Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,142
- 30,493
Nimekuwa na kawaida siku hizi kuwa ninaposoma Makala ya historia basi huenda kwenye kazi zangu zilizopita na kuangalia nini nimeandika.
Ndugu yangu Abdulkarim Ally ameandika makala (haipo hapa) iliyonivutia sana kuhusu siasa za Uchaggani wakati wa ukoloni.
Imesadif kuwa mimi nilitafiti na kuandika kitabu kuhusu maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama kutoka Nkuu, Machame.
Katika maisha ya Mzee Rajabu ambae alizaliwa miaka ya mwishoni 1800 na kufariki mwaka wa 1962 maisha yake yaliingiliana na watu ambao
Abdulkarim Ally kawataja katika makala yake.
Abdulkarim kamtaja Sir Charles Dundas.
Nimemweleza Charles Dundas kwa maneno haya:
Charles Dundas:
‘’Historia ya Wachagga imeandikwa kwenye upeo wa hali ya juu na Wazungu kiasi cha kumstaajabisha msomaji.
Inawezekanaje kwa Mzungu kutoka Ulaya mtu mgeni kuijua historia kwa undani wa kiasi kuweza kueleza mambo yaliyotokea miaka mingi sana iliyopita.
Mwandishi Mwingereza Charles Dundas ameandika historia ya Wachagga kwa kiwango cha kustaajabisha.
Charles Dundas ameelezea mengi ambayo mtu hupata tabu hata kuyafikiri achilia mbali kuyajua hadi awe ameyasoma.
Wachagga wana hulka pale wanapompenda mgeni basi watampa lakabu inayoendana na heshima ya kabila lao.
Charles Dundas walimwita, Wasaoye-o-Wachagga, yaani Mzee wa Kichagga.’’
Joseph Merinyo:
‘’Kaka yake jina lake Ngulelo waliochangia mama mmoja akawa Mangi wa Machame na Ngulelo alitawala hadi 1916 na ulipofika mwaka wa 1917 Waingereza wakamtoa kuwa Mangi wakampeleka uhamishoni Kismayu, Somaliland.
Taarifa nyingine zinasema alipelekwa Lamu, Kenya na kuwekwa kifungoni hapo kisiwani.
Waingereza wakamweka Joseph Merinyo kushika nafasi ile kwa muda.
Joseph Merinyo ana historia ya pekee katika siasa za Wachagga.
Joseph Merinyo alikuwa amesafiri hadi Ujerumani wakati huo akifanya kazi kwa Mjerumani ambaye ndiye aliyemchukua hadi Ulaya.
Kwa miaka ile kwa Mwafrika kufika Ulaya ilikuwa ni elimu tosha.
Joseph Merinyo akaja kuwa mkulima wa kahawa katika wakulima wa mwanzo Uchaggani kuingia katika kilimo hicho na alitajirika.
Mchagga mwingine aliyekuwa mkulima wa kahawa nyakati zile alikuwa Petro Njau.
Ngulelo alipokuwa kifungoni ndiyo akasilimu na kuwa Muislam akachagua jina la Selemani.
Ngulelo akawa Muislam wa kwanza katika ukoo wa machifu wa Kichagga.
Aliporudi kutoka kifungoni Ngulelo sasa akijulikana kama Mangi Selemani akaishi Machame mahali panaitwa Ng’ambo kwa kuwa kufika huko ilikuwa lazima uvuke bonde.
Inasemekana kuwa alipokuwa mtawala wa Machame Ngulelo hakuwa na uhusiano mzuri na Wamishionari ambao walikuwa wamedekezwa sana chini ya utawala wa Shangali.’’
Wapo wengi aliowataja Abdulkarim Ally ambao wako katika kitabu hicho hapo chini.
Hapa nimeweka machache kiasi.
Alichoandika Abdulkarim Ally:
Mr A. L. B. (Ben) Bennett DFC.( Distinguished Flying Cross) Alikuwa Rubani Wa Ndege za kivita katika Jeshi la Anga la Uingereza Royal Air force katika wakati Wa vita ya Kwanza ya Dunia .
Mwaka 1927 A. L. B. (Ben) Bennett DFC pichani, rubani wa kivita katika Vita vya Kwanza vya Dunia kutoka Uingereza alifika Kilimanjaro kama Afisa Kazi.
Kwa kushirikiana na Sir Charles Dundas aliekuwa Mkuu Wa wilaya ya Moshi walisaidia wazawa kuunda Umoja wao kwa mujibu wa kanuni za ushirika ambazo zilisisitiza haja ya kuwa na Vyama vya Ushirika vya Msingi.
1932 Vyama vya msingi 11 vilisajiliwa, ambavyo ni Kibong’oto, Uru Central, Kilema, Kibosho Central, Kibosho East, Kibosho West, Machame Central, Mamba, Tarakea, Mkuu Rombo, and Useri.
Uundaji wa Vyama hivi vya Msingi ulifungua njia ya kuanzishwa kwa Kilimanjaro Native Cooperative Union kwa mujibu wa sheria ya Ushirika.
Kahawa ilipandwa kwa mara ya kwanza huko Kilema na Wamisionari Wakatoliki mwaka 1898, na baadaye Walowezi wa Ujerumani.
Wenyeji wa Kilimanjaro hawakuruhusiwa kupanda kahawa badala yake walifanya kazi kwenye mashamba ya Settlers.
Ilikuwa hadi mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka 1918 ambapo Ujerumani ilishindwa vita hivyo ikapoteza makoloni yake ikiwa ni pamoja na Tanganyika ya wakati huo.
Mwanzilishi wa Vyama vya Wazawa wa Kilimanjaro alikuwa wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Moshi wa kwanza Mwingereza Sir Charles Cecil Farquharson Dundas (1884 - 1956) aliwaruhusu wazawa kulima kahawa kama zao la biashara.
Alieneza uzalishaji wa kahawa katika eneo hilo, na akapewa jina la Wasaoye-o-Wachagga (Mzee wa Wachagga) na Arthur Bennett akapewa Jina la heshima la Mbuya -o- Wachanga yaani Rafiki Wa Wachagga.
Kuruhusiwa kulima kahawa wenyeji walipata mbegu kutoka kwa makanisa ambako kahawa ilikuzwa.
Walipanda mazao lakini hawakuwa na ujuzi wa zao hilo.
Vita vya Kidunia vilikuwa vimesababisha uhitaji mkubwa wa kahawa huko Uropa kwa hivyo wanunuzi wengi walikuwa walowezi wa kizungu wanaoiuza nje. Wenyeji walitumia ndoo, mifuko na njia nyinginezo kubebea kahawa kwa walowezi.
Machafuko ya kijamii na kiuchumi yaliyoletwa na White Settlers na wafanyabiashara wa Asia wakati wa biashara yaliwalazimisha wakulima wadogo kuanzisha vyama vya ushirika kwa ajili ya ukombozi wa kijamii na kiuchumi.
Mwaka 1925 wenyeji waliunda Kilimanjaro Native Planters Association (K.N.P.A) huku Joseph Melinyo, kiongozi wa kwanza wa chama hicho akiwa mpinzani wa White Settlers.
Kwa hivyo, nyingi za jamii za ushiriks ziliundwa ndani ya vituo vilivyoanzishwa vya machifu.
Na baadhi yao walipewa ardhi na “Mangi” (Kiongozi wa Jadi).
Baada ya muda, zao hilo lilienea katika eneo lote za jamii hizi zilihudumiwa na KNCU.
Vijiji vingi vya miteremko ya Mlima Kilimanjaro vilikuza kahawa na kahawa ikawa zao la jadi kwa Wachaga.