Kitabu: Maisha, mila na desturi za Wanyamwezi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,239
12,756
Muandishi: N. D. Yongolo, 1953
Unaweza kukisoma ndani ya maktaba app. TuPm Kuungwa.

1 WATOTO
2 MICHEZO NA DESTURI ZA WATOTO
3 NDOA
4 DINI NA IMANI YA WANYAMWEZI
5 SHERIA NA HAKI KATIKA NCHI
6 UCHAWI 417 MATUMIZI YA DAWA
8 HOFU NA MIIKO YA VIFO
9 MAMBO YA POMBE 6510 MAMBO YA URITHI
11 JINSI WALIVYOANZA KUBADILI MAISHAYAO KAMA TULIVYOJARIBU 7

WATOTO HUTENGWA katika mafungu mbalimbali yanayoonyesha kuzaliwa kwao jinsi kulivyotokea. Basi, hapa nitajaribu kueleza habari hizi za watoto kwa kufuata mafungu kama hivi:

1. WATOTO
(a) Watoto wa kawaida na jinsi ya kuwapa majina: Mtoto ye yote wa kiume au wa kike azaliwapo, mzalishaji (nsimbya) wake hutoa sheria ya kutomtoa nje kabla ya kuanguka kitovu (tluila) lakini hungoja mpaka kitovu kimeanguka; asubuhi yake ndipo hutolewa nje kusudi aitwe jina kwani tangu siku aliyozaliwa alikuwa hajaitwa jina bado. Wakati wa kumtoa nje mzalishaji humchukua mtoto mikononi mwake; hapo mtoto hupewa jina na akina mama hushangilia kwa vigelegele. Kuita majina hufuata sheria mbalimbali. Huitwa jina la babu au la bibi yake akiwa msichana; pengine mzalishaji wake humwita kwa jina lake au la wazazi wake. Lakini huenda mimba ya mtoto huyo ilikuwa ya udhia, baada ya kuzaliwa mtoto huitwa jina kulifuata jambo lililotokea kabla ya kuzaliwa kwake. Hupewa majina mojawapo la haya Maganga (mimba ya dawa) Misambwa (tambiko) Kalamata (kung'ang'ania) na kadhalika. Iwapo baba au mama akifa baada ya kuzaliwa mtoto huitwa 'Mulekwa ' au 'Kalekwa ' (yaani kaachwa au aliyeachwa). Kabla ya kumtoa mtoto nje, huwapo sheria pia humo ndani (mukinyumba), yaani takataka zote zinazofagiwa humo ndani hukusanywa pamoja na kinyesi cha mtoto na kuachwa mumo humo ndani mpaka siku ya kutoka mtoto nje ndipo takataka zote hutupwa. Hufikiri kuwa ni vibaya mno takataka zikimtangulia mtoto kutoka nje; ni hatari ya kufa.

Baada ya mtoto kutolewa nje, akiwa wa kiume, baba yake humtengenezea upinde mdogo pamoja na mshale mmoja, kusudi apelekwe kukabidhiwa kwenye baraza la wazee wa mji (kwibanza) pamoja na upinde wake kuwa alama ya silaha za kiume. Mama wa mtoto hupika ugali kwa kitoweo cha jogoo akapeleka kule kwenye baraza la wazee wa mji; pamoja na ugali huo hupelekwa na njugu mawe au karanga za maganda zilizookwa. Baada ya kwisha kula chakula, wazee wale huchukua karanga moja moja na kila mmoja humvunjia mtoto sikioni pake. Kwa Kinyamwezi tunaita 'bupatula matwi'; kusudi lake ni kumwonya mtoto yule akue mwenye kusikia barabara. Hali kadhalika akiwa wa kike, hufuatwa kawaida ya mtoto wa kiume, isipokuwa yeye hupelekwa kwenye baraza la mabibi wa mji. Lakini si lazima kupata jogoo bali nyama ya aina yo yote hufaa tu, isipokuwa karanga lazima ziwepo. Mtoto hawezi kunyolewa nywele zake (ikiwa mimba yake ilianzia kwa dawa au tambiko) mpaka mama yake apike pombe ya kunyolewa nywele. Kila mara mama wa mtoto anyoapo nywele zake, lazima aachie fungu dogo la nywele kisogoni (‘kasunzu’) huwa alama ya uzazi.

(b) Kuzaa mapacha na mambo yawapasayo wazazi wao: Kuzaa watoto mapacha ni jambo la kuogofya sana kwa kila mzazi, maana hupata taabu kubwa mno na shughuli huwa nyingi kuliko kuzaa mtoto mmoja wa kawaida. Mzalishaji wa watoto hawa huitwa ‘Kambula' na wa pili ‘Kiyola.' Wazalishaji kazi yao kuu ni kuzindika ili mapacha wale wasije wakaleta madhara yo yote kwa wazazi wao au kwa wengine wa mlango huo. Mara nyingi mapacha hawakuachwa waishi wote; kwa sababu hudhaniwa kuwa mapacha ni wachawi na hawapatani kuishi pamoja lakini lazima mmoja wao ashindwe. Pengine kwa bahati waliweza kuishi wote wawili na hapo huwa taabu kwa wazazi wao—atakufa baba au mama yao. Kwa ajili ya hofu hiyo wazazi hushawishiwa wachague bahati njema au mbaya, yaani pacha mmoja auawe kabla ya kukua; bila hivyo mmoja wao wenyewe atakufa! Kwa ujinga wa wazazi wengi walichagua kumwua mtoto mmoja na kumwacha mmoja aishi.

Mambo yawapasayo wazazi wa mapacha: Haifuatwi taratibu kama ile ya watoto wa kawaida, bali siku ile ile watoto hutolewa nje na huitwa majina. Maana kuna majina ya peke yao. Mkubwa huitwa ‘Mutunda' na 'Doto' au pengine ‘Kulwa na Mpasa.' Tangu siku hiyo ya kuzaa wazazi husumbuliwa sana kwa kutukanwa na mtu ye yote wala hawakasiriki. Kwa sababu husemwa kuwa ati wasipofanywa hivyo balaa litawaandama daima; kufanywa vile hulifukuza balaa. Baba watoto hulazimika atafute kiasi cha Shs. 10/-, ada ya kuombea ngoma kwa mtemi au kwa chini ya mtemi; ngoma hiyo ni ya kuchezea mabibi wazee (kusendela), pia huhitajiwa mbuzi mmoja kuwapa wazee wale. Wazazi hukaa bila kunyoa mpaka watakapopata Shs. 40/- (kusonga mabasa); pesa hizo huhitajiwa na mtemi au chini ya mtemi ili kupata idhini ya kunyoa. Hapa natumia kutaja fedha ya kisasa lakini yakupasa kukumbuka kuwa zamani fedha hizo hazikuwapo; hivyo basi, walitumia simbi, kauri au mifugo na kadhalika badala ya fedha. Waipatapo fedha hiyo hupika pombe, na siku hiyo huchezwa ngoma ya ajabu kwani nyimbo zinazoimbwa hapo hazikuwa nzuri ila ni nyimbo za matusi matupu. Nyimbo hizo huimbwa ovyo bila kumjali mtu, hata kama yupo mkwe, basi atukanwe tu. Juu ya mambo hayo hakuna aliyeweza kuchukizwa, maana shabaha yao ni kufukuza balaa kama nilivyokwisha eleza hapo juu. Wazee wale huchagua tungi moja la kutumiwa na wao wote (limuntonga) wa mji ule, wa kiume na wa kike. Wakati huo huinywa pombe ile kwa nyimbo mbaya mno. Hudhaniwa kuwa hapo kuna uchawi mwingi kati ya wazee na hupimana ili kuonyeshana ufundi wao.

Wazazi wa watoto walivumilia masumbufu yote bila kunung'unika; pia kule kutoa fedha yao hawakujali maana walikuwa na hofu sana kwamba wasipofanya hivyo hawatakuwa na baraka yo yote katika maisha yao. Pengine wakati wa kuzaliwa watoto hao, wote wawili walitoka wamekufa; hapo mambo yote niliyoyataja juu huendeshwa sawasawa kama kwa watoto wazima au pengine baada ya kukua; mmoja wao akifa (kubomba ipasa), wazazi pia walidaiwa shughuli ya kulipa fedha ya kumzikia. Kazi ya kuzika mapacha ni kazi ya wanawake. Watoto wachanga huzikwa ukingoni mwa bwawa lisilokauka maji yake. Maana ya kuwazika humo ni makusudi kuyapoza makali yake. Lakini mapacha wakifa wakubwa huzikwa penye jaa, ambalo husawazishwa sawasawa bila kuonekana kaburi. Yasemwa kuwa mapacha hao wakizikwa mahali pengine wakati wa masika mvua huwa ngumu, yaani hupaa, na vile vile radi zitakuwa nyingi zaidi. Baada ya kuzika, huombolezwa kwa ngoma na nyimbo.

(c) Kuzaa mtoto azaliwaye kwa kutanguliza miguu ‘Kasindye’: Kuzaa ‘Kasindye' kulikuwa hakuna tofauti kubwa kwa yule aliyezaa mapacha; tofauti iliyokuwapo ni kuzidiana juu ya gharama ya kuwalipa wakuu wa nchi. Hutakiwa kiasi cha Shs. 40/- kwa mambo yote. Kama nilivyoeleza hapo juu kwa ajili ya mapacha, shughuli zizo hizo huhitajiwa kwa ‘Kasindye' pia. Lakini afapo, hazikwi kama mapacha. Huzikwa kama kawaida isipokuwa baada ya kuzika, huombolezwa kwa ngoma na nyimbo kama siku ya kuzaliwa wanapofanya 'kusendela.'

(d) Mtoto Kigego (‘sinkula'): Mtoto huyu huzaliwa kama kawaida ya watoto wengine lakini hutokea bahati mbaya kwake aanzapo kuota meno, ya kwanza huanzia kuota juu. Watoto wenye hali hii mara nyingi hawakuachwa kuishi; bali waliweza kuuawa mara ile kwa idhini ya wazazi wao. Kwa bahati sana, labda kabla ya kuonwa na watu wengine, kuwa mtoto fulani kaanza kuota meno ya juu, wazazi wenyewe kwa kuwahi kumkagua mtoto mapema, walijitahidi kupata dawa za kuzuia meno yasijitokeze. Yasemwa kuwa Wakifaulu basi ni bahati yake kuishi. ingawa mtoto alipata bahati ya kuishi, lakini atakapokuwa mtu mzima, mara nyingi hawi na sudi njema kama watu wengine. Kwa nadra sana wengine husema kuwa kigego hutoka na meno yake ya juu. Husemwa kuwa mtoto wa namna hiyo ni hatari kubwa kuliko aotaye meno baada ya kuzaliwa. Siku hizi mambo haya ya vigego yamefifia, bali kwa mapacha na 'kasindye' wengi bado wanaendelea nayo.
 
WATOTO

MICHEZO NA DESTURI ZA WATOTO

Michezo ya wavulana: Hii ilikuwa ikitegemea tabia au hali ya nchi na kazi za wazazi wao kwa mfano, kazi za mikono mbalimbali, uwindaji, uvuvi, uchungaji na nyinginezo. Juu ya kazi hizo watoto hujaribu kuwaiga wazazi wao jinsi walivyokuwa wakiwaona wakifanya. Watoto hujenga nyumba za mabua au manyasi nje ya mji, wasichana huhitajiwa na wavulana washirikiane huko kwa michezo inayohusu kuoa. Pengine wakati wa usiku wa mbalamwezi, hukusanyika pamoja katika uwanja wa mji wakajenga nyumba kwa mchanga (kwa kupiga mistari chini) badala ya zile za nje ya mji na hufanya kuiga namna ya kuoa na kuolewa, yaani kufanya arusi.

Basi, baadhi yao walio wakubwa kuliko wenzao huchaguliwa wawili, mvulana na msichana mmoja, wakawatawalisha, yaani mtemi na ‘mgoli' (mke wa mtemi). Kila raia lazima kutii amri ya mtemi, na mmoja akikaidi hufukuzwa katika mchezo na hudharauliwa na wote. Baada ya kumchagua mtemi, huchaguliwa kikosi kingine kuwa majogoo wa kuwaamsha usingizini kuwa kumekucha; wengine hupewa daraja la fisi. Kikosi cha fisi mara nyingi walichaguliwa watoto waliokuwa watundu au wale waliodharauliwa kwa ajili ya hali ya utu wao. Michezo kadha wa kadha ilichezwa usiku pamoja na ya kike. Zile nyumba zao za nje, pengine wale watoto wa kike walijishughulisha kupata unga na mboga kwa kusudi la kupika chakula kwa mabwana zao; waliweza kupata unga kwa njia ya kuokota mabaki ya vyakula katika mashamba wakatwanga wenyewe. Michezo ya namna hii pengine ilileta hasara kwa wazazi, yaani badala ya kuokota nafaka mashambani watoto waliingia nyumbani kuiba unga na chumvi, pengine wavulana waliwatega kuku wakawanasa na kuwapeleka huko katika kijiji chao. Lakini pengine iliweza kutokea hasara iliyokuwa kubwa kwa wote ya kuunguliwa mji wao iwapo kijiji cha watoto kitaungua; hivyo basi moto uliweza kuenea kwa ajili ya manyasi yaliyozunguka mji wao. Vile vile wengine waliweza kupata hasara ya kuunguza vyakula vilivyokuwa bado vimeachwa nje, kama mitama iliyokuwa imewekwa nje, yaani kabla ya kupigwa na kuhifadhiwa vizuri.

Haya sasa tuwarudie wavulana tu ili tuone michezo yao ya pekee. Kama nilivyozungumza hapo juu watoto waliweza kuwaiga wazazi wao (mpaka hivi sasa). Basi, wazazi hupenda kucheza bao, watoto nao huchuma nyanya mwitu, labda mia moja na zaidi. Hujipanga katika vikosi viwili na wengine huwa na mstari wa nyanya mwitu zilizopangwa chini, na kikosi cha pili huchukua nyanya mwitu moja ya kupiga shabaha. Yule achaguliwaye kushika nyanya ya shabaha, lazima alinge shabaha kwa uangalifu ili azipige na kuzipata nyingine kutoka katika mstari uliopangwa kule upande wa pili. Iwapo atakosea shabaha, basi hubadili vikao na wengine huchukua ile nyanya shabaha. Kikosi ambacho kitapata bahati ya kuzimaliza nyanya zilizopangwa ndio walioshinda bao moja. Waliendelea vivi hivi tu mpaka wengine wapate bahati ya kujikomboa, wasipoweza kujikomboa; basi iliwapasa kuwa na zamu ya kuzipanga nyanya zile mpaka mwisho wa mchezo huo.

Watoto wakubwa walikuwa na mashindano mara nyingi ya kupiga ndege kwa pinde. Wamwonapo ndege, kama dudumizi (‘livilivili'), hawakutaka kumnyemelea mpaka karibu bali humfukuza kwa kumrusha kila atuapo, mpaka ndege huwa amechoka sana; hapo huwahi kumwua ndege huyo; hasa hayo hutokea kwa wale waliowazidi wenzao kupiga mbio. Aliyempata ndege, hung'oa manyoya ya mabawa akawavika wenzake wote vichwani mwao, ndiyo alama ya kushindwa (‘kubasivya '). Ajivuaye nyoya lake ni yule aliyeweza kumwua ndege mwingine, yeye pia huwavika wengine walio bado hawajaua. Vile vile mchezo huu wa uwindaji mara kwa mara uliweza kuleta hasara ya kuuana wenyewe kwa wenyewe; maana watoto wakubwa kwa wakubwa walijaribiana shabaha ('ndalwe’), yaani mmoja huenda mbele ya wenzake umbali fulani na wengine hujaribu kumpiga kwa mishale, naye hurudisha kwao. Hivyo aliyepumbaa kuuepa mshale alipigwa. Na ikiwa mtoto huyo atakufa haikuwa 'nzigu' (kole) kamwe. Walisema ni shauri la manyani. Nieleze hapa kwamba 'nzigu' ni desturi ya Wanyamwezi inayotumika ikiwa mtu amekufa kwa sababu kadha wa kadha: basi, inamhusu fulani kulipa fidia. Hasa hufuatwa kama mwanamke akifariki, wakati wa kuzaa; lazima mume wake amlipe baba ya mkewe ‘nzigu.’ Neno hili litakutwa mara kwa mara katika kurasa zijazo.

Katika kuchunga mbuzi watoto wakubwa waliwasumbua sana watoto wadogo kwa kuwatuma kuwarudisha mbuzi, ili watulie mahali pamoja. Mtoto mwenye zamu ya kuwarudisha mbuzi hana ruhusa hata kuguna aambiwapo kwenda kuwarudisha mbuzi; agunapo hupigwa mijeledi mpaka atosheke. Labda wakati wa kurudi nyumbani wazazi wake watamwona jinsi alivyoenea alama za mijeledi mwili mzima, lakini wamwulizapo hawezi kutaja kama alipigwa na fulani; hujisingizia kwa namna nyingine. Na kama akitaja kuwa alipigwa na fulani huko malishoni, basi fahamu siku ya pili atakwenda kupigwa zaidi kuliko mapigo ya siku ya kwanza.

Mara nyingi katika uchungaji yalitokea matata ya kuwagombanisha watu wazima, maana labda siku fulani watoto wa upande mwingine walipigwa sana na watoto basi wazazi wao walikasirika sana wa upande huu; wakaumua ugomvi wa maana hasa. Asubuhi ya pili waliweza kumtuma mtoto mwenye mbio aende kuwatukana wazazi wa watoto waliowapiga watoto wao jana. Basi akienda wale hufahamu kuwa mtoto huyo alikuwa ametumwa na wakubwa na bila shaka huko mbugani kuna wakubwa waliomtuma kuja kuwatukana matusi hayo. Basi, kila mmoja alitoka na gongo lake kwenda kugombana nao. Wengine katika ugomvi huo waliweza kuuawa, lakini walikufa bure tu. Hukumu haikuwapo bali kuwacheka tu juu ya kufuata mashauri ya manyani na hali wao wana akili zao timamu.

Vijana wakubwa walikuwa na mchezo unaofanana na ule mchezo wa Kizungu uitwao 'cricket,' kwa Kinyamwezi huitwa 'nega.' Kabla ya kuanzisha mchezo huenda kwa mtemi kuomba ruhusa, lakini pia hupeleka 'kitano,' yaani kiasi cha Shs. 10/-. Iwapo itatokea hatari ya mtu kuuawa haliwezi kuwapo lawama la 'nzigu' yo yote. Huchonga fimbo kila mtu yake, kiisha huchonga kijiti mfano wa pia ('nambile'). Vikiwa tayari, hualikana vijana wa vijiji fulani na fulani kesho kukutana katika mpaka wa vijiji vyao. Wakifika hujipanga mistari miwili, upande huu na upande ule tayari kushambuliana. Basi, wale wenye pia huanza kuitupa juu kwa kupokezana kuipiga kabla haijaanguka chini, kwa kuivurumishia upande wa maadui zao. Na maadui wale nao huipokea wakavurumisha kuirudisha kule kule. Wakati pia inapopigwa huifuata kwa mbio sana sana, ili wapate kuipokea na kuivurumishia mbele zaidi. Kushinda kwa mchezo huu ni kuwa sehemu moja katika mbili iwezayo kuiingiza pia ndani, yaani kuuvuka mpaka wa kijiji cha wenzao—hao huwa wameshinda.

Mchezo huo ulikuwa na furaha mno kama hivi sasa sisi tunaufurahia mchezo wa mpira uitwao kwa Kizungu 'football.' Wengine kwa bahati mbaya waliweza kuwa na chongo, au kuuawa kwa kupigwa na pia; lakini hayakutokea mashauri yo yote kwa sababu ni shauri la mchezo tu. Waliweza kuingia shaurini ikiwa kabla kuanza chama chao hawakutaka idhini kwanza kwa mtemi; hapo yule aliyepiga pia kumwumiza fulani au kumwua ilimlazimu kuwa na shauri ya 'nzigu.'

Vijana na watu wazima walishirikiana katika mchezo wa kamari (kwesa nsimbi). Mchezo huu pia ulitegemea ruhusa ya mtemi, maana mara kwa mara yaliweza kutokea matata ya kuuana wao kwa wao. Kwa kuwa fedha haikuwapo wakati huo walitumia majembe na kauri, pembe za tembo na watu, yaani watumwa. Kila mchezaji alijipatia simbi nne au vipande vinne vya vigae vya vyungu vilivyofanywa kuwa duara hasa; na huleta ada au dau lake atakalotoa. Na iwapo mtu fulani aliweza kufutwa au kufilisiwa kabisa, aliweza hata kumweka mke na watoto wake (kuvega); kwa bahati mbaya labda alifutwa tena; basi alichagua kuweka njia rehani, na iwapo hata njia atafutwa, ilimlazimu kupita porini tu mpaka hapo atakapopata ukombo wa kuweza kuikomboa njia. Yaani, alipoiweka njia rehani, ndiyo kusema kuwa yeye hakuwa na ruhusa kufuata au kuipita njia yo yote katika kijiji chao. Lakini wengine baada ya muda fulani walikaidi masharti hayo wakaanza kuzitumia njia bila ukombo wo wote. Watu wa namna hii walishtakiwa mabarazani wakalazimishwa kulipa na deni likaongezeka zaidi.

Jambo hili la kamari lilileta mauaji kadha wa kadha kwa ajili ya uchungu wa mali au kupotelewa na mke na watoto. Wengi walipoona dhiki kama hizi, walijifunza uaskari ili waende kwingine kuteka nyara na kupata watumwa kuwa ukombo wa jamaa zao. Lakini wao ambao waliumua ugomvi tu, kwa kuzivunja sheria za mchezo huo, walishtakiwa barazani wakatozwa faini.

Michezo ya wasichana: Wasichana pia huwaiga akina mama wanavyofanya; vile vile michezo yao huelekea tabia za akina mama. Wasichana wengi hupenda kazi za ufinyanzi, hujaribu kufinyanga vyombo, kama vyungu. Hupenda pia kuumba watoto wa kuiga, na kadhalika, yaani watoto wa bandia, hufanya sanamu za wanyama na vinginevyo kama ng'ombe, mbuzi na wengineo. Watoto wa bandia hubebwa migongoni na hujaribu kuwabembeleza kwa kila jinsi. Lakini si mabandia ya udongo tu ndiyo yaliyokuwa yakitumiwa, mabunzi ya mihindi pia yalitumiwa badala ya udongo. Wakati wa jioni vile vile huwa na michezo yao ya pekee; kama kukimbizana na kujificha, wengine wawatafute walipojificha. Wale waliokuwa wakienda wawatafute wenzao waliojificha, huenda huku wakiimba hivi:

'Kambisule, mbisule, kali mwitina lya mung'ongo, Hanifuli kaluzi, chweee'! Na kadha wa kadha.

Huendelea hivi kwa zamu impaka wamebadili mchezo mwingine.

Maisha na kubalehe kwa watoto: Watoto wa Kinyamwezi wa siku hizi wana raha kabisa katika maisha yao kuliko wale walioishi zamani; maana siku hizi azaliwapo mtoto mara huambatana na nguo mpaka atakapojua kuwa kitu hiki kina kazi gani kwake; lakini zamani mtoto wa kila hali hakupewa nguo ya kuvaa mpaka amekuwa na makamo ya kuanza kubalehe, au msichana ameanza kuingia katika hali ya kuvunja ungo, ndipo hupewa nguo. Nadhani wengi watasema 'Je, watoto hao hawakuteswa hivyo kwa sababu ya ukosefu wa nguo tu?' Nakubali kuwa ni swali au wazo kamili, lakini kumbukeni kidogo kuwa jambo la nguo ni la kigeni kabisa katika nchi yetu. Je, wasingaliweza kuwatengenezea namna ya nguo walizozitumia wenyewe? Kama maondo au ngozi?' Mawazo yao wakati huo yalikuwa kinyume kabisa cha mawazo yetu; wao waliyafikiria maisha ya mtoto ya baadaye wakawaza kwamba mtoto avikwapo nguo mara moja yaweza kumletea balehe isiyokuwa ya kweli, yaani walifikiri eti kuwa nguo huufanya mwili uwe na joto kisha jasho huwa jingi; hivyo jasho laweza kumfanya mtoto abalehe mapema kabla ya siku zake. Tena nguo yaweza kumletea mtoto makuu na kiburi na kuwadharau wengine, hasa watoto wa kimaskini.

Baada ya kubalehe, wavulana hujikusanya pamoja kujenga nyumba, kwa Kinyamwezi huitwa 'nsalo,' na kila nyumba huwamo wavulana sita au kadiri ya masikilizano yao yalivyo. Vile vile wasichana wavunjao ungo hujengewa nyumba, Kinyamwezi huitwa 'ndalo.' Hao waliishi katika nyumba hizo mpaka muda wa kuoa au kuolewa umewadia, ndipo walipoweza kufarakana na wenzao.

Katika nyumba za wasichana, pengine binti fulani alipatwa na mimba. Aliulizwa na bibi yake au wengine aeleze ni nani aliyempa mzigo ule. Bwana aliyetajwa kwa shauri hilo huwa taabu kwake; maana alitozwa deni (lakini habari hizi nitazieleza zaidi huko mbele katika mlango wa 3). Lakini juu ya shauri la namna hii mara nyingi ilitokea bahati ya kuvuka katika ‘nzigu' anapozaliwa mtoto mzima pia mama wa mtoto kama hakufa kwa uzazi, Kinyamwezi 'ipata lya nda.'
 
Back
Top Bottom