Mtu mjinga asiye na hoja hutumia Dini na Ukabila

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,058
"Mtu mjinga, asiye na hoja wala ushawishi, hutumia dini na Ukabila. Unamwuliza, kwa nini tumchague huyu? Anasema, kwa sababu ni wa dini yetu. Kwa sababu ni wa kabila letu" - Mwalimu Nyerere.

Mwalimu Nyerere kwa vyovyote, alikuwa ni super intelligent. Sifa kubwa ya kwanza ya super intelligent person, ni kuyaona mambo kabla hayajatokea.

Nukuu ya hapo juu ya Mwalimu Nyerere (RIP), aliitoa miaka mingi iliyopita. Lakini hayo aliyoyaona wakati huo yanatokea leo!! Amesikika kiongozi mmoja wa dini akiwaomba waislam waungane kuhakikisha wanamchagua Rais Samia mwaka 2025 kwenye uchaguzi wa Rais. Kauli hii ni ya kijinga na ya uwendawazimu wa hali ya juu.

Mwaka 2025 tunachagua kiongozi mkuu wa nchi na wawakilishi wa wananchi, hatuchagui mufti mkuu wala askofu mkuu na viongozi wa misikiti na makanisa. Watu wajinga wanaotaka kura zipigwe kwa kuegemea udini, ukabila au ukanda wanatakiwa kupingwa na kila mtu anayelipenda Taifa hili. Wanaotaka Rais Samia achaguliwe kwa sababu ni muislam wanamchafua na kumharibia.

Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake alisema kuwa kuna watu walikuwa wanapenda sana kumsifia yeye, hata alipotaka kung'atuka walikuwa wanamshawishi sana asifanye hivyo. Akawakemea na kusema kuwa alichokigundua ni kwamba watu wanaokusifia sana Rais wanafanya hivyo kwa sababu ya maslahi ya familia zao, na siyo kwa sababu ya maslahi ya Taifa.

Hayo tunayaona leo, namna wateuliwa wote, na wengine huko mitaani, walivyogeuka kuwa machawa. Siyo kwa sababu ya maslahi ya nchi au kwa sababu wanampenda sana Rais, bali wanampa rushwa ya sifa Rais kwaajili ya maslahi yao na familia zao.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa nchi ili iweze kuendelea inawahitaji vijana jeuri, vijana wanaohoji na kukosoa, siyo vijana waimba sifa za viongozi.

Leo tunashuhudia tulivyo na vijana punguani, wasiohoji chochote, wasioweza kukosoa chochote; ndiyo maana nchi inasinzia, viongozi wamebweteka kwa sababu wanajua hakuna vijana wa kuwahoji na kuwakosoa hata wakikosa kutimiza wajibu wao au hata wakifanya ufisadi.

Kwa sasa ufisadi na upokeaji wa rushwa upo kwa kiwango cha juu, nahisi kwa kiasi ambacho hakijawahi kuwepo.

Kuna wafanyabiashara nimewasikia kwa masikio yangu wakilalamika namna wanavyoonekana kulazimishwa kutakiwa kuwapa pesa viongozi wa kisiasa eti kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025 kuhakikisha wanashinda uchaguzi na kuendelea na nafasi zao za sasa, na kuwa wakiendelea kwenye nafasi zao za sasa, wataendelea kulinda bishara na vitega uchumi vya hao wanaotakiwa kuwapa pesa.

Ukweli ni kwamba, nchi yetu haitabadilika na kuwa kwenye maendeleo ya kweli mpaka siku Taifa litakapokuwa na vijana jeuri, vijana wanaohoji, vijana wanaokosoa, vijana wasiokubali dhuluma, wasiokubali kurubuniwa na kugeuzwa ndondocha wa wanasiasa.

Kwa sasa, vijana ni kundi kubwa lakini linalotembea gizani, likipapasa bila kuuona mwanga wa kuelekea kwenye maendeleo ya kweli. Wengi wameamua kuwekeza kwenye ujinga na uchawa wakiamini kuwa hiyo ndiyo njia itakayowatoa kimaisha.
 
Nyerere alikuwa muongeaji ila vitendo zero ,yeye ndio mdini na mkabila namba moja kuwahi kutokea
Usiseme tu kwa sababu una uwezo wa kusema. Weka uthibitisho wa unayoyasema.

Mtu pekee anayetajwa kuwa wa alikuwa wa karibu sana na Mwalimu Nyerere alikuwa ni Rashid Kawawa. Mwenyewe wakati wote alimwita Rashid. Huyu hakuwa wa dini yake wala kabila lake.

Mtu ambaye aliaminiwa sana na Mwalimu Nyerere katika mambo magumu (tena ni kwa kauli yake), alikuwa Amir Jamal. Huyu alikuwa mhindi, si wa dini yake wala kabila lake.

Mtu ambaye aliaminiwa na Mwalimu, lakini kuoishana naye vibaya, hata kulazimika kukimbia nchi, ni Oscar Kambona, mtu wa dini yake.

Shule nyingi zilizotaifishwa (siungi mkono utaifishaji wa mali za watu au taasisi kama zimepatikana kwa njia halali) ili watoto wa dini zote na makabila yote, wasome kwa uhuru kabisa zilikuwa za Kanisa Katoliki, yaani zilizomilikiwa na dini yake na dhehebu lake.

Huo ukabila na udini wa Mwalimu ulikuwa kwenye nini?
 
Rashid kawawa kwa vile hana jinsi ,rudi shule usome kwanza usiwe kilaza kulikuwa na haja gani hata ya kuweka mfumo wa namba kweny mitihani.

Nyerere alikuwa mdini namba moja kutokea Tz hata useme nn.

Nyerere ni mdini na Mwaipopo ni mjinga tena mdini ,huyu mnyakyusa hana tabia za kiislamu kwa ujinga wake anatumwa kuongea ujinga.

Wakoloni waliweka sheria watu wabdili dini ndio wasome kweny shule zao ... Tanganyika haikuwa nchi ya kidini ila ni sheria ya wakoloni waliweka kama unabisha kaulize wazee wako unapomuona mzee makamba alibadili dini ili asome ndio maana wanawe haswa January ni mkristo ..

Kuwa makini nchi chini ya wakoloni ilikuwa ili upate elimu lazima kufuata mila zao hata bi Titi alikataa kusoma kwani ni lazima kufuata dini fulani....Misingi ya maendeleo wazungu walijenga kwa wakristo wao ndio walianza ubaguzi.

Baada ya kupata uhuru lazima wote wasome ,huyo Nyerere dini yake ndio ilimfanyw kufika pale.
 
"Mtu mjinga, asiye na hoja wala ushawishi, hutumia dini na Ukabila. Unamwuliza, kwa nini tumchague huyu? Anasema, kwa sababu ni wa dini yetu. Kwa sababu ni wa kabila letu" - Mwalimu Nyerere.

Mwalimu Nyerere kwa vyovyote, alikuwa ni super intelligent. Sifa kubwa ya kwanza ya super intelligent person, ni kuyaona mambo kabla hayajatokea.

Nukuu ya hapo juu ya Mwalimu Nyerere (RIP), aliitoa miaka mingi iliyopita. Lakini hayo aliyoyaona wakati huo yanatokea leo!! Amesikika kiongozi mmoja wa dini akiwaomba waislam waungane kuhakikisha wanamchagua Rais Samia mwaka 2025 kwenye uchaguzi wa Rais. Kauli hii ni ya kijinga na ya uwendawazimu wa hali ya juu.

Mwaka 2025 tunachagua kiongozi mkuu wa nchi na wawakilishi wa wananchi, hatuchagui mufti mkuu wala askofu mkuu na viongozi wa misikiti na makanisa. Watu wajinga wanaotaka kura zipigwe kwa kuegemea udini, ukabila au ukanda wanatakiwa kupingwa na kila mtu anayelipenda Taifa hili. Wanaotaka Rais Samia achaguliwe kwa sababu ni muislam wanamchafua na kumharibia.

Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake alisema kuwa kuna watu walikuwa wanapenda sana kumsifia yeye, hata alipotaka kung'atuka walikuwa wanamshawishi sana asifanye hivyo. Akawakemea na kusema kuwa alichokigundua ni kwamba watu wanaokusifia sana Rais wanafanya hivyo kwa sababu ya maslahi ya familia zao, na siyo kwa sababu ya maslahi ya Taifa.

Hayo tunayaona leo, namna wateuliwa wote, na wengine huko mitaani, walivyogeuka kuwa machawa. Siyo kwa sababu ya maslahi ya nchi au kwa sababu wanampenda sana Rais, bali wanampa rushwa ya sifa Rais kwaajili ya maslahi yao na familia zao.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa nchi ili iweze kuendelea inawahitaji vijana jeuri, vijana wanaohoji na kukosoa, siyo vijana waimba sifa za viongozi.

Leo tunashuhudia tulivyo na vijana punguani, wasiohoji chochote, wasioweza kukosoa chochote; ndiyo maana nchi inasinzia, viongozi wamebweteka kwa sababu wanajua hakuna vijana wa kuwahoji na kuwakosoa hata wakikosa kutimiza wajibu wao au hata wakifanya ufisadi.

Kwa sasa ufisadi na upokeaji wa rushwa upo kwa kiwango cha juu, nahisi kwa kiasi ambacho hakijawahi kuwepo.

Kuna wafanyabiashara nimewasikia kwa masikio yangu wakilalamika namna wanavyoonekana kulazimishwa kutakiwa kuwapa pesa viongozi wa kisiasa eti kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025 kuhakikisha wanashinda uchaguzi na kuendelea na nafasi zao za sasa, na kuwa wakiendelea kwenye nafasi zao za sasa, wataendelea kulinda bishara na vitega uchumi vya hao wanaotakiwa kuwapa pesa.

Ukweli ni kwamba, nchi yetu haitabadilika na kuwa kwenye maendeleo ya kweli mpaka siku Taifa litakapokuwa na vijana jeuri, vijana wanaohoji, vijana wanaokosoa, vijana wasiokubali dhuluma, wasiokubali kurubuniwa na kugeuzwa ndondocha wa wanasiasa.

Kwa sasa, vijana ni kundi kubwa lakini linalotembea gizani, likipapasa bila kuuona mwanga wa kuelekea kwenye maendeleo ya kweli. Wengi wameamua kuwekeza kwenye ujinga na uchawa wakiamini kuwa hiyo ndiyo njia itakayowatoa kimaisha.
Kama vile dini yenu ya 🌈 mlivyokuwa mnatumia hiyo kete kumchafua Samia Kwa kudai kwamba anateua Waislamu tuu.

Kama vile dini yenu ya 🌈 inavyotumia dini kupinga Kampuni za Waarabu(Waislamu) ila mnakumbatia Wazungu(Wakristo).
 
Rashid kawawa kwa vile hana jinsi ,rudi shule usome kwanza usiwe kilaza kulikuwa na haja gani hata ya kuweka mfumo wa namba kweny mitihani.

Nyerere alikuwa mdini namba moja kutokea Tz hata useme nn.

Nyerere ni mdini na Mwaipopo ni mjinga tena mdini ,huyu mnyakyusa hana tabia za kiislamu kwa ujinga wake anatumwa kuongea ujinga.

Wakoloni waliweka sheria watu wabdili dini ndio wasome kweny shule zao ... Tanganyika haikuwa nchi ya kidini ila ni sheria ya wakoloni waliweka kama unabisha kaulize wazee wako unapomuona mzee makamba alibadili dini ili asome ndio maana wanawe haswa January ni mkristo ..

Kuwa makini nchi chini ya wakoloni ilikuwa ili upate elimu lazima kufuata mila zao hata bi Titi alikataa kusoma kwani ni lazima kufuata dini fulani....Misingi ya maendeleo wazungu walijenga kwa wakristo wao ndio walianza ubaguzi.

Baada ya kupata uhuru lazima wote wasome ,huyo Nyerere dini yake ndio ilimfanyw kufika pale.
Naona unachanganya mambo hapa, na ni dhahiri hata historia huijui.
 
Back
Top Bottom