Tufanye nini sasa juu ya haya mapenzi?

Tufanye nini sasa juu ya haya mapenzi?

Ilikuweza kudumu na mmoja na kufanya msichokane ni njia moja tu.
1 Kuaminiana
2 Kutenga mda wa kutembea kila siku mkiwa wamoja
3 Muwe marafiki(ondoa mfumo wowote wa kuhodhi au kuhodhiwa)
4 Mshirikiane katika bajeti
5 Mpange siku ya kutembelea ndugu kama mnaishi nao jirani(hii itakomaza sana uhusiano wenu)
6 Punguzeni bajeti ya matumizi
7 Pangeni siku ya kufanya usafi wa mazingira kwa pamoja
8 Mkaoge maji pamoja
9 Muwe na tabia ya kukaa na majirani zenu au hata nje ya nyumba ili muonekane
10 Kuweni mashabiki au wapenzi wa mchezo fulani(hii itajenga ukaribu wa kuongea kwa utani)
11 Muwe mnachati kwa sms WhatsApp na kwingineko. Sio mda wote voice tu
Kila la heri na ukipata ahueni kupitia ushauri wangu usisahau kunitumia buku la airtel money 0788686616 jina Adija Mwanamboka
Sawa mkuu
 
[emoji16][emoji16][emoji16]Usipo badilika dunia itakubadilisha au itakuacha nje ya mfumo wake kitu ambacho ni hatari kwa maana utakuwa upo upo tu, Cha msingi wwe fuata mfumo wa dunia ya Sasa unavyotaka, usiwe expert wa Mapenzi Bali kuwa expert wa ngono tu inatosha , Utajiepusha na maumivu ya moyo pamoja na fedheha [emoji457]
Amina
 
Mapenzi ama kitu chochote cha kudumu hujengwa na muda na uvumilivu,
Na waliowengi skuhizi hawana uvumilivu

Unataka mkutane leo kesho muwe kwa penzi zito before hamjafahamiana vizuri?!
Sahihi kabisa lugha za kimagharibi huwa zinatuzuzua hakuna kitu kinaitwa 'fall in love' au 'love at the first sight' hakuna kitu kama hicho ulimwenguni.

Kitu kilichopo ni 'growth of love' ambayo inachukua muda mpaka kukua na kupevuka hivyo hapa katikati ni jukumu la _me na _ke kumwagilia na kupalilia ili penzi lao listawi, ambapo kunakuwa na changamoto nyingi sana ila somo ni uvumilivu na uaminifu.

Kinyume nakuijua hiyo definition tutaishia kulalama ooh mapenzi hakuna siku hizi sio siku hizi hata zamani kulikuwa hakuna hayo mapenzi ya 'european version' ambayo mnayataka baada ya kupumbazwa na utandawazi, ukitaka kupata mpenzi wa kweli fuata sheria za asili ambazo wengi mnaziita za kizamani au zimepitwa na wakati ila nakuhakikishia ukizifuata na Mungu akakujalia kumpata mwenza anayezifahamu na kuzifuata mtazeeka wote pamoja, kinyume na hapo hakuna na hatakuwepo sio bar, shuleni, kazini, kanisani wala msikitini.

#Back_to_my_roots
 
Maneno mazuri
 
Jana nilikuwa na kazi kumpa ushauri jamaa yangu mmoja mtu wa system. Ana kila kitu cha kidunia ambacho wanawake wengi wanapenda ( mali)
Lakini kapigwa na kitu kizito kichwani ,analia kama mtoto mdogo.
Mapenzi ni mtihani mgumu nowdays..
Kwasasa mapenz nikubet tu wekeza kweny mirad yapesa jipend mwenyew wengin wawe nyongeza tu
 
Mapenzi ni kama dini tu, bila imani wote mnakuwa hamuuishi uhalisia wa mapenzi. Mtu umeshaumizwa mara 1000 huko then unakuja kuingia kwenye mahusiano mengine ukiwa una makovu ya mahusiano ya nyuma.

Na hata mtazamo unakuwa umebadilika, kwa hiyo inakuwa ngumu kubadili mtazamo wako baada ya kupitia maumivu.
 
Inawezekana kabisa mbona tatizo wanawake mnaumia kwa kutotambua wa kweli na waongo
 
Mapenzi ni kama dini tu, bila imani wote mnakuwa hamuuishi uhalisia wa mapenzi. Mtu umeshaumizwa mara 1000 huko then unakuja kuingia kwenye mahusiano mengine ukiwa una makovu ya mahusiano ya nyuma. Na hata mtazamo unakuwa umebadilika, kwa hiyo inakuwa ngumu kubadili mtazamo wako baada ya kupitia maumivu.
Unashauri nn
 
Mapenzi ama kitu chochote cha kudumu hujengwa na muda na uvumilivu,
Na waliowengi skuhizi hawana uvumilivu

Unataka mkutane leo kesho muwe kwa penzi zito before hamjafahamiana vizuri?!
Wengi hawaish kiuharisia tunaiga mapenz tunatak tufananishe nawatu tunao waona uvumiliv haupo hasa kwa vijan ambao jobless
 
Back
Top Bottom