Internet ya uhakika na bei sawa na bure ni Adsl ya TTCL

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
ttc.jpg

Usije ukadhani haya manguzo yenye nyaya zile nyembaba za ttcl zilizokuwa zinatumika zamani kwenye simu za mezani ni uchafu kwenye miji, nakujuza kwamba hizo nyaya ndizo zilikuwa zinasambaza internet miaka ile 2000 hadi 2010 enzi hizo ili upate internet inabidi uende internet cafe ambayo ilikuwa ni sehemu yenye computer zilizoungwa kwenye mtandao.. kwenye miaka ya kuanzia 2012 simu za kisasa zilianza kushika kasi tukaanza kutumia internet za minara ya simu, hali hii ilifafanya internet cafes nyingi zikafungwa, lakini licha ya haya yote bado huduma ya internet ya kwenye nyaya za zamani bado ipo mpaka leo ila ni watu wachache sana wanatumia tena kwa elf 25 tu.

Tunasikia sikia hizi kelele za internet ya fiber ambayo ni internet ya kisasa lakini ubaya ni kwamba hii fiber ipo kwenye majiji na mbaya zaidi hata kwenye hayo majiji ni yale maeneo center kati, wanasema kwa sasa wanafanya survey panapo majaliwa itasambaa mwezi wa 11 lakini ni nani asiezijua ahadi za serikali ?

Nadhani ni bora tujikite zaidi huku kwenye adsl ambayo tayari ipo kuliko kusubiri ahadi za fiber, kwa sasa uhakika ni kutumia adsl ambayo ipo tangu zamani, Uzuri wa Adsl ni kwamba imesambaa kila mikoa na wilaya nyingi.

Kama upo eneo lina nguzo za ttcl zenye zile nyaya nyembamba zilizokuwa zinatumika kwenye simu za mezani zamani basi hapo tayari una internet. Utachotakiwa kufanya ni kwenda ofisi ya ttcl, fanya jitihada ukutane na mafundi, pale mapokezi mara nyingi hawana uelewa wa mambo haya wanaweza kukwambia hio huduma haipo.

nenda na fundi wao nyumbani au ofisi unayaotaka kuwekewa, baada ya hapo utanunua kifaa cha kuchomeka ule waya kinachosambaza internet kwa elf 55, ni zoezi la muda mfupi tu, wakimaliza unalipia kifurushi cha elf 25..

Speed ni nzuri unaweza kucheki video HD 720P kwenye Youtube, netflix, n.k.

Kwa wale wazee wa kushusha muvi, series, games, mafaili

MB 1 ndani ya sekunde mbili
MB 30 ndani ya dakika
GB 1.8 ndani ya saa
Kwa siku unaweza kuchota hata gb 30

kama unahitaji spidi maradufu ya hapo inabifdi ulipie elf 50,
 
Internet inazidi kuwa muhimu sana katika maisha ya ulimwengu wa sasa lakini kwetu hapa nchini mambo yamekuwa ni tofauti. bei za internet zimepandishwa sana hali inayopelekea watu wajibane sana kwenye matumizi ya inyernet, mfano GB 1 pekee kwa sasa ni elf 2 ambayo kwa mwananchi wa hali ya kawaida hii ni gharama kubwa sana, Hali hii imetulazimu tuanze kufatilia mibadala ya uhakika yenye gharama nafuu, nami nimeamua kuleta mbinu ya uhakika ya ku enjoy internet unlimited kwa elf 25 tu ya mwezi.

Kuna habari za hapa na pale kwamba fibre inakuja lakini haya mambo ya serikali nadhani wengi sio wageni, faiba hii ajenda ni ya miaka karibia mitano lakini hadi leo ni dana dana na maneno mengi huku vitendo haviridhishi, Tunaomba hili jambo la fibre liende sawa lakini kama mjuavyo jaya mambo unaweza kuta pesa za fibre vigogo wanazitandika, wanaweza kuona faiba itapoteza kodi za wananchi wanaonunua vifurushi, n.k lolote laweza tokea

Kwa sasa uhakika ni internet ya adsl ambayo miundo mbinu yake imesambaa hata mikoani, Kama upo eneo lina mstimu wa ttcl zile nyaya nyembamba zilizokuwa zinatumika kwenye simu za mezani basi hapo ayari una internet, cable zile ukichana na kutumika kwenye simu za mezani huwa zinatumika pia kwenye internet.

UTacotakiwa kufanya ni kwenda ttcl , nashauri sana sana ufanye jitihada ukutane na wahandisi / engineers maana pale mapokezi wengi wao mambo haya yanawapiga chenga sana na hili nimeshahakikisha mara kadhaa,

baada ya hapo muende na muhandisi eneo ulilopo, kama miundombinu haijaharibika basi utanunua tu router kwa elf 55, baada ya hapo wanaku connect na kale kawaya nyumbani ama ghetto kwako unapata internet kwa wifi kutoka kwenye router .
Speed ni nusu MB hivi, ndani ya dakika waweza kushusha MB 3O na ndani ya saa GB 1.8. unavyoenda kulala unaweza kushusha hata mzigo wa GB 10. Ni speed nzuri wala si haba kustream youtube, netflix, n.k kama unahitaji spidi maradufu ya hapo inabifdi ulipie elf 50,
25 kwa mwezi si haba, ukipiga hesabu za 2000 kila siku kwa mwezi ni 60K upumbavu sana bora ulipie hio 25K
 
Vifaa vyako vina feutures szipi za ziada ukiachana na vile vya ttcl?

Ilichukua masaa mangapi kwa installation ?
Adsl ni za kizamani sana kifaa chochote cha sasa kina speed kubwa sana kushinda adsl hivyo router yoyote utakayotumia ni sawa unless upigwe router ya kizamani sana, ila kuwa safe tumia vya TTCL. Mimi wakati naweka Vifaa vya TTCL vilikuwa vimeisha, sikutaka kusubiri nikanunua vyangu mwenyewe, mpaka 5000 unapata router ya adsl mtumba wale wanaomwaga barabarani.

Haichukui muda ni hapo hapo tu wakikuwekea setting zao.
 
25 kwa mwezi si haba, ukipiga hesabu za 2000 kila siku kwa mwezi ni 60K upumbavu sana bora ulipie hio 25K
Ni kweli kabisa, mwezi ujao nitafunga hii kitu, nmechelewa sana, nilikuwa nadhani ni zile nyaya nene ndizo zenye internet ambazo zipo mjini ndizo pekee zenye internet kumbe ni hutu tunyaya twa kwenye simu, wacha nivunje kibubu nigharamike kuiweka, mwenzangu nilipita kwake jioni hii kuna jirani kaweka ana enjoy hana habari na vifurushi.
 
Adsl ni za kizamani sana kifaa chochote cha sasa kina speed kubwa sana kushinda adsl hivyo router yoyote utakayotumia ni sawa unless upigwe router ya kizamani sana, ila kuwa safe tumia vya TTCL. Mimi wakati naweka Vifaa vya TTCL vilikuwa vimeisha, sikutaka kusubiri nikanunua vyangu mwenyewe, mpaka 5000 unapata router ya adsl mtumba wale wanaomwaga barabarani.

Haichukui muda ni hapo hapo tu wakikuwekea setting zao.
Mkuu net ikoje haikati kati?
 
Internet inazidi kuwa muhimu sana katika maisha ya ulimwengu wa sasa lakini kwetu hapa nchini mambo yamekuwa ni tofauti. bei za internet zimepandishwa sana hali inayopelekea watu wajibane sana kwenye matumizi ya inyernet, mfano GB 1 pekee kwa sasa ni elf 2 ambayo kwa mwananchi wa hali ya kawaida hii ni gharama kubwa sana, Hali hii imetulazimu tuanze kufatilia mibadala ya uhakika yenye gharama nafuu, nami nimeamua kuleta mbinu ya uhakika ya ku enjoy internet unlimited kwa elf 25 tu ya mwezi.

Kuna habari za hapa na pale kwamba fibre inakuja lakini haya mambo ya serikali nadhani wengi sio wageni, faiba hii ajenda ni ya miaka karibia mitano lakini hadi leo ni dana dana na maneno mengi huku vitendo haviridhishi, Tunaomba hili jambo la fibre liende sawa lakini kama mjuavyo jaya mambo unaweza kuta pesa za fibre vigogo wanazitandika, wanaweza kuona faiba itapoteza kodi za wananchi wanaonunua vifurushi, n.k lolote laweza tokea

Kwa sasa uhakika ni internet ya adsl ambayo miundo mbinu yake imesambaa hata mikoani, Kama upo eneo lina mstimu wa ttcl zile nyaya nyembamba zilizokuwa zinatumika kwenye simu za mezani basi hapo ayari una internet, cable zile ukichana na kutumika kwenye simu za mezani huwa zinatumika pia kwenye internet.

UTacotakiwa kufanya ni kwenda ttcl , nashauri sana sana ufanye jitihada ukutane na wahandisi / engineers maana pale mapokezi wengi wao mambo haya yanawapiga chenga sana na hili nimeshahakikisha mara kadhaa,

baada ya hapo muende na muhandisi eneo ulilopo, kama miundombinu haijaharibika basi utanunua tu router kwa elf 55, baada ya hapo wanaku connect na kale kawaya nyumbani ama ghetto kwako unapata internet kwa wifi kutoka kwenye router .
Speed ni nusu MB hivi, ndani ya dakika waweza kushusha MB 3O na ndani ya saa GB 1.8. unavyoenda kulala unaweza kushusha hata mzigo wa GB 10. Ni speed nzuri wala si haba kustream youtube, netflix, n.k kama unahitaji spidi maradufu ya hapo inabifdi ulipie elf 50
Kama inastream hata 720p iko poa hio gharama nafuu
 
Ila naona TTCL bado wana fikira za kizee sna. Hadi uwe karibu na nguzo za waya!! Hayo mawaya na miguzo yanachafua miji. Why wasi tumie Vile vidude vya WIFI kama vya Tigo na Airtel. Vina connect hadi watu 10.
Havina maana yoyote mkuu
 
Chief-Mkwawa nisaidie picha ya adsl yako ya ttcl niiweke kwenye post
 
Back
Top Bottom