Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 21,854
- 26,094
USHAURI WANAOPUNGUZWA WAINGIZWE KWENYE MOTOR VEHICLE INSPECTOR WAPIGWE MSASA KWANZA!
Hahaha..Wahuni wale walikua hawapunguzi ajali Wala nini. Ajali ya gari la wanafunzi Mtwara isingetokea Kama Hawa Wala rushwa wangekua wanakagua magari.
Nimpongeze IGP kwa hatua hii nzuri hasa kumuondoa trafik mmoja wa kike pale Ruvu jirani kabisa na hoteli ya JKT.
Mpangieni Yule mla rushwa kulinda nyumba ya DC wa kike awe anasikiliza miguno usiku.
Aliringa utafikiri daraja la Ruvu kalijenga babake.
Nipe sababu kwanini pale chalinze mpaka msoga paliponyooka pana mstari usioruhusu kuovertake... Bepari2020 ana hoja; tusimbeze. Tuwe wakweli, eneo linaloenda kuongezeka ajali ni wrong overtaking. Uwepo wa trafiki uliwafanya madereva waogope ku-overtake ovyo ovyo. Dereva haoni mbele kuna nini ana-overtake tu halafu analazimisha kuchomekea; wale wa mabasi mnawajua. Ukimkuta anayechomekewa naye ni m`bishi hiyo tayari ni ajali.
Ni kweli trafiki wana kero zao, ila their presence ina msaada mkubwa kuwafanya madereva wa ovyo ovyo kutokuvunja sheria ovyo hususan zile zenye serious impact.
Hatukatai ndugu kuwa ni kweli kuwa kuna baadhi ya maaskari wamewageuza wenye magari kuwa ndio maduka yao.....lakini hiyo hairamishi uwepo wa wengine WANAOZINGATIA weledi wa kazi....Kuna siku nipo na Noah,nikatolewa upepo buku tano bila sababu za msingi,sikua na kosa...walikuwa wengi mno barabarani
Mbeya wanafanya hivyo, asubuhi kusindikiza magari yanayoenda mikoani kutoka jijini Mbeya.Trafiki hawapunguzi ajari ila wanasababisha usumbufu tu sisi hatusemi watoke kabisa bali wapungue ama wasindikize magari.
Sidhani Kama wanetolewa woteHatukatai ndugu kuwa ni kweli kuwa kuna baadhi ya maaskari wamewageuza wenye magari kuwa ndio maduka yao.....lakini hiyo hairamishi uwepo wa wengine WANAOZINGATIA weledi wa kazi....
Tusuburi ajali za barabarani ziongezeke
Kinyota ni matrafiki maofisa , jina hili wamepewa na Makonda wa daladalaHahahahahaha kuna mmoja anaitwa kinyota Askari flani hivi yupo hapo Mlandiz saa ingine pale pale Ruvu Darajani
Hivi kwa mfano kukutwa na leseni ya udereva iliyoisha muda wake (kwa wiki kadhaa) ni kosa la kuandikiwa faini?Kuna yeyote humu amewahi kukamatwa na trafiki na akalipishwa faini bila kosa lolote? Be honest; yaliyo moyoni kwako wayajua mwenyewe.
Hizo rushwa za elfu 5 au 10 sio sisi wenyewe tunawabembeleza kukwepa kulipa elfu 30? Tunawalaumu kwa lipi kuhusu rushwa? Unless tunalaumu mapato ya serikali kupotea which I don't think kama ndicho kinacholalamikwa na madereva.
... na mimi ndio huwa najiuliza hilo swali; kwamba leseni iki-expire automatically na skills za udereva zina-expire? Kimsingi hilo lilitakiwa liwe kosa la onyo tu ila trafiki wa nchi hii hawakuachi aisee; kwao ni bonge la bingo.Hivi kwa mfano kukutwa na leseni ya udereva iliyoisha muda wake (kwa wiki kadhaa) ni kosa la kuandikiwa faini?
... jukumu la kusimamia sheria ya usalama barabarani ni la polisi/trafiki; sio kazi yao kuweka alama zinazotafsiri sheria. Kuweka alama ni kazi ya TANROADS.Nipe sababu kwanini pale chalinze mpaka msoga paliponyooka pana mstari usioruhusu kuovertake
Gazeti la Raia Mwema limeripoti kwamba tayari panga limekwisha tembea, huku MCHEZO WA UPATU waliokuwa wanacheza Trafiki hao kila siku ukibaki njia panda , kwa vile wengi wamepangiwa kazi zingine ambazo haziingizi chochote zaidi ya Mshahara , TAARIFA ZINADOKEZA KWAMBA TRAFIKI WENGINE WALIKUWA NA MCHEZO WA UPATU WA KULIPA HADI SH LAKI MOJA KWA SIKU , ambapo inaelezwa kwamba chanzo cha hela hizo ilikuwa ni Rushwa za barabarani .
Kwa mujibu wa gazeti hilo , Trafiki wengi wanamlaumu Kinana kwa kuibua jambo hilo .
Endelea kubaki JF kwa taarifa zaidi.
PIA SOMA: Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura
... jadili hoja objectively acha kujadili kwa hisia.Weye utakuwa trafenga
Aroo afande........ jadili hoja objectively acha kujadili kwa hisia.
... mkuu uliamua tu kuwapa pesa kwa utashi wako; kama kweli hukuwa na kosa ulitakiwa kukataa. Kuna siku natokea Mbeya nimevuka Iringa mahali fulani patamu sana "kuokolea muda" pamenyooka sana karibu kuitafuta Ilula.Kuna siku nipo na Noah,nikatolewa upepo buku tano bila sababu za msingi,sikua na kosa...walikuwa wengi mno barabarani
Hahahahah nashukuru sana kwa hilo muda muafaka sasa wa kuamsha chombo changu 😂😂😂 afadhali nikomae na mafuta sheli ila sio hawa shenzi waliokuwa wametugeuza shamba labibi
Gazeti la Raia Mwema limeripoti kwamba tayari panga limekwisha tembea, huku MCHEZO WA UPATU waliokuwa wanacheza Trafiki hao kila siku ukibaki njia panda , kwa vile wengi wamepangiwa kazi zingine ambazo haziingizi chochote zaidi ya Mshahara , TAARIFA ZINADOKEZA KWAMBA TRAFIKI WENGINE WALIKUWA NA MCHEZO WA UPATU WA KULIPA HADI SH LAKI MOJA KWA SIKU , ambapo inaelezwa kwamba chanzo cha hela hizo ilikuwa ni Rushwa za barabarani .
Kwa mujibu wa gazeti hilo , Trafiki wengi wanamlaumu Kinana kwa kuibua jambo hilo .
Endelea kubaki JF kwa taarifa zaidi.
PIA SOMA: Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura