Waafrika ni wajinga au ukabila unatutafuna?

Katali

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
798
627
Usipoelewa wajibu wako katika jamii, kamwe huwezi kutoa mchango wowote wa maana.

Kulingana na Watafiti mbalimbali, kuna aina tatu za watu Duniani:
  • Wajinga,
  • Watu wenye kabila,Udini,Itikadi na yanayofanana na hayo, pamoja na
RAIA wema/Wazalendo au Wananchi.

Tafiti hizo zinaonesha 10% tu ya Waafrika hususani Tanzania ni Raia wema/Wazalendo.
waliobaki 90% ni wenye ukabila udini na ufia itikadi za vyama au wajinga.

2. Watafiti walipotumia neno "mpumbavu",au wajinga hawakulitumia kama neno la laana.
Wajinga ni watu ambao hawajali tu. Wakiwa kwenye mitihani, watadanganya. Wakiwa Serikalini wataiba.Mjinga hajali kabisa,hata akila ndizi anatupa maganda popote badala ya kuweka kwenye pipa la takataka,wengine wakiingia chooni watajisaidia nje ya Sink! Kulingana na Watafiti, jamii zingine zina wajinga zaidi kuliko wenye ukabila na raia wema.

3. Kundi linalofuata la watu ni "wenye ukabila", hawa ni watu wanaotazama kila kitu kwa mtazamo wa kabila lao. Hawa ni watu wanaokuamini ikiwa wewe ni sehemu ya makabila yao. Inaweza kuwa mbaya zaidi kuwa na ukabila kama kiongozi,maana atawatenga wengine tu kwasababu siyo wanaotokana na kabila lake.

Watafiti wanapozungumzia juu ya makabila, sio tu juu ya ukabila, pia wanaona dini na siasa kama kabila.
Asilimia kubwa ya Waafrika ni watu wa kabila, kwa sababu wao hutazama kila kitu kwa mtazamo wa makabila yao. Wanawaamini watu wa kabila lao tu.

4. Kundi la mwisho ni "wananchi".au RAIA wema. Hawa ni watu wanaopenda kufanya mambo kwa njia sahihi.
Wataheshimu sheria za taa Barabarani, hata kama hakuna anayezitazama. Wanaendesha kwa mwendo uliowekwa kisheria kwakufuata vibao vya maelekezo.

Wanaheshimu sheria, hawatafanya udanganyifu katika mitihani. Serikalini hawataiba. Wana huruma na hutoa kwa wengine ili kukuza ustawi wao.

Mara nyingi wananchi huendeleza miradi inayomnufaisha kila mtu. Watafiti waliita kundi hili raia wema au wananchi wenye mapenzi mema.

Nchi zingine zina raia wema wengi kuliko watu wenye ukabila na wajinga. Wengine wana wajinga wengi sana.

Mtu mwenye ukabila anaweza kuwa raia kupitia mafunzo na elimu iliyo bora. Na mjinga anaweza kuwa raia mwema kwa mafunzo na utekelezaji wa sheria mara kwa mara. Lakini sio aina ya utekelezaji wa sheria tunayopitia sasa.

Lakini mambo yanaharibika kwenye uchaguzi tukimchagua mjinga au mkabila kutuongoza ikiwa hajafanyiwa marekebisho.

Wewe upo katika kundi lipi?
Je, wewe ni mjinga, mkabila au raia mwema?

Tafakari kuhusu maisha yako.
 
Waafrika wengi si kwamba ni wakabila ama ni wajinga bali wanakosa ustaarabu katika mambo mengi ya msingi. Tatizo kubwa lilianzia mara baada ya kutawaliwa na wakoloni.

Wakoloni kitu kikubwa walichokifanya ni kuharibu misingi ya ustaarabu ya mtu mweusi kuendana utamaduni wa asili, na kupandikiza ustaarabu mpya wenye uchotara wa tamaduni zao zaidi na ule wa asili wa Kiafrika kwa kiasi fulani.

Ukitaka kuchunguza ustaarabu wa Mwafrika, ebu jaribu kumpima uwezo wake katika kuthamini juu ya matumizi ya huduma mbalimbali za umma na hata za binafsi, utunzaji wa rasilimali za msingi za taifa, utunzaji wa mazingira yanayomzunguka, uchaguzi wa kuweka vipaumbele kutokana uhaba wa rasilimali, uteuzi na hata kuaminiana katika kuweka rasilimali watu wenye sifa stahiki kutokana weledi, uzoefu, elimu, stadi, na hata utaalamu wao.

Kiinachokosekana ni ustaarabu. Ebu nenda bungeni ili ukaishi na jamii hiyo ya wabunge kwa muda wa mwezi mmoja tu kisha uje ulete mrejesho umejifunza nini juu ya maisha ya kila siku ya hao wawakilishi wa wananchi wanaojiita waheshimiwa
 
Wajinga tu, na hatutaki kukubali kama sisi ni wajinga na wajibu wetu wa kwanza kuuondoa ujinga.

Huwezi kuwa mwerevu, mjanja nk kama waliokuzunguka ni wajinga na primitive.
 
Back
Top Bottom