Trafiki wapukutishwa barabarani, Vilio vyatawala

Trafiki wapukutishwa barabarani, Vilio vyatawala

Tusuburi ajali za barabarani ziongezeke
Hivi wewe mzima kweli?walivyokua wamejazana barabarani ajali zilikuwepo au hazikuwepo?tena kwa taarifa yako kujazana kwao barabarani na kutufanya mradi wao ndio ajali zilizidi maana walikua wakipoozwa na buku 2 wanaachia hata magari mabovu,jambo la msingi hapa ni tufate sheria na mwenye gari akiwa hajatimia apigwe fine kweli na fine ifike sehemu husika uone kama madereva hawajanyooka.
 
Tusuburi ajali za barabarani ziongezeke
Hakuna kitu ni wapi ukiwa kwenye usafili mkasimamishwa na trafic na kufanya la maana?
Watajifanya wanaingia ndani ya gari, na kushuka huku huku elfu5 au zaidi ikiwekwa kwenye kadi, au inakunjwa kwanye karatasi Kama msokoto wa bangi dreva anasogeza gari ,konda anashuka kumaliza mchezo
 
... teknoloji ina limitations zake; makosa ya barabarani ambayo yanaweza kuwa monitored na teknoloji ni baadhi - speed, wrong overtaking, unpaid fines, expired insurances, stika ya nenda kwa usalama, etc. Kuna mengine yanahitaji human intervention - driving without/expired driving license, kutofunga mkanda, kuendesha bila viatu, kutokuwa na fire extinguisher, kutokuwa na triangles, drunkenness, etc.
Ingekuwa wanafanya kazi kwa uadilifu wasingelalamikiwa na kuonekana ni kero, kwamfano;
  • Kuna sababu gani gari moja, ndani ya mji mmoja kwa safari zilezile, kusimamishwa kila siku na kuombwa pesa
  • Kuna sababu gani magari kusimamishwa kila baada ya Km moja kukaguliwa kila siku magari yaleyale mji uleule
  • Kuna sababu gani gari lilelile kusimamishwa likienda na likirudi nd na askari yuleyule kila siku
  • Kuna sababu gani kuwa na stika za nenda kwa usalama kama gari linatakiwa kusimamishwa kila siku likaguliwe
  • Kuna sababu gani askari kujificha vichakani na kumtaka dereva akaongee nao huko na sio kwenye gari lilipo kosa
 
Gazeti la Raia Mwema limeripoti kwamba tayari panga limekwisha tembea, huku MCHEZO WA UPATU waliokuwa wanacheza Trafiki hao kila siku ukibaki njia panda , kwa vile wengi wamepangiwa kazi zingine ambazo haziingizi chochote zaidi ya Mshahara , TAARIFA ZINADOKEZA KWAMBA TRAFIKI WENGINE WALIKUWA NA MCHEZO WA UPATU WA KULIPA HADI SH LAKI MOJA KWA SIKU , ambapo inaelezwa kwamba chanzo cha hela hizo ilikuwa ni Rushwa za barabarani .

Kwa mujibu wa gazeti hilo , Trafiki wengi wanamlaumu Kinana kwa kuibua jambo hilo .

Endelea kubaki JF kwa taarifa zaidi.

PIA SOMA: Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura
1659769757593.png
Nimehesabu kofia zipo 10 kwa gari moja, tena passo, je lingekuwa bus au lorry zingekuwa kofia ngapi
 
Ingekuwa wanafanya kazi kwa uadilifu wasingelalamikiwa na kuonekana ni kero, kwamfano;
  • Kuna sababu gani gari moja, ndani ya mji mmoja kwa safari zilezile, kusimamishwa kila siku na kuombwa pesa
  • Kuna sababu gani magari kusimamishwa kila baada ya Km moja kukaguliwa kila siku magari yaleyale mji uleule
  • Kuna sababu gani gari lilelile kusimamishwa likienda na likirudi nd na askari yuleyule kila siku
  • Kuna sababu gani kuwa na stika za nenda kwa usalama kama gari linatakiwa kusimamishwa kila siku likaguliwe
  • Kuna sababu gani askari kujificha vichakani na kumtaka dereva akaongee nao huko na sio kwenye gari lilipo kosa
... kwa maana hiyo kutokana na kero za trafiki ulizo taja, trafiki waachane na ukaguzi wa magari na yale makosa ambayo hayawezi kuwa detected na teknoloji yafutwe kwenye orodha ya makosa ya barabarani?
 
Majibu unayo kutokana na unavyowajua
 
Hakuna kitu ni wapi ukiwa kwenye usafili mkasimamishwa na trafic na kufanya la maana?
Watajifanya wanaingia ndani ya gari, na kushuka huku huku elfu5 au zaidi ikiwekwa kwenye kadi, au inakunjwa kwanye karatasi Kama msokoto wa bangi dreva anasogeza gari ,konda anashuka kumaliza mzezo
... Bepari2020 ana hoja; tusimbeze. Tuwe wakweli, eneo linaloenda kuongezeka ajali ni wrong overtaking. Uwepo wa trafiki uliwafanya madereva waogope ku-overtake ovyo ovyo. Dereva haoni mbele kuna nini ana-overtake tu halafu analazimisha kuchomekea; wale wa mabasi mnawajua. Ukimkuta anayechomekewa naye ni m`bishi hiyo tayari ni ajali.

Ni kweli trafiki wana kero zao, ila their presence ina msaada mkubwa kuwafanya madereva wa ovyo ovyo kutokuvunja sheria ovyo hususan zile zenye serious impact.
 
... Bepari2020 ana hoja; tusimbeze. Tuwe wakweli, eneo linaloenda kuongezeka ajali ni wrong overtaking. Uwepo wa trafiki uliwafanya madereva waogope ku-overtake ovyo ovyo. Dereva haoni mbele kuna nini ana-overtake tu; wale wa mabasi mnawajua.

Ni kweli trafiki wana kero zao, ila their presence ina msaada mkubwa kuwafanya madereva wa ovyo ovyo kutokuvunja sheria ovyo hususan zile zenye serious impact.
Sawa si wamepunguzwa tu ,lazima sehem Kama hizo watakua wapeana maelekezo jinsi ya kuzikabili,
 
Huyu alibak na leseni yangu Hadi leo miaka miwili sijaenda kuchukua kosa baulb ya endicator kuungua bila jua alikuwa na roho mbaya zaidi ya shetani
 
Mh. Kinana ongea na IGP amewasahau Tigo wasumbufu sana wanapendelea kua maeneo ya Oysterbay wawili nikiwakuta nitawavizia niwapige picha

Wale uwa wanajifanya ni traffic wanaomba na driving license Kazi Yao ni ipi
Laiti Hamza angefufuka na kusema ukweli Dunia ingezizima
 
Kuna yeyote humu amewahi kukamatwa na trafiki na akalipishwa faini bila kosa lolote? Be honest; yaliyo moyoni kwako wayajua mwenyewe.

Hizo rushwa za elfu 5 au 10 sio sisi wenyewe tunawabembeleza kukwepa kulipa elfu 30? Tunawalaumu kwa lipi kuhusu rushwa? Unless tunalaumu mapato ya serikali kupotea which I don't think kama ndicho kinacholalamikwa na madereva.
Well said kiongozi, sometimes watanzania tunajitoa ufahamu kwa kushabikia serious and sensitive issues kama hii ya kupunguzwa traffic barabarani pasi na kujua negative impact ya ongezeko la ajari barabarani.

Ushauri wangu kwa Jeshi la Polisi ni kutoa maamuzi kwa kujiongeza ("akili za mbayumbayu...") pale yanapotokea matamko na maagizo kutoka kwa wanasiasa.
 
Wahuni wale walikua hawapunguzi ajali Wala nini. Ajali ya gari la wanafunzi Mtwara isingetokea Kama Hawa Wala rushwa wangekua wanakagua magari.

Nimpongeze IGP kwa hatua hii nzuri hasa kumuondoa trafik mmoja wa kike pale Ruvu jirani kabisa na hoteli ya JKT.

Mpangieni Yule mla rushwa kulinda nyumba ya DC wa kike awe anasikiliza miguno usiku.

Aliringa utafikiri daraja la Ruvu kalijenga babake.
Watu wafunguke jamani, polisi walikuwa ni kero, hadi kuhatarisha mustakabadhi WA baadae WA chama chetu ccm, Kwa manufaa ya matumb.. yao!! Hawastahili kurudi, ajali siku zote hutokea Kwa utashi WA dereva na Sio uwepo WA wingi au kutokuwepo askari wapokea rushwa
 
Well said kiongozi, sometimes watanzania tunajitoa ufahamu kwa kushabikia serious and sensitive issues kama hii ya kupunguzwa traffic barabarani pasi na kujua negative impact ya ongezeko la ajari barabarani.

Ushauri wangu kwa Jeshi la Polisi ni kutoa maamuzi kwa kujiongeza ("akili za mbayumbayu...") pale yanapotokea matamko na maagizo kutoka kwa wanasiasa.
Ndugu umepotea sana, hajawahi kutokea wingi WA askari ukawa suluhisho la ajali!! Dereva kuendesha Kwa stress barabarani ndio huongeza wingi WA ajali!! Mfano rahisi Fikiria dereva ambaye anaendesha Gari Huku kabambikiziwa faini ya kosa la onyo!!
 
Wakati mwingine unazitafakari akili za raia wa Tanzania katikati ya tafakuri yako ndio inakujia picha kwanini CCM bado ipo madarakani.

Kwa lugha nyepesi watanzania tuna uwezo mdogo sana wa kutafakari kwa kina na kuchanganua mambo ni kama mtoto mdogo anayepokonywa noti ya elfu kumi na kupoozwa na pipi ya mia akifurahia.
Kwamba una upeo mkubwa!!!...acha hizo jamma yangu,huna upeo zaidi ya kimo Cha mbuzi
 
Back
Top Bottom