Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Tujikumbushie matukio na mambo ya miaka 2000

Miaka hiyo liliibuka bifu la wanamuziki wa bongo fleva wawili wa kike, Zay B na Sister P. Wakaanza kutungiana nyimbo kupeana makavu bila chenga, nyimbo zikaenda hewani maredioni na kupokelewa vema na mashabiki wao. Bifu likawa zito ikabidi waandishi wa habari wawakutanishe ana kwa ana waombane msamaha ugomvi uishe. Mmoja akawa hataki 'maridhiano' tifu likabaki vilevile. Haijulikani bifu lao liliishaje na hao wanamuziki haijulikani kama wapo kwenye game au waliishaachana na muziki, bila shaka umri umesonga na wako nje ya game la muziki
Kulikua na bifu la kibonzo Zena na betina gazeti la sani.
 
Waliozaliwa '95 kuja hivi walizaliwa nyakati ambazo ukimwi ulikuwa tishio sana. Wengine walizaliwa nao na baadhi nadhani kwa sababu dawa hazikuwa kwa wingi walifariki mapema tu.

Tulibahatika kushuhudia Y2K, kwamba 2000 inaweza kuwa mwisho wa dunia.
Inaweza? Wakati watu waliuza mifugo yao na mali zao zote😆😆😆
 
Katuni za kwenye magazeti nilikuwa napenda sana, magazeti ya ijumaa mzee akileta nasoma story na miziki page za mwisho😆, kukata picha za wasanii na kubandika kwneye daftari uwii🫣
 
Wazazi walikuwa hawapendi tukae kae mtaani kwa hiyo waliweka means za kutufanya tukae ndani kama hivyo tunaletewa games tofauti tofauti kwenye computer ya nyumbani

Ushua? Sidhani 😂
Labda sababu Mimi nilikuwa mitaa ya uswahilini sana choka mbaya ila nilipoanza kujielewa kuanzia 2005 ilienda mpaka 2009 hivi watu wenye Tv ni wakuhesabu mtaani . Kompyuta na ma games ndio kabisa unaweza kuta nyumba mbili tu mtaani ndio maana tulikuwa tunawaona washua .
 
Labda watu walikuwa wanatuona hivyo lakini binafsi naona maisha yetu nyumbani yalikuwa ya kawaida sana 😆
 
Hii ndio miaka millenials wapo primary and secondary huku bado wadogo zao gen z wapo kwenye mifuko na mayai🤣

Miaka hio tunsulzana mbna isidingo Haiishi maana tangu late 90s watu wanaangalia😬

Miaka 2000 ndio ilikuwa golden age ya burudani na media katika nchi hii

Between 2000 hadi 2009 taifa lilikuwa limeshatengeneza watu ambao leo ni legends katika taifa hili.

Maigizo/mchezo ya kaole ndani ya ITV, pale ndipo tulipomtambua kanumba na ray, hadi wao kuanza safari ya filamu. Ile filamu ya girlfriend ya wakina TID ilishika kasi sana😁

Nakumbuka kanda za albamu za wasanii zilimiminika katika nyumba za watu, mimi binafsi nakumbuka albamu ya wachuja nafaka, ile nyambizi ya dully sykes, maisha na muziki ya mr 2, etc zilikuwa pale home.

Miaka 2000 star wa mpila alikuwa juma kaseja, huku mastaa wengine wakiwa wakina sunta, huyu dada ambae alitaka kula hela za mengi zote😁,

Miaka 2000 ilikuw na original comedians, wakina kibakuli🤣, bambo, pembe, joti na mpoki pamoja wakifanya vituko😂

Miaka ya 2000 yalitokea matangazo ya TV maarufu, kama chai jaba, lile tangazo la wasanii kuimba usione soo sema nae nafikiri kampeni ya ugonjwa wa ukimwi, alafu matangazl ya condom yalikuwa mengi sanaa maana ukimwi ulikuwa mkali 🤣

Miaka ya 2000 ujambazi hatarii, kuna tukio moja la kuvamia benk hata itv walionesha tena kwa kuiba kuiba marisadi yanapiga (taarifa ya habari)
View attachment 3536714
View attachment 3536715
View attachment 3536717
Daaah Umenikumbusha WestLife Coast to Coast Album - My Love ilikuwa balaaa Radio One lazima aipige ABoubakar Sadiq.

Umenikumbusha Celin Dion wa woto balaa ,kila basi la kwenda Mkoani lazima wawe na Album ya Celin yaani bandika bandua I Love You ,It's all coming back to me ,Because you loved me ,My heart will go On ,immortality ,Tell Him ,When i need you.

Dr Cheni ,Nora Ngwizukulu ,Max Zembwela ,Shigongo na magazeti yake yaani WAMOTO.
 
Miaka hiyo liliibuka bifu la wanamuziki wa bongo fleva wawili wa kike, Zay B na Sister P. Wakaanza kutungiana nyimbo kupeana makavu bila chenga, nyimbo zikaenda hewani maredioni na kupokelewa vema na mashabiki wao. Bifu likawa zito ikabidi waandishi wa habari wawakutanishe ana kwa ana waombane msamaha ugomvi uishe. Mmoja akawa hataki 'maridhiano' tifu likabaki vilevile. Haijulikani bifu lao liliishaje na hao wanamuziki haijulikani kama wapo kwenye game au waliishaachana na muziki, bila shaka umri umesonga na wako nje ya game la muziki
Bila shaka ni wazee sasa.
 
Back
Top Bottom