Tuache utani TTCL hawako serious kwenye biashara ya internet

Infopaedia

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
1,103
2,000
Hii idea ya kuhujumiwa mi naikataa kabisa. Hakuna kitu kama hicho. Ni mawazo potofu tu ambayo viongozi wazembe wamefanikiwa kuwapandikizia wananchi ili viongozi hao waendekee kukwepa wajibu wao.
Juzijuzi hapa wamefanikiwa kupandikiza tena "kijana usilalamike tu, toa suluhu". Na sisi tumeidandia hiyo slogan, viongozi wazembe officialy wamefanikiwa ku-justify uzembe wao.
Wewe kiongozi tumekuweka hapo coz umesoma utusaidie kutatua matatizo, halafu unasema 'usilalamike toa suluhu'. Hiyo ofisi tuliyokupa kwa kigezo cha ujuzi wako maana yake ni nini sasa!!! Tungemtafuta std seven leaver tumpe ofisi then wananchi wanakuja na suluhu zao, nchi inakwenda. Cha ajabu, kiongozi anasema wananchi muache kulalamika. Baada ya wiki anakuja tena anasema shirika linahujumiwa. Kasahau alituambia sisi tusilalamike, leo na yeye kaja kulalamika. Halafu analalamika wakati nyenzo zote ziko within his/her reach. Kuna awamu mpaka President alikuwa analalamika pamoja na organs zote ambazo katiba na wanachi tumemuhalalishia. Hii sio sawa kabisa.
Hakuna shirika la uma linalohujumiwa. Serikali ndiyo imeshika hatamu na inaendesha haya mashirika na ina mkono mrefu, inahujumiwaje na mwananchi kwa mfano???. Labda kichwa changu kizito kuelewa. Kitendo cha officer wa ttcl kupewa pesa na kutangaza ticket zimeisha, hiyo haina tofauti na police wa barabarani kuchukua pesa na kuacha bus bovu liendelee na safari. Tofauti ni kwamba officer wa ttcl anakwenda kuuwa shirika, polisi wa barabarani anakwenda kuuwa abiria.
Ni uzembe tu wa haya mashirika na kutokuwa na ubunifu wa kibiashara na utamaduni wa 'kama kawaida' (business as usual).
Hujuma unaonekana ni msamiati mkubwa sana ambao haiwezekani kuudhibiti. Na ukubwa wa huu msamiati ni kutokana na historia kipindi ambacho taifa moja hutafuta njia ya kunyanyuka juu ya taifa jingine. Kwa mwananchi, taifa moja kufanya hujuma dhidi ya taifa jingine, ni swala kubwa sana ambalo mwananchi hawezi kushughulika nalo. Na msamiati wa 'hujuma' ukawa unatumika kwa maswala makubwa ya uzito huo. Viongozi na wanasiasa wazembe wakagundua 'hujuma' ni msamiati mkubwa sana ambao wakijificha nyuma yake, hawataonekana. Basi wakawa wanautumia na kutuaminisha wananchi asa if hujuma ni swala la kumuachia Mungu, liko nje ya uwezo wa sisi sote. Ukichanganya na hujuma za taifa juu ya taifa, ndio kabisa tunaona ni swala zito kabisa. Viongozi waligundua watanzania ukiwaambia ni 'hujuma' huwa hawahoji, ni swala la kumuachia Mungu.
Ndio maana nakataa hakuna shirika lolote la serekali linalohujumiwa.
Mbona kwa huduma mbovu za hospitali za serikali hatusemi hospitali za serikali zinahujumiwa???. Pale kijijini kwenu kata ina zahanati moja tu, nani anahujumu ili zahanati yake binafsi ipate wateja????
Kimsingi, serikali isiyoweza kutoa huduma kwa wananchi wake kwa usahihi kamwe haitoweza kufanya biashara kwa usahihi. Na mzizi wa tatizo hilo ni mmoja, uzembe na mfumo wetu wa kufikiri. Kibaya zaidi viongozi na waliopewa madaraka wanajua jinsi ya kucheza na akili za wananchi.
Watanzania na Afica bado tuna safari ndefu ya kugeuza mitazamo na namna ya kufikiri kulingana na matatizo yanayotukabili.
 
Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,918
2,000
Mtumishi mmoja wa TTCL aliwahi kutuambia wanao iuwa hiyo kampuni ni serikali wenyewe....maana kwenye huduma ya internet wenyewe ndio wanao wauzia mitandao mingine,jiulize sasa kwa nini wao wawe slow halafu wanao uziwa wawe fasta?

-Miaka ya 2013 tulitembelea TTCl makao makuu ya mkoa flani....jamaa wana miundo mbinu ya kufa mtu kwenye upande wa telecom nadhani kwa bongo watakuwa wanaongoza,hadi server za mitandao kama tigo kwa mikoani zilikuwa ndani ya ofisi za TTCL na wachina ndio ma engineer wanaondesha kila kitu.

Hata hiyo njia ya fiber optic mitandao mingine inachukulia TTCL sasa haya madudu yanatoka wapi?

Labda wizara/waziri wa mawasiliano aje atoe ufafanuzi kuhusu upupu huu wa TTCL.
Hii kitu niliishuhudia mkoa flani nyada za juu kusini makao makuu ya TTCL, nilikuta wana server computers za kutosha zimejaa chumba kizima na zina operate 24/7 mpaka mashine za tcra za ku monitor matangazo ya redio za mkoa mzima nlzkuta makao makuu ya ttcl! Ila ajabu mtandao wao ulkua slow mbaya palepale ofisini na mnara upo hapo hapo nikawa nawaza sana, how this comes.
 
Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,918
2,000
Anachokisema jamaa ni kweli, kwa Dom hata ttcl iko na speed sasa kulko tigo na voda, tena voda hapo Dom kuna kipindi walkua hovyo mpaka wana roam kwa mtandao wa tritel, nowadays naona wame improve.
 
Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
18,322
2,000
Hii kitu niliishuhudia mkoa flani nyada za juu kusini makao makuu ya TTCL, nilikuta wana server computers za kutosha zimejaa chumba kizima na zina operate 24/7 mpaka mashine za tcra za ku monitor matangazo ya redio za mkoa mzima nlzkuta makao makuu ya ttcl! Ila ajabu mtandao wao ulkua slow mbaya palepale ofisini na mnara upo hapo hapo nikawa nawaza sana, how this comes.

Chai
 
NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
2,211
45
Usihangaike kufikiria sana kitu kikiwa na element za serikali kinakuwa bogus.Magufuli alijitajidi kutoa hili ombwe bahati mbaya mungu akampenda kuliko sisi.
 
Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
18,322
2,000
Hii idea ya kuhujumiwa mi naikataa kabisa. Hakuna kitu kama hicho. Ni mawazo potofu tu ambayo viongozi wazembe wamefanikiwa kuwapandikizia wananchi ili viongozi hao waendekee kukwepa wajibu wao.
Juzijuzi hapa wamefanikiwa kupandikiza tena "kijana usilalamike tu, toa suluhu". Na sisi tumeidandia hiyo slogan, viongozi wazembe officialy wamefanikiwa ku-justify uzembe wao.
Wewe kiongozi tumekuweka hapo coz umesoma utusaidie kutatua matatizo, halafu unasema 'usilalamike toa suluhu'. Hiyo ofisi tuliyokupa kwa kigezo cha ujuzi wako maana yake ni nini sasa!!! Tungemtafuta std seven leaver tumpe ofisi then wananchi wanakuja na suluhu zao, nchi inakwenda. Cha ajabu, kiongozi anasema wananchi muache kulalamika. Baada ya wiki anakuja tena anasema shirika linahujumiwa. Kasahau alituambia sisi tusilalamike, leo na yeye kaja kulalamika. Halafu analalamika wakati nyenzo zote ziko within his/her reach. Kuna awamu mpaka President alikuwa analalamika pamoja na organs zote ambazo katiba na wanachi tumemuhalalishia. Hii sio sawa kabisa.
Hakuna shirika la uma linalohujumiwa. Serikali ndiyo imeshika hatamu na inaendesha haya mashirika na ina mkono mrefu, inahujumiwaje na mwananchi kwa mfano???. Labda kichwa changu kizito kuelewa. Kitendo cha officer wa ttcl kupewa pesa na kutangaza ticket zimeisha, hiyo haina tofauti na police wa barabarani kuchukua pesa na kuacha bus bovu liendelee na safari. Tofauti ni kwamba officer wa ttcl anakwenda kuuwa shirika, polisi wa barabarani anakwenda kuuwa abiria.
Ni uzembe tu wa haya mashirika na kutokuwa na ubunifu wa kibiashara na utamaduni wa 'kama kawaida' (business as usual).
Hujuma unaonekana ni msamiati mkubwa sana ambao haiwezekani kuudhibiti. Na ukubwa wa huu msamiati ni kutokana na historia kipindi ambacho taifa moja hutafuta njia ya kunyanyuka juu ya taifa jingine. Kwa mwananchi, taifa moja kufanya hujuma dhidi ya taifa jingine, ni swala kubwa sana ambalo mwananchi hawezi kushughulika nalo. Na msamiati wa 'hujuma' ukawa unatumika kwa maswala makubwa ya uzito huo. Viongozi na wanasiasa wazembe wakagundua 'hujuma' ni msamiati mkubwa sana ambao wakijificha nyuma yake, hawataonekana. Basi wakawa wanautumia na kutuaminisha wananchi asa if hujuma ni swala la kumuachia Mungu, liko nje ya uwezo wa sisi sote. Ukichanganya na hujuma za taifa juu ya taifa, ndio kabisa tunaona ni swala zito kabisa. Viongozi waligundua watanzania ukiwaambia ni 'hujuma' huwa hawahoji, ni swala la kumuachia Mungu.
Ndio maana nakataa hakuna shirika lolote la serekali linalohujumiwa.
Mbona kwa huduma mbovu za hospitali za serikali hatusemi hospitali za serikali zinahujumiwa???. Pale kijijini kwenu kata ina zahanati moja tu, nani anahujumu ili zahanati yake binafsi ipate wateja????
Kimsingi, serikali isiyoweza kutoa huduma kwa wananchi wake kwa usahihi kamwe haitoweza kufanya biashara kwa usahihi. Na mzizi wa tatizo hilo ni mmoja, uzembe na mfumo wetu wa kufikiri. Kibaya zaidi viongozi na waliopewa madaraka wanajua jinsi ya kucheza na akili za wananchi.
Watanzania na Afica bado tuna safari ndefu ya kugeuza mitazamo na namna ya kufikiri kulingana na matatizo yanayotukabili.

Mzee, agiza kinywaji chochote kile nakuja kulipa
 
Aug 24, 2021
27
45
Ttcl kwa arusha ipo vizuri kama yote. Lakini kikubwa wajitahidi kwenye swala la kutupatia waya liwe bure. watuachie tu tununue router. Na kama watanihakikishia kuwa kupata waya wao ni bure mi najiunga mazima.
kingine ni kwamba, watuwekee bei nzuri ya radio transmission internet ili watanzania tuweze kununua kwa wingi.
cha mwisho wachangamke wakati ndio huu, vijana tunataka mtandao wetu wa ttcl ndio utubebe kwenye maswala ya internet.
kama nyie ndio wa kwanza kuweni wa kwanza kweli si tupo pamoja na nyie. atutaki mbabaishe.
mi naona mnaweza na mtatupa huduma nzuri. long live ttcl.
 
Sikupingi mzee baba, tumesikia kilio chako.
 
Jamaa_Mbishi

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
8,071
2,000
Kwa kweli mimi nimeinua mikono kwa internet ya TTCL. Ni internet ya hovyo sijawahi kuona.

Kuna mtu aliwahi kuandika humu kwamba mshikaji wake anaishi Tabata, anatumia mtandao wa TTCL, akilalia ubavu wa kulia anapata mtandao ila akibadilisha akalala ubavu aa kushoto ama akalala chali hakuna mtandao watu tukafikiri utani, mimi sasa nimeamini.

January mwaka huu nilipewa simu ya ofisi na line TTCL ili kurahisisha shughuli za ofisi, kila mwezi wanaweka salio kubwa tu la kufanyia mawasiliano.

Toka nimeanza kutumia hii laini hasa upande wa internet ni majanga, na mbaya zaidi ofisi zetu ziko mjini city centre lakini TTCL internet yake ni hovyo sijawahi kuona. Unaweza kukaa nusu saa au zaidi haipo kabisa, ila ikija dakika 2 inakuja kwa spidi kali sana kisha inatoweka nusu saa tena.

Muda mwingi mtandao wa TTCL haupatikani. Wakati mwingine natumia simu yangu nyingine kuweka hotpot kuunganisha na hii simu yenye laini ya TTCL ili niwe hewani niendelee kufanya mambo yangu wakati TTCL nina ma GB ya kutosha mengi sana.

TTCL wakileta ile option ya kuhamisha salio la kawaida kwenda mtandao mwingine, hela itakua ikiingia tu naihamishia mtandao mwingine, huu labda voice calls tu ila internet intakufedhehesha tu.

TTCL kuweni serious na business.
TTCL ni shirika moja la kishenzi sana, wanalitia serikali hasara kila kukicha. Hili ni shirika la kiserikali na ilibidi liwe imara zaidi kushindana na mashirika ya private lakini wapi. Wako so incompete kwenye sekta yao ya IT na huduma zao zaonyesha hivyo. Serikali nayo inabidi waanze kukata wafanyakazi wasiojuwa wafanyacho la sivyo watazidi kula hasara tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom