Tujikumbushe vitabu vya zamani

Tujikumbushe vitabu vya zamani

kikosi cha kisasi, Dunia uwanja wa fujo, njama,kufa na kupona. vyote vya ERISTABLAS ELVIS MUSIBA.
 
Namkumbuka sana "Omusolopagasi" alivyokuwa anapiga wale Kaa huku wakitoa mapovu!!
 
Cha Harrison Mwakyembe simo! Duka lipo IPS Building karibu na Askari Monument, ukifika utaliona Ben and Company Ltd, wanavitabu vingi sana na wanauza jumla pia!

Ahsante sana mkuu...!!
Hilo neno simo ndiyo sijaelewa maana yake au unamaanisha HUTAKI KESI...!!??
 
Ni Agoro Anduru.
nilisoma kitabu nikiwa kidato cha pili so ni ngumu kukumbuka r and l, by the way kwetu sisi hatunaga hizo, karibu kwetu unywe mavele..(maziwa) si ya hawa ngombe wenu wanaokula chipsi mayai then wanakamuliwa, ni pure milk , karibu.
 
Pili pilipili - katalambula Hussein Hassan (RIP)
 
Ndiyo ndugu yangu sitaki kesi kabisa

Haaaaaaaa haaaaaa haaaaaaa...!! Usiogope mkuu, hamna kesi hapo.

Dr Harrison Mwakyembe ni mwandishi wa riwaya pia, aliwahi andika riwaya inayoitwa PEPO YA MABWEGE miaka ya 1980...ilikuwa ni riwaya nzuri mno kwa muktadha ule...!! Kwa hiyo huitaji kuogopa kesi kwa sababu ni ukweli mtupu. Riwaya hiyo niliisoma na baadhi ya wahusika wake ni Mwapaker, Josina Simango aliyekataa kuolewa na mtoto wa Mkurugenzi Mwapaker...!! Natamani niisome tena nione kama Mwakyembe wa PEPO YA MABWEGE ni Mwakyembe huyu huyu wa leo au AMEIKANA RIWAYA YAKE KAMA MOHAMED SEIF KHATIBU ALIVYOIKANA MALENGA YAKE ILIYOITWA FUNGATE YA UHURU...!!

Tafakari...!!
 
kikosi cha kisasi, Dunia uwanja wa fujo, njama,kufa na kupona. vyote vya ERISTABLAS ELVIS MUSIBA

Dunia Uwanja wa Fujo ni cha KEZIRAHABI...!! Vitabu wa E. Musiba ni:
1: Kikosi cha Kisasi
2: Kikomo
3: Kufa na Kupona
4: Njama
5: ....nimesahau jina la kitabu chake cha mwisho...

Tafakari...!!
 
Haaaaaaaa haaaaaa haaaaaaa...!! Usiogope mkuu, hamna kesi hapo.

Dr Harrison Mwakyembe ni mwandishi wa riwaya pia, aliwahi andika riwaya inayoitwa PEPO YA MABWEGE miaka ya 1980...ilikuwa ni riwaya nzuri mno kwa muktadha ule...!! Kwa hiyo huitaji kuogopa kesi kwa sababu ni ukweli mtupu. Riwaya hiyo niliisoma na baadhi ya wahusika wake ni Mwapaker, Josina Simango aliyekataa kuolewa na mtoto wa Mkurugenzi Mwapaker...!! Natamani niisome tena nione kama Mwakyembe wa PEPO YA MABWEGE ni Mwakyembe huyu huyu wa leo au AMEIKANA RIWAYA YAKE KAMA MOHAMED SEIF KHATIBU ALIVYOIKANA MALENGA YAKE ILIYOITWA FUNGATE YA UHURU...!!

Tafakari...!!
Kazi kweli kweli! Huwa naamini sana katika amani na upendo
 
Kazi kweli kweli! Huwa naamini sana katika amani na upendo

Umechagua fungu jema, kwani meandikwa:
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana atakayemuona Bwana asipokuwa nao. Ebrania 12:14
Tena imeandikwa: Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhari toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha. Rumi 14:13

Amen Ra!
 
TINTIN
9c34ce480116c9b7afcc145fb560a5ef.jpg
 
jamani kwema kabisa, ni nani aliewahi soma kitabu cha mfalme JUHA naona ndo utawala wa JPM
 
Natumaini mu-wazima

Ni wangapi wanakumbuka kitabu cha Rosa Mistika kilichoandikwa na Kezilahabi na My Life in Crime na mwendelezo wake My Life with a Criminal hiki kilihusu jambazi aliyebobea katika wizi wa Mabank huko Nairobi.
By John kiriamiti,hahahaha long time!
 
Wajumbe, nani alisoma vitabu vile vya enzi za Kibanga Ampinga Mkoloni, Someni kwa Furaha, Nunda Mla Watu, Uza Ghali Usiuze Rahisi, Alfu Lela Ulela, Bulicheka.

Duh!! nakumbuka mbali sana.
Kuna Mtangazaji mmoja zama hizo,kama sijakosea wa RTD anaitwa Abdul Ngarawa. Alikuwa ni mtangazaji wa kipindi cha "Mazungumzo baada ya habari"kila baada ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku. Kipindi kilitoa mafundisho mazuri sana ya namna ya kuwa mzalendo wa nchi yako. Alitumia hadithi za vitabu mbalimbali mf."Tujenge nchi yetu" n.k. Natamani kipindi hicho kirudi japo muda ni ukuta!
 
Nakumbuka moja ya hizo hadithi alizokuwa akizitoa vitabuni ni ile ya "Kautipe na Utumbo wa Kuku". Nyingine ni ile ya Kimbwenelehi (Umenionea wapi) na Masurupwete (kutoka kitabu cha Mtu ni Utu cha George A. Mhina?)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom