Tuache kupandikiza Ukanda, Ukabila na Udini

Tuache kupandikiza Ukanda, Ukabila na Udini

Naona huu ni mgongano wa maslahi!hata mwenyewe families zetu huwa hatukawii kusema' yaani brother ana roho mbaya' kisa eti hataki kukusaidia,we mwenyewe kujihangaisha hutaki. Sasa mie nikusaidieje? Kukuruka utatoboa tu kila leo kumlilia huyo serikali sijui ndio nani! Kwa serikali yako mwenyewe uone jinsi mambo zinakuwa kama rula!!
 
Wamenyamaza sababu mchakato wake umeanza kabla Magufuli hata hajafikira kuwa ataingia madarakani. Hili sio shati kusema utatungua dukani, kuna kutayarisha michoro, upembuzi yakinifu, upatikanaji na uidhinishaji wa pesa. Wabunge wetu wanajua mchakato wake ndiyo maana wamekaa kimya.
akiwa waziri mwenye dhamana ya ujenzi wa viwanjaa ndege, mwe!
 
mbona nyanda za juu kusini hatembelei? au atatembelea wakati wa kampeni?
 
Jinsi mwafrika alivyo hataweza kuacha ukabila. Taja nchi moja tu ambayo hakuna ukabila Afrika.
 
Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli tunataka kupandikiza ukabila udini na ukanda awamu hii kuliko kipindi chochote .

Serikali inapandikiza Ukanda, wananchi wanapandikiza ukabila

Dini zinapandikiza udini kwa kuleta mpaka CV za waslamu jamii forum sijui ndio zitusaidie nini.

Tumeamua kuondoa utaifa na kuwa wabaguzi lakini makosa makubwa yapo kwa rais wetu ambaye anaonekana wazi wazi kupendelea chato halafu kuna watu wanamsapoti.

Tatizo lipo tena kwa watanzania kuamini kutoendelea kwao ni kwa sababu kumesababishwa na watu wa kasikazini maana wao wameendelea yaani watu wa kasikazini kwa ujumla.

Leo hii tunashangilia uwanja wa ndege wa kiwango cha kimataifa kujengwa kwenye population ya ya watu 17,000 hii haijawai fanyika duniani kote.

Ukabila ukabila ukabila Nyerere hatukumuelewa alipokuwa akipigania utaifa kwanza.

Hivi wahaya,wachaga na wasukuma tukijifanya nchi hii ni yetu makabila mengine yakiungana nini kitatokea?

Waislamu hii nchi wakijifanya ni yao Christians wakiungana nini kitatokea

Christian hii nchi wakijifanya ni yao waislamu wakiungana nini kitatokea?

Huku mtaani tunaishi na watu wa kila aina mwingine mmakonde,Mjaluo,Waha wanyamwezi tunacheka tunakunywa tunafurahia lakini unaamka asubuhi unaanza kueneza ukabila kwa vile unatumia I'd fake jamii forum wakati ukute wewe ni kiongozi wa kitaifa au chama.

Wengine kama mimi ni wakatoriki lakini tulisoma shule za waislamu. Vijini waislamu na dini zingine wanashirikiana sana tena kwa upendo mkubwa .

Lakini mijitu misomi ndio inashinda jamii forum kupandikiza chuku na uhasama wa kidini ukanda na ukabila.

Lazima tukubali ukweli kuwa Rais anapopendelea kwao tuungane kama taifa tumshauri ajirejebishe.

Serikali inapotutangazia kuwa mkoa wa Kagera ni mkoa masikini wakati una umeme kila kijiji tena kila nyumba karibu ina luku lazima tutafakari kuwa kwanini watangaze kagera ni mkoa masikini?

Kumbukeni makabila yote ya Tanzania Tanzania sio kwenu ni waamihaji walio wengi ukiondoa wagogo ndio wazawa .

Hayo yote unayoyasema yamesababishwa na CCM pamoja na sirikali yake.

Huwezi kupanda maharagwe utegemee kuvuna mpunga. Mmeamua kuichagua CCM na hayo ndo matunda yake.
 
Angalia sana isiwe kua umeandika huu Uzi kwa ajili ya kurejea uwanja unaojengwa huko chato .Kila mradi hua unafanyika kulingana na mikakati iliyopangwa awali na haitakua sahihi kuanza kumtumia lawama MH Rais kwa kutekeleza mradi ambazo tayari ulishapangwa kufanyika hata kabla ya yeye kuwepo madarakani kwakua tu eti mda wa utekelelezaji wa huo mradi umeangukia kipindi ambacho yeye ndiyo Rais aliyepo.Hayo maswala mengine ya ukabila na using nakubaliana na wewe kua ni ya kuepuka sana kwa maslahi mapana ya taifa letu.
Embu tuambie ni awamu gani hiyo ilipanga kujenga uwanja wa KIMATAIFA wa Chato kama si awamu hii???

Hata MOBUTU SESEKO alijenga International Airport kijijini kwake. Na yeye alikuwa na mikakati kama ya Magu. Sasa limebaki gofu tu.

Tumekosa vipaumbele na ndo mana nchi hii IMEDUMAA kimaendeleo
 
viongozi wote serikali ya awamu hii ni upande wa pili na wasukuma wamejaa sasa.

swissme
Wasukuma wakipendelewa nchi hii na wakafanya ukabila itakuwa janga, waza kwa busara. Hadi sasa wateule wengi ni Iringa, Bukoba na Mara. Wachaga bado mnateuliwa uliza mashirika ya umma. Usitafute vurugu, wasikuma ni watu wanyenyekevu hata utawala huu utasikia wanateuliwa wanaostahili na siyo kupendelewa kama mlivyofanya nyuma.
 
Technically, acha uchochezi wewe, wewe ndo unapandikiza chuki, naamini nikwasababu ya chuki yako dhidi ya viongozi wetu, mbona kilimanjaro kuna uwanja wa ndege, na hapo hapo kuna mikoa ambayo iko kama kilimanjaro,but wewe hujaongea chochote, mie naamini kuna watu mna chuki binafsi na viongozi wetu, kwahiyo mnakuza mambo ili kufanikisha agenda zenu za kipuuzi. Kuna mikoa kama kilimanjaro, arusha, huduma za jamii kama maji, umeme, shule na hata viwanja vya ndege vipo tofauti na mikoa mingine kama simiyu, geita,,kigoma, ambapo baadhi ya huduma za jamii haziko improved sana ukicompare ta kilimanjaro, sasa sijua technically, unatatizo gani, au unalipwa kwa ajili ya kumchafua mh. rais. naamini kama unalipwa kwa kazi ya kumchafua kiongozi et kisa tu wa kwako ulie mtaka alishindwa, basi jiandae kupata laana kwasababu,Mh. RAIS ANAFANYA MENGI KWA AJILI YETU SISI WANYONGE, NA SI kwa ajili ya wapiga dili ulio wataka.
 
Embu tuambie ni awamu gani hiyo ilipanga kujenga uwanja wa KIMATAIFA wa Chato kama si awamu hii???

Hata MOBUTU SESEKO alijenga International Airport kijijini kwake. Na yeye alikuwa na mikakati kama ya Magu. Sasa limebaki gofu tu.

Tumekosa vipaumbele na ndo mana nchi hii IMEDUMAA kimaendeleo
Nchi itaendelea tu,tumsaidie JPM kwakua amefanya,anafanya,na atafanya mambo makubwa kwa nchi hii, fahamu kua JPM hakuanza juzi wala Jana.Hayo ya uwanja charity begins at home.
 
ndg zangu kuna mikoa wananch wake wamedumaa kiakil,mfano kuna mko wa lind,mtwara,na Ruvuma mikoa hii watu wake asilimia 99 wamedumaa kiakil na ndio mikoa inayoongoza kuuweka utawala huu unawil miongo na miongo,mikoa hii n ya mwisho kwa maendeleo ingawa mungu ameijalia neema! mikoa h mpaka sasa wanatumia umeme wa jenereta na kupelekea uchum wake kudidimia mwaka had mwaka,tambua kusin kumesha wah kutoa kiongoz mkubwa wa nch lkn hakuwaza kuboresha maisha ya makaz wa huku kusin ukifka masas utaona kama kakichaka hv lakn ndio kaliko mtoa kiongoz mkubwa wa nch hii, barabara ya lami ndo imekamilika mwaka jana ilikuwa ikiitwa mtwara korido kwa nguv za mkwere ingawa alikula lkn alikula na kipofu bila kumgusa mkono lkn pia kuna makaa ya mawe kule mangaka kama wanavyoita,kuna urenium kule namtumbo lkn kuna ges kule mtwara h yote n neema ya watu wa kusin lkn kwa kuwa wa2 hawa wamedumaa kiakil hawajui faida yake na hv vyote vnaenda kaskazn,masharik,magharib n nyanda za kat na kuwaacha wao hoi hae! chato uwanga wa ndege
acha matusi wewe Ruvuma ndio mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa mahindi hapa Tanzania na watu wa Ruvuma wana maisha mazuri kupita Dar na Arusha
 
Technically, acha uchochezi wewe, wewe ndo unapandikiza chuki, naamini nikwasababu ya chuki yako dhidi ya viongozi wetu, mbona kilimanjaro kuna uwanja wa ndege, na hapo hapo kuna mikoa ambayo iko kama kilimanjaro,but wewe hujaongea chochote, mie naamini kuna watu mna chuki binafsi na viongozi wetu, kwahiyo mnakuza mambo ili kufanikisha agenda zenu za kipuuzi. Kuna mikoa kama kilimanjaro, arusha, huduma za jamii kama maji, umeme, shule na hata viwanja vya ndege vipo tofauti na mikoa mingine kama simiyu, geita,,kigoma, ambapo baadhi ya huduma za jamii haziko improved sana ukicompare ta kilimanjaro, sasa sijua technically, unatatizo gani, au unalipwa kwa ajili ya kumchafua mh. rais. naamini kama unalipwa kwa kazi ya kumchafua kiongozi et kisa tu wa kwako ulie mtaka alishindwa, basi jiandae kupata laana kwasababu,Mh. RAIS ANAFANYA MENGI KWA AJILI YETU SISI WANYONGE, NA SI kwa ajili ya wapiga dili ulio wataka.
Ukweli usemwe hata kama unapenya kupapasa na kuuma .
 
wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya asilimia 48 ni kutoka kanda ya ziwa zilizobaki jumlisha kanda zote hapo ndipo utajua kuwa kanda ya ziwa tu ina 48% kusini kati na kwingineko wanagawana asilimia 52% ukabila tu hapo no comment.

swissme
Ndo ya akina waziri mkuu msaafu sumaye wakuu wa mikoa na wilaya ilikuwa hizo % kutoka kwake
Nimarudio tu yote haya
 
Technically, hata Chadema, wote viongozi kama akina mrema, mallya, mowe, wote wanatoka kaskazini, na chama kiko hivo, bora hata JPM anajitahidi coz mie natoka kasikazini, lakini kuna jamaa yangu tunatoka kijiji kimoja kamteuwa sasa sijui, unalalamika nini??. ila pia baadhi ya ndugu zetu waache upiga dili au wizi kwasababu kuna wengine wanatumbuliwa kwasababu wanakula rushwa, sasa JPM hataki mchezo yeye anataka uadilifu zaidi.
 
Haaaaah mkuu Mimi kwanza nikwambie ukweli kwetu ni kanda ya ziwa ingawa nimekulia DSM ...

Mambo ya kasikazini kuwa mafisadi unaweza jua wewe but Mimi sina uhakika na hilo ....

Mimi hata ukinifatilia huwa najitahidi kuwa mkweli na kuongea ukweli....

Hawezi jenga uwanja wa ndege chato yenye population ya watu 17,000 ukaanza kumtetea kwenye kichaka cha uwanja wa ndege KIA ambapo Moshi ina population ya watu Milioni 1......

Na shuguli kibao za utalii....

Lazima tuwe wakweli kujenga uwanja wa ndege kwenye population ya watu 17,000 halafu wa kimataifa na wala hakuna utaliii wowote haya ni maajabu ya dunia mengine...

Tatizo sio uwanja tatizo ni uwanja wenye uwezo wa kimataifa kujenga kwenye eneo lisilo na resources, tourism, population.......
 
Nilijua umeongea point mwishon ukaharibu yaan umehamasisha watu waachane na ukabila, udini na ukanda vzr baadae unawapandikiza chuki kwa kusema rais anapendelea kwao, mbona miaka ya nyuma enzi Msuya akiwa PM alijenga lami kwao mradi ambao haukua wa huko aliongea nani?, pili kuna miradi mikubwa ya maendeleo kwa sasa inayiendelea kujengwa sehemu mbalimbali za nchi hii je kila mkoa ukikosoa kwamba mradi fulan unapaswa kuwa mkoa wao unadhan itakuwaje?, halafu inaonekana kama watu wengi wa kaskazin ndio wanaotoka povu sana awamu hii sijui kwa nn au ubinafsi unawasumbua? Mbona mikoa ya kaskazin imeendelezwa sana toka Uhuru hakuna anayelalamika? Kwa hiyo hamtaki na mikoa mingine ipatiwe hata vimiradi kidogo?. Inasikitisha sana BUT sio mkaz wa kanda ya ziwa wala sio ccm nimeongea kama mtz anayekerwa na watu wabinafsi wanaotaka kila jambo zuri lifanyike mikoa yao tu
Nimekupa Likes 100 mkuu.
Haya majitu ni mabinafsi kupita ubinafsi. Ndio maana Mh Rais anayashughulikia ipasavyo na dawa inawaingia.
 
Haujui sera ya ccm gawanya uwatawale,ni mabingwa wa propaganda za udini,ukabila,ukanda,umaskini,Amani ,utulivu,maandamano,mikutano ya siasa na bunge live,kwenye haya mambo wanatumia kila njia kugawanya watu
Divide and rule policy
 
Back
Top Bottom