... mkuu uliamua tu kuwapa pesa kwa utashi wako; kama kweli hukuwa na kosa ulitakiwa kukataa. Kuna siku natokea Mbeya nimevuka Iringa mahali fulani patamu sana "kuokolea muda" pamenyooka sana karibu kuitafuta Ilula.
Kwa mbali kule nikaona kigari kimepaki pembeni kinatazama upande wa Iringa; nikajua tayari ni wenyewe; sikujali nikachochea. Kuwafikia nikawekwa pembeni ndani wako wanne. Naulizwa hujaona katazo la 50 pale? Nikawajibu hakuna katazo. Nikaulizwa, mbona kibao cha 50 kinaonekana pale?
Nikawajibu, 50 ya uelekeo wa Iringa inanihusu nini mimi nayeelekea Morogoro? Nikaulizwa, hata kama hukuona 50, si pana zebra pale? Jibu, hakuna alama yoyote inayoonesha kukariba zebra. Nilikomaa nao hadi wakanifukuza pale bila kuwapa chochote. Kama huna kosa, kuwa jasiri kama simba watakutimua japo utakuwa umepoteza dakika 10 au 15 hivi.
Tatizo ni kwamba kibao cha 50 ukitokea Iringa kuikaribia zebra kilikuwa hakipo japo just before nguzo bila kibao ilikuwepo hamad nilishaikaribia zebra ilikuwa ni hatari kufunga breki za ghafla and in fact mahali penyewe ni kapori fulani unajiuliza pana sababu gani ya kuweka zebra pale. Ila kwa trafiki tayari kwao ni fursa kuwapiga madereva. Narudia tena, huna kosa be CONFIDENT, usitoe pesa.