Tuache kupandikiza Ukanda, Ukabila na Udini

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli tunataka kupandikiza ukabila udini na ukanda awamu hii kuliko kipindi chochote .

Serikali inapandikiza Ukanda, wananchi wanapandikiza ukabila

Dini zinapandikiza udini kwa kuleta mpaka CV za waslamu jamii forum sijui ndio zitusaidie nini.

Tumeamua kuondoa utaifa na kuwa wabaguzi lakini makosa makubwa yapo kwa rais wetu ambaye anaonekana wazi wazi kupendelea chato halafu kuna watu wanamsapoti.

Tatizo lipo tena kwa watanzania kuamini kutoendelea kwao ni kwa sababu kumesababishwa na watu wa kasikazini maana wao wameendelea yaani watu wa kasikazini kwa ujumla.

Leo hii tunashangilia uwanja wa ndege wa kiwango cha kimataifa kujengwa kwenye population ya ya watu 17,000 hii haijawai fanyika duniani kote.

Ukabila ukabila ukabila Nyerere hatukumuelewa alipokuwa akipigania utaifa kwanza.

Hivi wahaya,wachaga na wasukuma tukijifanya nchi hii ni yetu makabila mengine yakiungana nini kitatokea?

Waislamu hii nchi wakijifanya ni yao Christians wakiungana nini kitatokea

Christian hii nchi wakijifanya ni yao waislamu wakiungana nini kitatokea?

Huku mtaani tunaishi na watu wa kila aina mwingine mmakonde,Mjaluo,Waha wanyamwezi tunacheka tunakunywa tunafurahia lakini unaamka asubuhi unaanza kueneza ukabila kwa vile unatumia I'd fake jamii forum wakati ukute wewe ni kiongozi wa kitaifa au chama.

Wengine kama mimi ni wakatoriki lakini tulisoma shule za waislamu. Vijini waislamu na dini zingine wanashirikiana sana tena kwa upendo mkubwa .

Lakini mijitu misomi ndio inashinda jamii forum kupandikiza chuku na uhasama wa kidini ukanda na ukabila.

Lazima tukubali ukweli kuwa Rais anapopendelea kwao tuungane kama taifa tumshauri ajirejebishe.

Serikali inapotutangazia kuwa mkoa wa Kagera ni mkoa masikini wakati una umeme kila kijiji tena kila nyumba karibu ina luku lazima tutafakari kuwa kwanini watangaze kagera ni mkoa masikini?

Kumbukeni makabila yote ya Tanzania Tanzania sio kwenu ni waamihaji walio wengi ukiondoa wagogo ndio wazawa .

mimi nadhani tanzania hakuna ukabila ila wapo wanaojifanya kupinga ukabila kumbe wao ndio wanajenga hisia za chuki na fitina katika vichwa vya watu.

akitaka kupinga jambo fulani anaweka ukabila, anaweka udini ndio hoja yake ibebwe na hayo lakini matokeo yake anajenga hisia za ukabila vichwani mwa watu.

mfano kuna watu vi viwembe kupindukia, msichana hakatizi mbele yake, ametembea na watu idadi haihesabiki lakini watu wakiingia katika stori za kawaida unamkuta mtu huyu anasema kabila fulani ni malaya? Sasa unajiuliza hivi huyu anayoyaongea anayajua? je yeye anajitambua? je ana ushahdi kuwa lile kabila analolisema ameona tabia za kipekee katika hoja hiyo? kwa utafiti wangu nimebaini hakuna anayejenga hoja hizi kwa ushahidi bali kuna misemo watu wamezoea kusema ndio wanabeba na unakuta analolisema mtu kutuhumu wengine yeye kakubuhu.

wito wangu tutoke kwenye hadithi tunazorithishana tutafute ukweli. tusikimbilie kujenga hoja ya kaskazini wamependelewa wakati wewe huoni mwenyewe unaogopa hata kujenga nyumbani kwenu ukiogopa kurogwa sasa waliofanya juhudi na kwa ku play their role na serikali ikawaunga mkono tusifanye unafiki kuwafitini bali tuige.

yawezekana kweli huko nyuma walikuwepo viongozi wengi kutoka huko wakapeleka miradi mingi huko lakini hizo ndizo zilikuwa tawala za huko nyuma kila anayechaguliwa anakimbilia kufanya kwao.

kwa sasa tutazame tunakwendaje lakini sio kuvurugana kwa kusakiziana hoja za udini na ukabila.

hakuna jamii inayoweza kuvumilia kupakwa matope mda wote kila anayeibuka akitokea jamii isiyoendelea anadhani hojua ni kupaka matope jamii zilizombele. Zipo sababu nyingi za kihistoria, kijiografia na kitamaduni zinazoweza kusababisha jamii zisiwe sawa na anayetaka kutafuta maendeleo kwa jamii yake azitazame hizo na aangalie ni wapi pa kurekebisha.
 
wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya asilimia 48 ni kutoka kanda ya ziwa zilizobaki jumlisha kanda zote hapo ndipo utajua kuwa kanda ya ziwa tu ina 48% kusini kati na kwingineko wanagawana asilimia 52% ukabila tu hapo no comment.

swissme
Kwenye vyeo vyote vikubwa vyenye maamuzi ukimtoa JPM mwenyewe simuoni yeyote mwenye asili ya usukuma akiwapo. Mfano halisi ni kutokuwapo waziri yeyote (siyo naibu waziri) msukuma kwenye baraza la JPM. Kwa hali hiyo Bado ni ngumu kumweka JPM kwenye lawama za ubaguzi.
 
Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli tunataka kupandikiza ukabila udini na ukanda awamu hii kuliko kipindi chochote .

Serikali inapandikiza Ukanda, wananchi wanapandikiza ukabila

Dini zinapandikiza udini kwa kuleta mpaka CV za waslamu jamii forum sijui ndio zitusaidie nini.

Tumeamua kuondoa utaifa na kuwa wabaguzi lakini makosa makubwa yapo kwa rais wetu ambaye anaonekana wazi wazi kupendelea chato halafu kuna watu wanamsapoti.

Tatizo lipo tena kwa watanzania kuamini kutoendelea kwao ni kwa sababu kumesababishwa na watu wa kasikazini maana wao wameendelea yaani watu wa kasikazini kwa ujumla.

Leo hii tunashangilia uwanja wa ndege wa kiwango cha kimataifa kujengwa kwenye population ya ya watu 17,000 hii haijawai fanyika duniani kote.

Ukabila ukabila ukabila Nyerere hatukumuelewa alipokuwa akipigania utaifa kwanza.

Hivi wahaya,wachaga na wasukuma tukijifanya nchi hii ni yetu makabila mengine yakiungana nini kitatokea?

Waislamu hii nchi wakijifanya ni yao Christians wakiungana nini kitatokea

Christian hii nchi wakijifanya ni yao waislamu wakiungana nini kitatokea?

Huku mtaani tunaishi na watu wa kila aina mwingine mmakonde,Mjaluo,Waha wanyamwezi tunacheka tunakunywa tunafurahia lakini unaamka asubuhi unaanza kueneza ukabila kwa vile unatumia I'd fake jamii forum wakati ukute wewe ni kiongozi wa kitaifa au chama.

Wengine kama mimi ni wakatoriki lakini tulisoma shule za waislamu. Vijini waislamu na dini zingine wanashirikiana sana tena kwa upendo mkubwa .

Lakini mijitu misomi ndio inashinda jamii forum kupandikiza chuku na uhasama wa kidini ukanda na ukabila.

Lazima tukubali ukweli kuwa Rais anapopendelea kwao tuungane kama taifa tumshauri ajirejebishe.

Serikali inapotutangazia kuwa mkoa wa Kagera ni mkoa masikini wakati una umeme kila kijiji tena kila nyumba karibu ina luku lazima tutafakari kuwa kwanini watangaze kagera ni mkoa masikini?

Kumbukeni makabila yote ya Tanzania Tanzania sio kwenu ni waamihaji walio wengi ukiondoa wagogo ndio wazawa .
Kwa hali ilivyo sasa hapa kuna harufu ya ukabila
 
Kanda ya ziwa ni wengi humu na pia wale wa imani yetu wanaongezeka.. Tuwe wapole hata mji mkuu wa Italy ulikuwepo kabla.
 
Kwenye vyeo vyote vikubwa vyenye maamuzi ukimtoa JPM mwenyewe simuoni yeyote mwenye asili ya usukuma akiwapo. Mfano halisi ni kutokuwapo waziri yeyote (siyo naibu waziri) msukuma kwenye baraza la JPM. Kwa hali hiyo Bado ni ngumu kumweka JPM kwenye lawama za ubaguzi.
Noted well
 
Mkuu hayo ndio tunayakataa ukija njoo na data wasukuma ni wangapi kwenye teuzi lakini kuendelea kuongea tu ni kupalilia chuki isiyo na maana
samahani hapo kwa wagogo umenidanganya wazawa wa Tanganyika ni wahadzabe
 
kama hali ndo hii na mm ngoja nikiingia nitajaza kabila langu lile "kabila teule hapa tz linalofananishwa na jews"
 
Wamenyamaza sababu mchakato wake umeanza kabla Magufuli hata hajafikira kuwa ataingia madarakani. Hili sio shati kusema utatungua dukani, kuna kutayarisha michoro, upembuzi yakinifu, upatikanaji na uidhinishaji wa pesa. Wabunge wetu wanajua mchakato wake ndiyo maana wamekaa kimya.
Itafahamika.
 
Mkuu hayo ndio tunayakataa ukija njoo na data wasukuma ni wangapi kwenye teuzi lakini kuendelea kuongea tu ni kupalilia chuki isiyo na maana
Mheshimiwa Technically umeandika mada ambayo pia inaweza sababisha kuchochea moto zaidi ya kutatua tatizo. Leo mchana nikiwa na jamaa zangu fulani walianzisha hiyo mada kuhusu uteuzi kwamba ikiwa wewe ukifika pale Chalinze kisha ukakata kulia kwenda huko Arusha basi wewe kuteuliwa sahau......Nikawajibu vizuri tu boss wa NIDA anaitwa Massawe au hili jina anatumia jina la ujombani? Maana kwa hiyo hoja ya uteuzi tayari yupo Masawe ambaye jina lake lipo wazi kabisa tena ni rafiki yake mkubwa tu.
Kuna hili swala mara hateui waislamu, hivi mnajua katibu mkuu ofisi ya raisi utumishi ni rafiki yake mkubwa tu na ni Alhaji Musa Iyombe.Tungesema aache kuteua watu ambao anawafahamu tu hapo tungekuwa tumejifanyia haki.
Kuhusu uwanja wa ndege, mimi nimeshawahi kutumia uwanja wa Mchauru ambao unamilikiwa na Geita Gold Mine (GGM) Geita kama mkoa hakuna uwanja wa ndege wa serekali kwa hiyo tungejadili kwa nini Chato na sio Geita mjini? Lakini tukihoji hilo tuhoji pia kwa nini KIA na sio Arusha mjini au Moshi mjini? Uwanja wa ndege mkoa wa Geita ni muhimu sana kwa sababu mkoa wa Geita kwanza unawachimbaji wadogowadogo ambao ni wengi na wanahitaji sana kutumia usafiri wa ndege. Usafiri wa barabara unakizingiti cha kutumia feri ya kigongo ambayo unaweza kuta haipo hata masaa matatu.
 
Mimi si msukuma wala mchaga,ila kuna haja ya kujenga Chato International Airport????
Why wasingeendeleza kiwanja cha Dodoma au wangejenga Morogoro ili watalii wawe wanatua pale na Kupelekwa MIKUMI????
Mkuu kiwanja cha Dodoma ndio kinamaliziwa kupanuliwa hilo hulijui? Pia morogoro uwanja ungeshajengwa muda mrefu shida pale kiwanja hakijengwi kwa sababu za kiusalama maana ndege nyingi za jeshi hufanyia mazoez pale, pia mm sio msukuma wala si mwenyeji wa kanda ya ziwa wala si mwana ccm ila ninachokiona na uroho ama wivu tu wa baadh ya watz wanaotaka maendeleo maeneo yao tu huku mikoa mingine ikiwa na hali mbaya wakati watz wote wanalipa kodi
 
Achana na ile airport ya Chako ni Chako,jamaa walikua na Kiwanja huko Veyula na watu walishawalipa fidia miaka na miaka.
Kama Moro ni usalama na Mikumi je?
 
Mkuu kiwanja cha Dodoma ndio kinamaliziwa kupanuliwa hilo hulijui? Pia morogoro uwanja ungeshajengwa muda mrefu shida pale kiwanja hakijengwi kwa sababu za kiusalama maana ndege nyingi za jeshi hufanyia mazoez pale, pia mm sio msukuma wala si mwenyeji wa kanda ya ziwa wala si mwana ccm ila ninachokiona na uroho ama wivu tu wa baadh ya watz wanaotaka maendeleo maeneo yao tu huku mikoa mingine ikiwa na hali mbaya wakati watz wote wanalipa kodi
Hakuna alokataa kama hawalipi kodi,kuna miundombinu huwekwa kwa sababu ya fursa za kiuchumi za eneo husika ndo maana unawekwa uwekezaji wa nguvu ili tu kuhakikisha faida itapatikana,ndo maana wanaokosoa huo mradi sio kwamba CHATO haistahili ila je kiuchumi unalipa?isije ikawa kama mighorofa ya NSSF ambayo naadae inakua majumba ya ndege na popo.Hayo maeneo nilokutajia like Dodoma yana tija,kama wanapeleka makao makuu waache na upanuz wa hii airport ndogo,kwanza ipo mjini sanaaa,pili ni kero hata kimazingira (sound polusheni).Why wasingejenga veyula?
Ndio maana utaona DSM wanahangaika na Fly overs maana mji wenye pirika za kibiashara na muhim kiuchumi,tena walipaswa hata kuweka uwanja mwingine hata Kibaha,
 
Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli tunataka kupandikiza ukabila udini na ukanda awamu hii kuliko kipindi chochote .

Serikali inapandikiza Ukanda, wananchi wanapandikiza ukabila

Dini zinapandikiza udini kwa kuleta mpaka CV za waslamu jamii forum sijui ndio zitusaidie nini.

Tumeamua kuondoa utaifa na kuwa wabaguzi lakini makosa makubwa yapo kwa rais wetu ambaye anaonekana wazi wazi kupendelea chato halafu kuna watu wanamsapoti.

Tatizo lipo tena kwa watanzania kuamini kutoendelea kwao ni kwa sababu kumesababishwa na watu wa kasikazini maana wao wameendelea yaani watu wa kasikazini kwa ujumla.

Leo hii tunashangilia uwanja wa ndege wa kiwango cha kimataifa kujengwa kwenye population ya ya watu 17,000 hii haijawai fanyika duniani kote.

Ukabila ukabila ukabila Nyerere hatukumuelewa alipokuwa akipigania utaifa kwanza.

Hivi wahaya,wachaga na wasukuma tukijifanya nchi hii ni yetu makabila mengine yakiungana nini kitatokea?

Waislamu hii nchi wakijifanya ni yao Christians wakiungana nini kitatokea

Christian hii nchi wakijifanya ni yao waislamu wakiungana nini kitatokea?

Huku mtaani tunaishi na watu wa kila aina mwingine mmakonde,Mjaluo,Waha wanyamwezi tunacheka tunakunywa tunafurahia lakini unaamka asubuhi unaanza kueneza ukabila kwa vile unatumia I'd fake jamii forum wakati ukute wewe ni kiongozi wa kitaifa au chama.

Wengine kama mimi ni wakatoriki lakini tulisoma shule za waislamu. Vijini waislamu na dini zingine wanashirikiana sana tena kwa upendo mkubwa .

Lakini mijitu misomi ndio inashinda jamii forum kupandikiza chuku na uhasama wa kidini ukanda na ukabila.

Lazima tukubali ukweli kuwa Rais anapopendelea kwao tuungane kama taifa tumshauri ajirejebishe.

Serikali inapotutangazia kuwa mkoa wa Kagera ni mkoa masikini wakati una umeme kila kijiji tena kila nyumba karibu ina luku lazima tutafakari kuwa kwanini watangaze kagera ni mkoa masikini?

Kumbukeni makabila yote ya Tanzania Tanzania sio kwenu ni waamihaji walio wengi ukiondoa wagogo ndio wazawa .

CCM na SERIKALI yake inachezea amani ya nchi hii.

Wazungu wanasema ''seeing is believind''

Ngoja tuuwane kama wenzetu warundi na wakrnya ndo tutaheshimiana
 
Back
Top Bottom