barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,324
- 29,586
Hivi kama jina lako ni la kisukum, hilo la kuzaliwa wakati wa baa la njaa, linaandikwa "Mayalla" au "Mayala"?? Mababu zako walikusudia liandikwaje??Wanabodi,
Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya!, hivyo mtu akiwa ni Msukuma kweli, kamwe hawezi kuwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kikanda, labda jinsia, na hili sio kosa lao, ni mfumo dume wa jamii za kiasili za kiafrika.
Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni Msukuma, na jina la Mayalla ni jina la ukoo toka kwa mababu na maana yake ni mtu aliyezaliwa wakati wa baa la njaa ( ukame, famine, drought), na sio njaa ya tumbo, au njaa ya shibe kama wengi walivyoaminishwa!.
Sisi Wasukuma sio wakabila wa ule ukabila m-baya kwa kufanya ubaguzi wa kikabila au kindugu, yaani undugunaization wa nepotism, Wasukuma ni watu poa sana, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa upendo, ndilo kabila linaloongoza kwa ukarimu, ndilo kabila linaloongoza kwa unyenyekevu, ndilo kabila linaloongoza kwa viongozi ambao they are "men of the people", yaani watu wa watu na down to earth. Hivyo ninavyoandika hapa simtetei Magufuli kwa vile ni Msukuma, namtetea kwa vile mambo mengine, wanamsingizia bure tuu huyu Msukuma wa watu!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A of the People...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...
Jee Magufuli Kweli ni Mkanda, Mdini na Mkabila?.
Hili naomba nilisilijibu ili nisiingilie uhuru wa mahakama, kwa sababu tayari kuna kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hizi ila nawaomba tuu tusimlaumu Magufuli kutokana na kauli zake.
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...
Conclusion.
Naendelea kusisitiza kwa dhati ya moyo wangu, ukanda, ukabila na udini ni sumu katika taifa letu, katika kupigana na vita hivi, ukweli usemwe, na katika kuusema ukweli huo, haki itendeke, hata kama kuna mnyonge, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.
Tanzania ni yetu sote, kila mmoja wetu, ana wajibu wa kuhakisha Tanzania inapa ustawi na maendeleo kwa kujengwa, kulindwa na kustawishwa na sisi Watanzania wenyewe, and it can be done if kila mmoja wetu, will play his part, this is my part
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni.
Wasalaam.
Paskali
Nimetoka nje ya mada kidogo kusahihishwa!