kabisa dunia imewahi kupitia ni 2000s hadi 2010

Filamu
Jumba la dhahabu ya Tuesday Kihangala
Shumileta na Nsyuka ya Musa Banzi na Sultan Tamba
Johari njia panda ya ray na kanumba
Misukosuko ya J bras na Seba

Muziki
1. Juma nature na hakuna kulala, ugali, mugambo wanaruka na kukanyagana
3. Temba na chege na Tmk wanaume family na Dar mpaka Moto
4. Mb Dogg na sagabrasha, latifa
5. Z anto na bint kiziwi na mpenzi jini
6. Ferooz na profess J state he
7. Mandojo na domokaya bila kusahai sog dogg

TV NA RADIO
1. Chemsha bongo ya redio one stereo
2. Mizengwe ya ITV
3. Nani zaidi ya redio one
4. Kwetu fleva ya DJ majizo ya magic FM
5. Mchezo ya Mzee jangala radio Tanzania
6. Matangazo ya chai Jaba na fataki na funda moja la ziada litakuumbua
7. Channeli ya C2C mtu kwao ilikuwa inapiga muziki balaa
8. Redio free afrika na kipindi cha sitasahau na je huu ni uungwa cha fredwaa

Kulikuwa ni kipindi cha dhahabu kwa kweli haitakaa itokee, sasa hv ni kama vile kila kitu kimepoteza mvuto
🔥🔥🔥🔥
 
Waliozaliwa '95 kuja hivi walizaliwa nyakati ambazo ukimwi ulikuwa tishio sana. Wengine walizaliwa nao na baadhi nadhani kwa sababu dawa hazikuwa kwa wingi walifariki mapema tu.

Tulibahatika kushuhudia Y2K, kwamba 2000 inaweza kuwa mwisho wa dunia.
Golikipa wa Argentina aliyedaka michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 1998 anaitwa Carlos Roa, alikataa kusajiliwa na timu yoyote kuanzia mwaka 1999 akiamini mwaka 2000 ni mwisho wà Dunia😄
 
Back
Top Bottom