Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,920
Mipango ya mezani ya Israel wanayoiita baada ya vita inawafurahisha mno wafuasi wa Israel na mayahudi kote duniani.Mipango hiyo kwa upande wa pili kama inawatia huzuni wapenda haki kote duniani.
Israel ikiendelea na mashauriano na mwenzake,Marekani wameweka mezani mikakati kadhaa ambayo wanaendelea kuifanyia kazi upi utakuwa ni bora zaidi kuanza nao.
1.Kupunguza upinzani wa raia wa nchi za kiarabu zinazoizunguka Israel itabidi watoe mamlaka kwa Palestina chini ya uongozi wa chama cha Fatah.Hili ni wazo ambalo Israel hawalipendelei hasa kwa vile wamekaribia mwisho kupoteza mipaka yote ya Palestina ya asili na ile ya baada ya 1967.Wanahisi ni kurudi nyuma ya mafanikio yao.
2.Kuweka eneo la usalama baina ya Gaza na Israel (buffer zone) ambalo litasimamiwa na vikosi vya UN.Hofu wanasema vikosi hivyo vitakuwa vikishambuliwa daima na wapalestina.
3.Gaza iachwe iendelee kuwepo lakini Saudi Arabia na UAE wawe ndio wasimamizi na wahakikishe itakuwa hakuna Hamas na wala fikra za kuyapa nguvu mafunzo yao kuhusu Israel
4.Baada ya kufanikiwa kuwaondosha Hamas Gaza jukumu litakalofuatia ni kuelekea kaskazini ya Israel na kufanya mashambulizi Lebanon ili kuwang'oa HizbuLlah.
Hayo nimeyaokoteza kutokana na mazungumzo yanayoendelea baina ya Anthony Blinken wa Marekani na Benjamin Netanyahu,waziri mkuu wa Israel.
Pale wawili hao walipotafautina juu ya kupambana na Hamas Benjamin Netanyahu,kwa kujiamini na ukali alimtamkia Blinken kuwa yeye alichukua kiapo cha kuifuta Hamas na Palestina na hakuna wa kumzuia.
Kila hatua itakayochukuliwa katika mzozo huu ni Israel na Marekani kuzama kwenye tope na kuwaingiza kwenye mzozo mwengine utakawadhoofisha kwa namna tofauti.Mimi nitaanza kujadili vipengele viwili tu,cha 3 na 4.
Saudia na UAE wanaweza wakakataa kibarua cha kulinda maslahi ya Israel Gaza dhidi ya maslahi ya waislamu,na kama wakichukua jukumu hilo hawatoweza kuendelea kuzuia fukuto lililopo kwenye raia wa nchi hizo na kunaweza kukatikisa tawala zao na hatimae kupinduliwa kabisa.
Kupambana na Hamas kumekuwa kugumu na kurefusha vita zaidi ya miezi 2 sasa.Jukumu la kupambana na Hizbulllah watalifanya wakati Hizbullah wamekuwa na nguvu sana na wanaendesha harakati zao kwa uwazi na kushirikiana na wenzao kote kuanzia Syria,Iraq,Iran na Yemen.
Jukumu hilo la kuendeleza vita Israel itakuwa wanalifanya wakati sehemu kubwa ya watu duniani wameshaerevuka na kuwa wapinzani wa sera zake.Na mwiba mkubwa itakuwa ni kuwa dhaifu kiuchumi yeye na mwenzake Marekani baada ya kujiingiza kwenye mizozo mingi bila umuhimu wowote,
Kudhoofika kijeshi na kiuchumi kwa Israel na Marekani kutawapa nguvu wapinzani kwenye nchi zote za kiarabu ambazo hazitokuwa tena na ulinzi kutoka kwa wale waliokuwa wakiwategemea.Hatimae wapinzani wataziangusha serikali za nchi zao na kuelekea kuikomboa masjid alAqsa na kuliunda kwa uhakika wake taifa la Palestina.