Tuifute Nyerere day ili nchi ipate mabadiliko ya kweli ya kiuchumi na kisiasa

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Nyerere alifanya jambo moja tu zuri ktk taifa hili, nalo ni kuondoa ukabila na ukanda, hivyo kuwafanya watanzania kuwa wamoja. Lakini mengine yote alikosea.

Hivyo kuendelea kumuenzi mwalimu Nyerere ni sawa na kusema tuendelee kuyakumbatia mabaya yake yote. Ambayo ni:-

1. Muungano.
Lengo lilikuwa zuri lakini aina ya muungano ndiyo tatizo. Huu muungano wetu umejaa utata mtupu. Haueleweki, hauelezeki na hautekelezeki lakini tumeukumbatia tu ili kumuenzi mwalimu.

2. Katiba yetu.
Katiba yetu ya Sasa iliundwa enzi za Nyerere 1977. Ktk katiba hii Nyerere alijitwika mamlaka na madaraka yote ya nchi. Kwa katiba hii rais yuko juu ya katiba. Sasa tukiendelea kumuenzi Nyerere maana yake tuendelee na hii katiba. Kwasabb tukiibalisha hata muungano utabadilka.

3. Mwenge.
Hiki kitu hakuna mwenye majibu ya nia, malengo, na umuhimu wake. Lakini kila mwaka mabilioni ya shilingi yanateketezwa ili kuuzungusha nchi nzima. Tunamuenzi Nyerere.

4. Ujamaa.
Wajuvi wanasema watanzania hawajitumi na hawana uthubutu ktk utafutaji kwasabb ya haka kaugonjwa ka ujamaa. Watu wengi wamebweteka kwasabb wanajua watasaidiwa na majirani , ndugu na jamaa. Mifano:-

*Huandai fedha ya harusi/sendoff kwasababu unajua utachangiwa.
*Huandai fedha ya jeneza na mahala pa kuzikiwa kwasbb unajua utachangiwa.
*Watu wengi wamejiunga na vikundi vya kijamii (vikoba, kwaya, jumuiya, soka legends, makanisa, jogging, misikiti, n.k) vinavyowapotezea muda
mwingi ili tu wakipatwa na shida wasaidiwe na vikundi hivyo.

My take: Hii siku ifutwe. Kumbukumbu za Nyerere ziwekwe makumbusho ya taifa huko. Ili tuweze kutekeleza fikra mbadala.
 
Nyerere alifanya jambo moja tu zuri ktk taifa hili, nalo ni kuondoa ukabila na ukanda, hivyo kuwafanya watanzania kuwa wamoja. Lkn mengine yote alikosea.

My take: Hii siku ifutwe. Kumbukumbu za Nyerere ziwekwe makumbusho ya taifa huko. Ili tuweze kutekeleza fikra mbadala.
Huo ukabila na udini ilio ondoa ni upi kwa Tanzania ipi?.......
 
Nyerere alifanya jambo moja tu zuri ktk taifa hili, nalo ni kuondoa ukabila na ukanda, hivyo kuwafanya watanzania kuwa wamoja. Lkn mengine yote alikosea.
asaidiwe na vikundi hivyo.

My take: Hii siku ifutwe. Kumbukumbu za Nyerere ziwekwe makumbusho ya taifa huko. Ili tuweze kutekeleza fikra mbadala.
Mawazo mengine tuyaache yaelee kwa ana haki ya kupumua
 
Nyerere alifanya jambo moja tu zuri ktk taifa hili, nalo ni kuondoa ukabila na ukanda, hivyo kuwafanya watanzania kuwa
mwingi ili tu wakipatwa na shida wasaidiwe na vikundi hivyo.

My take: Hii siku ifutwe. Kumbukumbu za Nyerere ziwekwe makumbusho ya taifa huko. Ili tuweze kutekeleza fikra mbadala.
Tena ndo katufikisha hapa. Nyerere day nashauri iwe ndo siku ya kusafisha Vyoo....
 
Nyerere day ifutwe sababu marehemu alikuwa mchapakazi na hata baada ya kustaafu alirudi kijijini na kulima kwa jembe la mkono lakini sisi tunamuenzi kwa kupumzikia.

Marehemu alikuwa siyo mdini wa makabilalakini Sasa hivi udini na ukabil umerudi kwa Kasi Ila sisi tunadanganya kumuenzi.

Marehemu alikataza rushwa na viongozi kutumia nafasi yao kujilimbikizia Mali kwa Sasa kinafanyika kinyume chake.

Mengine mtajazia.
 
Watanzania Ni Wapumbavu Sana,
Nyerere Kwenda Kulima Na Jembe La Mkono Butiama Inakusaidiaje Wewe Kudeal Na kupambana Na Changamoto Alizozileta Kama Zilivyotajwa Na Mtoa Mada Hapo Juu?
 
Kuwa na Heshima...Mwl hakuwa na human resources za kutosha akianza kazi.
Miaka 25? Wazungu waliwezaje? Tzn ya wakoloni ilikuwa nzuri kuliko aliyomuachia Mwinyi.

Shida ya Mwalimu alisahau hulka ya binadamu kwamba ni Asili ya ubinafsi.

Kutumia mda, rasilimali Fedha,watu nk kufanya kile aliita ukombozi Kwa watu wengine ilikuwa ni kosa kubwa.

Angeelimisha watu saizi tungekuwa mbali sana plus ujamaa wake umezakisha watu walalamishi tuu
 
Back
Top Bottom