Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Daaah Umenikumbusha WestLife Coast to Coast Album - My Love ilikuwa balaaa Radio One lazima aipige ABoubakar Sadiq.

Umenikumbusha Celin Dion wa woto balaa ,kila basi la kwenda Mkoani lazima wawe na Album ya Celin yaani bandika bandua I Love You ,It's all coming back to me ,Because you loved me ,My heart will go On ,immortality ,Tell Him ,When i need you.

Dr Cheni ,Nora Ngwizukulu ,Max Zembwela ,Shigongo na magazeti yake yaani WAMOTO.
I miss the old days bro😢
 
Miaka hiyo kulikuwa na tv chache kama DTV na ndugu zake kina,CTN channel ten na C2C, naona imebaki channel ten tu na imekuwa mali ya CCM. Media zingine ilikuwa ni ITV, Star tv na TVT ambayo kwa sasa ni TBC1. Tv bora wakati huo ilikuwa ni ITV tu ndio ilikuwa na watazamaji wengi kutokana na vipindi vyake na mawimbi ya upatikanaji wake. Huu ni upande wa tv kwa wakati huo
Loth lema unakuambuka ITV2 ambayo baadae ikawe channel 5
 
We utakuwa mdau wa baba ubaya,Kaboka mchizi na Faza hausi.
Nakumbuka tu baba ubaya😂 kuna fidodido na kipepe na kiokote😆😆
13E82456-CC8A-4559-9722-FE5CA4E3896B.jpeg
 
Basi ulikuwa wakishua wajuba tulikuwa enzi hizo games na movies mpaka vibanda umiza , majirani Wenye Tv masharti kibao wanavimba
1990'S Watu wanatoka Kigogo,Buguruni, Manzese etc kwenda kuangalia Kideo Magomeni Mapipa maana ndio kulikuwa na don mwenye nacho.
Mtaani ni mwendo wa zile Cinema za mkanda kama projector, Watu wanazunguuka mtaani na megaphone kutangaza ukumbi flani kutakuwa na show kuanzia saa 12 jioni Trailer Charlie Champlin.
2000 Manzese na Tandale zilikuwa balaa kuonyesha pilau yaani xnxx,xhamster ni manzese mzee miaka hiyo ubao unaandikwa pilau au picha la kutisha then watu wanatoka wameshusha fulana na mashati yao mapajani.
Uwanja wa fisi pia ulikuwa unatrend
 
Pia nakumbuka kwenye yale magazeti ya Udaku ni lazima ukute Lyrics ya nyimbo za nje.

Tulichana sana vipande vyenye nyimbo za WestLife, kina Rehana, Brandy na wengine wengi.

Kwetu tulikuwa na daftari special ya kubandikia hizo nyimbo ili tukiwa hatuna kazi na mama hayupo tusikilize tuimbe.

Uwiiii tulijua kuzikariri. Lol.
 
Mi nakumbuka enzi hizo Radio za Cassette ndo zilikuwa zimepamba moto.

Kwa sisi wa Uswahilini tulikuwa na Cassete kibao za wanamuziki sio wa ndani hadi wa ndani.
Hapo Ukute zimejaa za Tabu Ley,Bozi Boziana,Pepe Kalle,Samba Mapangala,Franco,Koffi,
 
Shadeeya wadada walikuwa wanapenda sana za Shania Twain,Ton Braxton,Celine Dion,Keith Sweat, Lione Richie na Wacko Jacko.
Lang'ata Sociall ulikuwa unaijua au ulikuwa mporipori?
 
Back
Top Bottom