Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

wewe ndio umesema, wasukuma ni wakabila mno, sema Mungu aliwanyima akili na uwezo.
Uwezo gani ? Nyinyi wenye uwezo mnawazidi nini ha wasukuma? Biashara, Kilimo, Ufugaji ,Madini,Elimu wanafanya vizuri kama nyinyi na hata kuwazidi pia! Akili ninayoijua mimi kama ndo hiyo unaiongelea basi wewe ndo mwenye matatizo!
Nyinyi mnaokula mbege huko migombani na kudanganyana kuwa ndo mna akili peke yenu na kuwa mnajua hela na maendeleo nyinyi tu endeleeni kujifariji!
 
Laiti ingefanywa sensa ya wanaume wa kabila gani wanaongoza kwa kuoa wanawake Wachagga, ungeshangaa!. Tuwachukie Wachagga for what?. Kati ya makabila 120 ya Tanzania, ni kweli kuna makabila yana chuki na makabila mengine hivyo wana ukabila m-baya, but very fortunately Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Japo Usukumani sio miongoni mwa mikoa ya pembezoni, wahamiaji haramu wanaojipenyeza mikoa ya pembezoni, na kujifanya ni Watanzania, kule wanabaguliwa na wenyeji, ila Usukumani ndio the only safe heaven, mtu wa kabila lolote anajifanya Msukuma, sisi Wasukuma og tunamjua fulani sio Msukuma, ila bado tunamkubali na tunamuacha kugombea nafasi yoyote, udiwani, ubunge, hadi... , nenda Uchagani ukagombee chochote kama wewe sio Mchagga uone kitakachotokea
P
Unawasema wajomba kaka.
 
Uwezo gani ? Nyinyi wenye uwezo mnawazidi nini ha wasukuma? Biashara, Kilimo, Ufugaji ,Madini,Elimu wanafanya vizuri kama nyinyi na hata kuwazidi pia! Akili ninayoijua mimi kama ndo hiyo unaiongelea basi wewe ndo mwenye matatizo!
Nyinyi mnaokula mbege huko migombani na kudanganyana kuwa ndo mna akili peke yenu na kuwa mnajua hela na maendeleo nyinyi tu endeleeni kujifariji!
Mtu yeyote anayesema Wasukuma hawana akili ya maisha au hawana pesa basi hajatembea nchi hii. Anaongelea upenuni mwa nyumba ya wazazi wake.
 
Uwezo gani ? Nyinyi wenye uwezo mnawazidi nini ha wasukuma? Biashara, Kilimo, Ufugaji ,Madini,Elimu wanafanya vizuri kama nyinyi na hata kuwazidi pia! Akili ninayoijua mimi kama ndo hiyo unaiongelea basi wewe ndo mwenye matatizo!
Nyinyi mnaokula mbege huko migombani na kudanganyana kuwa ndo mna akili peke yenu na kuwa mnajua hela na maendeleo nyinyi tu endeleeni kujifariji!
akili mzee, coconut. ni kitu muhimu mno.
 
akili mzee, coconut. ni kitu muhimu mno.
Sasa wewe na Erick Shigongo au King Msukuma nani ana akili?
Njoo huku Kanda ya ziwa ndo utajua una akili au hauna akili!
Tena wewe vijana wadogo tu Kahama na Katoro hapo wanakutoa ulimi nje!
Nyinyi mnasumbuliwa sana na Ukabila na kutopenda mafanikio ya wengine!
Lakini zama zimebadilika lazima mkubali matokeo!
 
Wanabodi,

Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya!, hivyo mtu akiwa ni Msukuma kweli, kamwe hawezi kuwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kikanda, labda jinsia, na hili sio kosa lao, ni mfumo dume wa jamii za kiasili za kiafrika.

Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni Msukuma, na jina la Mayalla ni jina la ukoo toka kwa mababu na maana yake ni mtu aliyezaliwa wakati wa baa la njaa ( ukame, famine, drought), na sio njaa ya tumbo, au njaa ya shibe kama wengi walivyoaminishwa!, mimi binafsi japo ni Msukuma lakini sio mkabila, na huu ni uthibitisho wa jinsi ninavyopinga ukabila, hata kama ni ukabila wa Wasukuma na 'Wasukuma'.
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na ...

Wasukuma Sio Wakabila.
Sisi Wasukuma sio wakabila wa ule ukabila m-baya kwa kufanya ubaguzi wa kikabila au kindugu, yaani undugunaization wa nepotism, Wasukuma ni watu poa sana, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa upendo, ndilo kabila linaloongoza kwa ukarimu, ndilo kabila linaloongoza kwa unyenyekevu, ndilo kabila linaloongoza kwa viongozi ambao they are "men of the people", yaani watu wa watu na down to earth. Hivyo ninavyoandika hapa simtetei Magufuli kwa vile ni Msukuma, namtetea kwa vile mambo mengine, wanamsingizia bure tuu huyu Msukuma wa watu!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A of the People...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...

Jee Magufuli Kweli ni Mkanda, Mdini na Mkabila?.

Hili naomba nilisilijibu ili nisiingilie uhuru wa mahakama, kwa sababu tayari kuna kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hizi ila nawaomba tuu tusimlaumu Magufuli kutokana na kauli zake.
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...

Conclusion.

Naendelea kusisitiza kwa dhati ya moyo wangu, ukanda, ukabila na udini ni sumu katika taifa letu, katika kupigana na vita hivi, ukweli usemwe, na katika kuusema ukweli huo, haki itendeke, hata kama kuna mnyonge, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.

Tanzania ni yetu sote, kila mmoja wetu, ana wajibu wa kuhakisha Tanzania inapa ustawi na maendeleo kwa kujengwa, kulindwa na kustawishwa na sisi Watanzania wenyewe, and it can be done if kila mmoja wetu, will play his part, this is my part
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni.

Wasalaam.

Paskali
Kweli wasukuma siyo wakabila ila kule chato alikuwa mkabila

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom