Tujadili mila, jadi na desturi za wachagga

Tujadili mila, jadi na desturi za wachagga

Naona kaanza kujisema mwenyewe mapema!
Na jina lako (mamndenyi) linamaanisha nini kichaga?

Naona kauchuna.... mimi nijuavyo jina hili linamaanisha ...wakuja, washamba, mshamba......asiyemchangamfu..... mshamba mshamba hivi....... Samahani dada yangu sijakutukana bali ni tafsiri ya jina lako ninayoielewa.
 
mlizoea kuwaacha wake zenu pale home, hivyo baba yako anapovinjari mahali pale anamkuta mkeo ni lazima aandaliwe mlo kidogo plus kipata cha mbege, ikipanda kichwani ni lazima avunje amri, kwingine hali ngumu ya maisha unapokuwa baba hauko umekwenda tuseme nairobi inapelea mama anavunje amri ili apate mahitaji, wengine ni uzinifu tu unalazimi kufanya hivyo, sharti lililopo ukirudi ukikuta mtoto huna namna yeyote ya kufanya fujo na utaendelea kuwalea watoto wote kama kawa.

hii kali sana, kwa kweli ndio maana wachagga wote ni ndugu
 
Naona kauchuna.... mimi nijuavyo jina hili linamaanisha ...wakuja, washamba, mshamba......asiyemchangamfu..... mshamba mshamba hivi....... Samahani dada yangu sijakutukana bali ni tafsiri ya jina lako ninayoielewa.

ndivyo hivyo hivyo nilivyo hata haujakosea; si unaona hata avatar yangu mkuu wangu, nachukua mfano wa kushikiliwa na mama mkuu.
 
Ukimpiga mkeo usiku akapiga yowe basi wazee wanakuja wanakamata ng'ombe au mbuzi wanachinja usiku huo huo na kumla. Kama huna basi ujue utapigwa au utoe pesa watu wakaburudike. Infact hairuhusiwi kupiga mkeo usiku.
Baadhi ya vyakula vya asili:-
-kiburu(kiumbo)
-machalari(ndizi)
-kitawa(ndizi zilizopikwa zikasongwa na kuchanganywa na maziwa mgando)
-kimamtine(damu iliyochanganywa na maziwa mgando) jina jingine ni MLASO
-ngararimo(mahindi yaliyopikwa bila kukobolewa yakachanganywa na maharage)

Kisusio damu mbichi ya mbuzi ama ngombe inachanganywa na supu ya nyama iliochemshwa
Kitawa - ndizi na maziwa mtindi(mgando) zinasongwa pamoja nakinauwa kama uji mzito
Kiburu/Kiumbo - Ndizi zilipikwa na maharage na magadi vinasongwa pamoja kinakuwa kama uji mzito
Ngande - ndizi na soko(maharage ama kunde) zinasongwa pamoja na kuwa kama ugali unaweza kula hivyo ama ukala na nyama ilioungwa kwa mchuzi hii haiwekwi magadi
Mtori - ndizi zinasongwa na kuwekwa supu ya nyama inakuwa ka uji mzito unachanganya na nyama

Aseeee! Nyie wachaga kweli kiboko.
Nasikia magadi na ndizi ndo yamewafanya muwe na akili sana. Ndo maana kila dec lazima mpande moshi kwenda kucharge kichwa.....
..kiumbo
...kisusio
...ngararimo
...mbege
....machalari ya utumbo wa mbusi,
....some more mbege
.... Mnakunywa hela yote mpaka ya mafuta ya kurudia mjini. Mnapiga simu kwa kijana wa dukani dsm atume hela ya mafuta ya kurudia dsm.

....MOSHI: Mungu Onyesha Sehemu Hela Ilipo.....halafu akishaonyesha unarudi dec moshi kuitumia hiyo hela yote. Damn wachaga noma.
 
wataalam wanasema magadi yanaleta kansa; hivyo waambieni hata ndugu zetu waachane nayo watafute tu mbinu mbadala.
 
Mkiru, nkuu uukie kashari, nyi iho kongo, uparo au tella, au oiyo nyi mndu wo karmeli.
Ke ngiwia bana nanii!!
 
mushi wengi wapo machame, kibosho, old moshi kama nimekosea bujibuji na mkirua hata piddy watanisahihisha.

Hujakosea my sister nilitaka tu kujua specifically huyu prof anatokea eneo gani walau tuwatetee hawa wa uru maana wananyanyaswa sana kisa ni wale kina mama waliokuwa wakileta ndizi mjini sasa baada ya vita vya Kagera pale YMCA (Kwenye round about) ikawekwa sanamu ya mwanajeshi akiwa na silaha as if anataka kushoot.... lo Kina mama si wakatupa mikungu ya ndizi pale na kutimua mbio wakiogopa kupigwa risasi. Wengi walivunjika miguu sasa na ilijabainika kuwa wengi walitokea eneo la kishumundu sasa hadi mtwara ukisema unatokea kishumundu wanajua is the waste place kwa wachagga...... kumbe pako bomba kinoma!!
 
Mkiru, nkuu uukie kashari, nyi iho kongo, uparo au tella, au oiyo nyi mndu wo karmeli.
Ke ngiwia bana nanii!!

Hahhahaaaaa!!! Halya iwa mshiki oko... aiyo ndao kanyi.....
 
Hujakosea my sister nilitaka tu kujua specifically huyu prof anatokea eneo gani walau tuwatetee hawa wa uru maana wananyanyaswa sana kisa ni wale kina mama waliokuwa wakileta ndizi mjini sasa baada ya vita vya Kagera pale YMCA (Kwenye round about) ikawekwa sanamu ya mwanajeshi akiwa na silaha as if anataka kushoot.... lo Kina mama si wakatupa mikungu ya ndizi pale na kutimua mbio wakiogopa kupigwa risasi. Wengi walivunjika miguu sasa na ilijabainika kuwa wengi walitokea eneo la kishumundu sasa hadi mtwara ukisema unatokea kishumundu wanajua is the waste place kwa wachagga...... kumbe pako bomba kinoma!!

kwa taarifa wa-uru ni matajiri wakubwa, wale kina mama wanavaa kaptula za kaki ndani ya gauni na kwenye mifuko ya ile kaptula kumejaa noti mangi, wale achana nao kabisa anaweza kukununua mzima mzima kwa pesa aliyonayo. Na uru si ndo kwa mama ana pia amejitahidi sana kuendeleza kwao, si unawajuwa tena dada zako huwa ni majasiri hawaachi asili.
 
kwanini wachagga hawapatani na wapare?

tunapatana, wapare ni sehemu ya wachaga, ila kuna wakati vita ilitokea akina mangi wakuu walikuwa wanapigana kule moshi , likawa linatumika sana neno wapare yaani 'wapige' kwa hiyo wale waliookuwa waooga kusikia wapare 'wapige' wakatimua mbio na kwenda kujificha kwenye milima ya upare, baada ya vita kwisha hawakurudi tena kule kwa mangi mkuu wakabaki kule kule upareni, kwa hilo wachaga wakaona wapare kama watu waliokimbia vita yaani kama ni waoga fulani hivi; ila kwa sasa kwa kuwa wale wakuu wa zamani waliojua hayo hawapo tena tumeanza kuwa tena kitu kimoja. nawasilisha mkuu wangu.
 
Wanapatana sana tu! Ni watani wazuri sana!
Ungeniambia wamachame na wakibosho ningekuelewa

Kuna miaka ya nyuma hapa kulikuwa na vita kati ya wakibosho na wamachame...ofcoz wakibosho tulishinda ile vita...sasa hadi leo hawa ndugu zetu bado wana bifu na sisi..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom