Tujikumbushe vitabu vya zamani

Tujikumbushe vitabu vya zamani

Mkuu hivi kwa kizazi chetu vijana unaona kuna dalili za kuendeleza uandishi kweli au ndio hivo tena tutaendelea kusoma kazi za wazee wetu.
Mkuu kwanza kupata mwandiko ulinyooka sasa hivi ni shida, watu wameharibiwa na smart phones. Tulijitahidi kuwa mwandiko wa kuridhisha kwasababu barua ilikuwa njia kuu ya mawasiliano. Hii ndiyo sababu yule mwana mama aliendakika vitabu vya Harry Porter alipata umaarufu na sifa nyingi kwa kurudisha vijana kwenye tabia ya kupenda kusoma. Watoto wa siku hizi wanaangalia tamthilia na kuchezea video games.
 
Mkuu kwanza kupata mwandiko ulinyooka sasa hivi ni shida, watu wameharibiwa na smart phones. Tulijitahidi kuwa mwandiko wa kuridhisha kwasababu barua ilikuwa njia kuu ya mawasiliano. Hii ndiyo sababu yule mwana mama aliendakika vitabu vya Harry Porter alipata sifa sana, kurudisha vijana kwenye tabia ya kupenda kusoma. Watoto wa siku hizi wanaangalia tamthilia na kuchezea video games.
Bahati mbaya siku hizi tunasoma vitabu ili kujibu mitihani na tukishafaulu tunatupa kule.Binafsi nina mswada ulio tayari kuchapwa lkn mfuko hautoshi.Nimejikongoja hadi kwa wahariri na nimekamilisha kulipia
na kilichobaki ni kujaza mkataba wa kuanza kuchapa lkn sina uwezo.
Niliwahi kiandika Uzi humu jf kuomba ufadhili ama mawazo yoyote namna ya kukamilisha huu mswada hatimaye kitabu lkn watu walipita kimya kimya.
 
Bahati mbaya siku hizi tunasoma vitabu ili kujibu mitihani na tukishafaulu tunatupa kule.Binafsi nina mswada ulio tayari kuchapwa lkn mfuko hautoshi.Nimejikongoja hadi kwa wahariri na nimekamilisha kulipia
na kilichobaki ni kujaza mkataba wa kuanza kuchapa lkn sina uwezo.
Niliwahi kiandika Uzi humu jf kuomba ufadhili ama mawazo yoyote namna ya kukamilisha huu mswada hatimaye kitabu lkn watu walipita kimya kimya.
Ni nini theme ya kitabu chako?
 
Zawadi tatu, debe la dhahabu, mfalme ana masikio kama ya pundà, hazina iliyozikwa, hizi ndo hadithi nilizosoma
 
Ni nini theme ya kitabu chako?
Nimezungimzia jinsi kijana anavokuwa na ndoto yake atakapokuwa mkubwa lkn anakutana na vikwazo kadhaa vinavyomhamisha kutoka kwenye lengo.Ni dhahiri kuwa walio wengi tunaishi nje ya ndoto zetu.Maeneo yanayochangia kuhama kwenye ndoto yanaweza kuwa ni kwenye familia,shule kwa maana ya shule ya msingi na selpndari Na chuo.Makundirika pia huchochea mtu kuishi nje na ndoto yake.hatimaye vipaumbele vya serikali humhamisha kijana kwenye ndoto.
Mkuu kwa kifupi nimejikita maeneo hayo huku nikionesha namna ya kutembea kwenye ndoto yako licha ya vikwazo.
 
Simu ya Kifo- Katalambula
Mzimu wa Watu wa Kale- Mohamed
Utu Bora Mkulima-
Aliyeonja Pepo-
Pepo ya Mabwege- H. Mwakyembe
Mabepari wa Venisi-
Kiu- Mohamed
Barua Ndefu Kama Hii-
Tendehogo-
Hawala ya Fedha-
Wasifu wa Siti Binti Said-
Lina Ubani-Penina Mlama
Nguzo Mama-
Njozi Iliyopotea- Mugogo
Nyota ya Rehema-
Usiku Utakapokwisha- E Kezirahabi
Fungate ya Uhuru- M. Seif Khatibu
Kuli- Shaffi A. Shaffi
Kasri ya Mwinyi Fuad- S. A. Shaffi
Kikomo- E. Musiba
Gamba la Nyoka-
Mashetani-






Tafakari...!!
Vyote vipo Ben and Company!
 
kuna kitabu fulani cha form II kinaitwa "in the beggining" by Joe Corrie was my best book @ that time
 
Vyote vipo Ben and Company!



Ahsante sana mkuu kwa taarifa. Naomba unihakikishie kama nitavipata vitabu vifuatavyo hapo kwa Ben maana navihitaji sana:
Njozi iliyopotea
Gamba la Nyoka
Pepo ya Mabwege
Mzimu wa Watu wa Kale
Rosa Misitika


Nahitaji sana kitabu cha PEPO YA MABWEGE ili nimsome kwa UPYA Dr. Harrison Mwakyembe kama mawazo yake kwenye riwaya hii kwa wakati ule ndiyo aliyonayo sasa. Niliisoma riwaya hiyo mwaka 1989...!!
Utanisaidia sana kunielekeza duka lilipo ili siku nikija Dar nitembelee duka hilo.






Tafakari...!!
 
Japokua siko katika rika la makamo. Nilivipata na bado nazitafuta kazi zingine za fasihi haswa za huyu Abdulla.
Nenda posta, mtaa wa samora, kuna bookshop inaitwa Tanzania Publishing House (TPH). Wana vitabu vingi Sana
 
Kitabu hiki:
Someni kwa furaha kitabu cha kwanza mpaka cha nne
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom