kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,315
- 12,614
Wasukuma ni wengi zaidi Tanzania, ni wachapakazi kwa asili. Wasukuma na wanyamwezi idadi Yao ni kubwa inakaribia theluthi ya Watanzania wote. Pamoja na wingi wao, uchapakazi wao mkubwa na wingi wa rasilimali zilizoko kwenye mikoa Yao, wasukuma walikuwa sio chochote Wala lolote huko nyuma kwenye awamu za kwanza hadi ya nne (4).
Mikoa ya wasukuma pamoja na kuzalisha kwa wingi dhahabu, almasi, ng'ombe, pamba, viazi vitamu, mpunga na Katanga lakini walikuwa hawana barabara za lami, shule, hospital Wala umeme kuliko mikoa ya kaskazini , nyanda za juu kusuni na masharaki. Nguvu na rasilimali zao zilikuwa zinatumika zaidi kuleta maendeleo huko kaskazini na mashariki.
Awamu ya tano (5) ilileta mapinduzi makubwa sana kwa wasukuma na wanyamwezi, imewafungua macho na kuiona nafasi Yao kwenye taifa. Rais Magufuli (Msukuma) hakupepesa macho Wala kumung'unya maneno katika kuwalipa wasukuma kile walichonyang'anywa na "wahuni" tangu wakati wa ukoloni hadi kwenye awamu ya nne. Madini, ng'ombe na maliasili kama mbao za tabora vilikuwa vikijenga barabara, reli, viwanja vya ndege, hospital, mashule na kusambaza maji na umeme kwenye Kanda nyingine.
JPM hasira hiyo iliionyesha waziwazi kwa kupeleka miradi mingi Kanda ya ziwa na kuacha kupeleka miradi kama hiyo kwenye Kanda zilizokuwa zikipendelewa na wakoloni na watawala baada ya Uhuru.
Wasukuma Sasa wamejitambua na wamegeuka kuwa zimwi kubwa kwa watawala watakaofuata baada ya JPM. Itafikia siku wasukuma watakuwa kama wakikuyu wa Kenya kwenye siasa za CCM na Tanzania, ukabila utarudi upyaaaa!
Uteuzi wa Mh. Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Mh. Makonda kuwa Katibu mwenezi, itikadi na msemaji wa CCM ni ushahidi wa jambo hili; bila kufanya hivi CCM itaanguka. Na Iko siku huko mble mgombea Urais lazima awe msukuma au aungwe mkono na wasukuma kwa mashariti magumu.
Wakoloni na Nyerere waliona mbali sana kuwatenga wasukuma kwenye nyazifa za juu.