Tuache utani TTCL hawako serious kwenye biashara ya internet

Wala siyo hujuma ni serikali yenywewe

1. Shirika linapata ruzuku

2. Mishahara iko pale pale tena wanapewa na posho.

Km muajiriwa mkuu haoni umuhimu wa shirika, je hao wafanyakazi watakuwa na uchungu na shirika?

Mm nimeajiriwa, nitoe pesa yangu kugharamia shirika? Hapana

3. Serikali (wazee). Serikali ni watu, hao watu ndiyo walee wazee wa kizamani na ndiyo wamejazana hapo.

Utamkuta mzee anakuambia, kijana wangu nimetumiwa meseji hapa naomba uniangalizie au anakupa simu anakuambia ni
mpigie John Mwaulanya.

Ndiyo manager mkuu pale unafikiri nini kinatokea?

Wazee wanajua internet vijana wanaingia kuangalia umbeya, porno na mambo mabaya ndiyo maana hawaoni umuhimu wa PAYPAL, wanawaza utakatishaji fedha na kazi ni kulima, ujenzi n.k

Kumbe unaweza kutengeneza hela nyingi mtandaoni

Hata vijana wachache waliopo hapo hawalioni tatizo....ila kuna wazee wanajitambua na wanajua dunia inavyokwenda tatizo ni hujuma.
 
Wapo hoi bi taabani, walinichosha siku nilipokwenda kuomba technical support wote wakanikimbia ati nisubiri waliokwenda mafunzoni china waje wanisaidie maana ndiyo wenye maarifa na ujuzi
 
Wala siyo hujuma ni serikali yenywewe
1. Shirika linapata ruzuku
2. Mishahara iko pale pale tena wanapewa na posho.
Km muajiriwa mkuu haoni umuhimu wa shirika, je hao wafanyakazi watakuwa na uchungu na shirika?
Mm nimeajiriwa, nitoe pesa yangu kugharamia shirika? Hapana
3. Serikali (wazee). Serikali ni watu, hao watu ndiyo walee wazee wa kizamani na ndiyo wamejazana hapo.
Utamkuta mzee anakuambia, kijana wangu nimetumiwa meseji hapa naomba uniangalizie au anakupa simu anakuambia ni
mpigie John Mwaulanya.
Ndiyo manager mkuu pale unafikiri nini kinatokea?
Wazee wanajua internet vijana wanaingia kuangalia umbeya, porno na mambo mabaya ndiyo maana hawaoni umuhimu wa PAYPAL, wanawaza utakatishaji fedha na kazi ni kulima, ujenzi n.k
Kumbe unaweza kutengeneza hela nyingi mtandaoni

Na wakifanikiwa kuwaonyofoa wazee pale TTCL basi wawanyofoe na wazee waliopo BOT wale ndo kikwazo PAYPAL ifeli hapa nchini.
 
hao simu zao za mezani.hizi zingine wanalazimisha tu.wao waendeleo na utaratibu ule ule wa kutoa vitabu vya namba.kuna siku nilisajili laini yao.kuingia kwenye menu nataka kujiunga kifurushi cha internet wanakuwekea limit.yaani mb kadhaa utumie mchana na nyingine utumie usiku.nikaona hawajielewi hawa.nikavunja na laini yenyewe
 
Vocha za TTCL zina shida. Tunapozikwangua .... Namba zinafutuka. Kwa kifupi ni hasara. Ukipiga customer care hakuna msaada wa maana unapata. Pesa imekwenda, vocha hazijaingia kwenye simu. Mnarekebisha lini hili.... Ni swala la muda mrefu sasa.
Pole sana kwa changamoto hizo.
Tunaomba namba yako inbox na serial namba za vocha ulizokwangua vibaya ili tufuatilie na kutatua tafadhali.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza
 
Back
Top Bottom